Ngoja niicheki hii itakuwa imekaa poa
Kwa ufupi fata hizi steps
1.shikilia Ctrl na shift kwa wakati mmoja kisha bonyeza enter (kubonyeza enter inabidi uendelee kuzishikilia hizo Ctrl na shift, hapo itatokea nafasi ya kuandika
2.andika cmd, hapo inaweza kukuuliza km unataka kuwork km administrator jibu yes kwa kubonyeza yes kisha bonyeza enter
3.andika diskpart kisha bonyeza enter (usiache nafasi kati ya neno na neno).
4. List disk kisha bonyeza enter
Utaona disk ziko listed hapo
5.select disk 'x' (hiyo x namaanisha utachagua namba utakayoona inawakilisha flash disk yako, mara nyingi utaijua kwa kuangalia capacity maana flash disk itaonekana kua na capacity ndogo interms of mbs tofauti na computer, so utachagua km ni namba 1au la.
6.andika clean kisha bonyeza enter
7.andika create partition primary kisha bonyeza enter
8.andika select partition 1
9. Andika active kisha bonyeza enter
10. Andika format fs=ntfs quick kisha bonyeza enter
Hapo utaona inahesabu asilimia hadi zifike 100, ikimaliza bonyeza enter iliufanye hatua ya 11
11. Andika assign kisha bonyeza enter
12.andika exit (hatua hii sio lazima kivile unaweza kuipotezea tu).
Kumbuka hatua namba 3 ndio hutaacha nafasi kati ya neno na neno, hatua zingine utaacha nafasi kama unavyoona nimeandika hapa).
Ukikwama tafuta msaada kwa binadamu au ingia google.com