Msaada wa kitabibu

Tobechukwu

Senior Member
Oct 15, 2018
112
415
Habari za leo wakuu, natumai mmeamshwa salama.

Nimekuja kwenu naombeni msaada wa kitabibu, nasumbuliwa na tumbo la chini la uzazi linaniuma sana mwezi wa pili sasa hasa upande wa kulia mpaka kiunoni kwa nyuma. Nilienda hospitali nikapimwa mkojo wakasema mkojo hauna infection yoyote.

Nikapimwa Ultrasound nikaambiwa kuna fluids, ila kwa vile nilitoka kumaliza period jana yake nikaambiwa nisubiri siku 7 zipite nirudi tena kama itaendelea kuepo au la nikarudi nyumbani na pain killer tu.

Ila maumivu yanazidi kuwa makali na saiv nakua naumwa yanaenda hadi mguu wa kulia upande huo huo tumbo linapouma, Kuhusu vagina discharge siielewi pia kwanza toka period inatoka kama makamasi na saivi bado inatoka kama makamasi na ina rangi ya cream kuelekea njano ila hauna harufu.

Nimeambatanisha na picha.

20221209_101800.jpg
 
Pole sana mamy mtafute huyu mama wa kihaya 0768890586 mueleze kila kitu unavyojisikia ana dawa za magonjwa ya kina mama nzuri sana
 
It's so sad kuishi nchi yetu, hasa linapokuja tatizo la kimatibabu, umasikini wetu ndio tatizo ila hapa ulitakiwa ufanyiwe vipimo vya xrays vya kueleweka,sip hivi vya kimchongo pia ulitakiwa uonane na madaktari bingwa sio GPs wetu, kama una nguvu kusanya pesa kidogo then panua wigo wako wa kutafuta matibabu bora zaidi, good luck
 
Alisema hamna cyst ovaries ziko poa, mi pia nilijua itakua hiyo imeruid maana ilinisumbua 2019 ila iliisha.
Walikupatia matibabu 2019?

Ushauri onana na Gynaecologist pia rudia kipimo sehemu tofauti na uliofanya awali....

Uponyaji mwema kwako mkuu
 
Walikupatia matibabu 2019?

Ushauri onana na Gynaecologist pia rudia kipimo sehemu tofauti na uliofanya awali....

Uponyaji mwema kwako mkuu
Ndiyo nilipatiwa na baada ya kumaliza dozi nilirudi tena kupia nika ambiwa imeisha nikawa sawa.
 
Habari za leo wakuu, natumai mmeamshwa salama.

Nimekuja kwenu naombeni msaada wa kitabibu, nasumbuliwa na tumbo la chini la uzazi linaniuma sana mwezi wa pili sasa hasa upande wa kulia mpaka kiunoni kwa nyuma. Nilienda hospitali nikapimwa mkojo wakasema mkojo hauna infection yoyote.

Nikapimwa Ultrasound nikaambiwa kuna fluids, ila kwa vile nilitoka kumaliza period jana yake nikaambiwa nisubiri siku 7 zipite nirudi tena kama itaendelea kuepo au la nikarudi nyumbani na pain killer tu.

Ila maumivu yanazidi kuwa makali na saiv nakua naumwa yanaenda hadi mguu wa kulia upande huo huo tumbo linapouma, Kuhusu vagina discharge siielewi pia kwanza toka period inatoka kama makamasi na saivi bado inatoka kama makamasi na ina rangi ya cream kuelekea njano ila hauna harufu.

Nimeambatanisha na picha.

View attachment 2440445
KUTOKWA NA UCHAFU UKENI.jpg

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI VAGINAL DISCHARGE)

Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano.

Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama Vaginosis.

Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla.

Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni:

Kuwa na wapenzi wengi
Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali
Uchafu
Uvutaji sigara
Pombe
Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni

Dalili

Kutokwa na uchafu usio wa kawaida
Kutokwa na uchafu wenye harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza
Kuwashwa sehemu za siri na ndani ya uke
Uke unaweza kubadilika na kuwa na rangi nyekundu
Maumivu sehemu za siri wakati wa kukojoa
Maumivu makali chini ya kitovu
Kutokwa uchafu uliochanganyika na damu

Matibabu

Mara uonapo dalili hizo unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa vipimo zaidi na dawa zaweza kuwa ni za kunywa au za kupaka.
Tumia dawa za hospitali kama hujapona nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako .
 
Habari zenu wakuu, napenda kuwashukuru kwa ushauri wenu, nilishapata tiba ya tatizo. Nilirudi tu hospital kwa dr mwingine, ambapo niliambiwa PID nikachomwa sindano moja na kupewa dawa zingine namshukuru Mungu nimepona nipo vizuri saivi.
 
Pole sana mamy mtafute huyu mama wa kihaya 0768890586 mueleze kila kitu unavyojisikia ana dawa za magonjwa ya kina mama nzuri sana
Shunie, huyo mama wa kihaya nilimtafuta, nikajielezea weee, akanijibu ''tiba utapata kwani si unaumwa hormone imbalance'' nikachoka nikamjibu tu nitakurudia hapohapo nikaamua tu kwenda hospitali.
 
Back
Top Bottom