Msaada: Wataalam wa kutoa mwiba

Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,293
2,000
Heshima kwenu wakuu.

Nimechomwa na mwiba mguuni kwenye unyayo. Nimejitahidi kuutafuta ili niutoe nimeshindwa kuubani. Maumivu makali sana. Leo ni siku ya 3.

Ni wapi nitapata wataalam waubaini kisha utolewe? Yaelekea ni mwiba mdogo sana maana siuoni lakini nauhisi kutokana na maumivu ninayoyapata.

Naombeni msaada.
 

Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
10,338
2,000
Pole sana mkuu japo nilijua unasema kutoa mimba

Anyway

Nenda hosp wakuchane wakutoe mwiba.

Aubosha mguu vizuri, kama una unyayo mweupe mwiba utaonekana utachana na wembe na kuutoa
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,770
2,000
Mkuu nenda hospital achana na wanasema watakucheka mzaa mzaa hutumbua usaa.. Kuna tumwiba tudogo tu lkn huwa na sumu ukipuuza utakaeumia ni wewe.
 

King Sae

JF-Expert Member
Mar 22, 2018
1,583
2,000
Tafuta mafuta ya mgando (ya kujipaka) weka donge dogo unapohisi mwiba uliingilia kisha tafuta mkaa wa moto anza kuchochea hapo hapo kwenye kidonda!! Dakika 2 mbili nyingi mwiba unajichomoa!!!
NB: KUNA MAUMIVU KIDOGO, SO JIANDAE KUYAVUMILIA
KWA jinsi anavyoonekana hii huduma labda afanyiwe na mtu mwingne kwa usimamiz maalumu mana maumivu yake nayajua..
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
20,120
2,000
Heshima kwenu wakuu.

Nimechomwa na mwiba mguuni kwenye unyayo. Nimejitahidi kuutafuta ili niutoe nimeshindwa kuubani. Maumivu makali sana. Leo ni siku ya 3.

Ni wapi nitapata wataalam waubaini kisha utolewe? Yaelekea ni mwiba mdogo sana maana siuoni lakini nauhisi kutokana na maumivu ninayoyapata.

Naombeni msaada.
Uache utunge usaha siku pakiiva ukibinya unapanda hapo speed hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom