Msaada wataalamu wa umeme

Msaada wataalamu wa umeme

Lukansola

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2010
Posts
5,435
Reaction score
1,611
Wadau, eti ni kweli kuwa ubora wa earthroad unaweza kuwa na athari kwenye kiwango cha matumizi ya umeme? naona matumizi yangu ya umeme sio ya kawaida, naweza maliza units 5 kwa 24 hours. Ndio jamaa mmoja akaniambia kuwa inawezekana earthroad ni fake.

Naombeni msaada wa ushauri tafadhali.
 
Inawezena live wire imechunika na inagusa earth wire hivo kupoteza umeme kupitia earth leakage. Pia vifaa yva umeme vibovu vinaweza kuchangia upotevu wa umeme.
 
Icho kitu inawezekana,nakushauri kwanza zima main switch halafu kaa kama kama masaa matatu then angalia unit zitakwenda,zikienda inawezekana wiring yako ikawa cyo nzuri,Inashauriwa ukaguzi wa wiring ufanyike kila baada ya miaka mitatu
 
yes nayo ni sababu pia ya kupotea umeme!.
kama utataka msaada zaid wa fundi ni pm nikupe fundi mkongwe akusaidie kugundua kama kuna kingne zaidi.
 
simplemind, mazina, faabroz asanteni sana kwa ushauri wenu, wakati nafanya wiring jamaa aliniingiza mjini akanifungia earthroad ambayo sio copper bali chuma kilichopakwa rangi ya shaba, faabroz, asante nitakutafuta nikizidiwa.
 
Last edited by a moderator:
hapana ubovu wa earthroad hauchangii matumizi makubwa ya umeme.

kama earthroad yako iko vizuri sana na imegusana na Live , basi umeme utatumika bila wewe kujua (Earth leakage), hii humaanisha kwamba Earthroad inapogusana na live ni sawa sawa na kufunga kifaa cha umeme somewhere bila wewe kujua. kama wiring yako iko vizuri(nikimaanisha hakuna wire zilizochubuka na kugusana, na pia connection zipo correct)
Basi earth leakage inaweza kusababishwa na ubovu wa vitu vinavyotumia earth connection kama vile fridge, jiko la umeme, computer(desktop),Air conditioner,etc etc. Hivi vitu vinaweza kuwa na ubovu unaosababisha kugusana kwa Live na Earth. Na endapo Earth itagusana na Live basi umeme unatumika. Kiasi cha umeme utakaotumia kapo utaongezeka kulingana na Ubora wa earth road yako.

Wadau, eti ni kweli kuwa ubora wa earthroad unaweza kuwa na athari kwenye kiwango cha matumizi ya umeme? naona matumizi yangu ya umeme sio ya kawaida, naweza maliza units 5 kwa 24 hours. Ndio jamaa mmoja akaniambia kuwa inawezekana earthroad ni fake.

Naombeni msaada wa ushauri tafadhali.
 
Wadau, eti ni kweli kuwa ubora wa earthroad unaweza kuwa na athari kwenye kiwango cha matumizi ya umeme? naona matumizi yangu ya umeme sio ya kawaida, naweza maliza units 5 kwa 24 hours. Ndio jamaa mmoja akaniambia kuwa inawezekana earthroad ni fake.

Naombeni msaada wa ushauri tafadhali.


ni lini umeanza kupata hili tatizo..?
kabla ya kupata hili tatizo umelikuwa unatumia unit ngapi. kwa hayo masaa.?
na huu utafiti umeufanya kwa muda gani wiki mwezi ..? hayo

umeshawahi tetemeshwa na kifaa chochote cha umeme mfano pasi,jiko fridge et.c
una used fridge isiyo na thermostat / temperature controller..?
kuna ELCB/earth leakage circuit breaker kwenye nyumba yako na iko active..?(ile karibu na main switch)
inafanya kazi fresh..?
wiring yako ina muda gani..? imefanywa muda muda mrefu sana..?

samahani maswali mengi sana ila yanaweza kukupa mwanga fulani kama unaweza nisaidia kuyajibu ..
na mimi naweza ongeza somo kidogo
 
Back
Top Bottom