Msaada WanaJF: Biashara ya BAR Dar es salaam

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
wanaJF siku zote nimekuwa nikitaka kujikomboa mimi kama mdada
kwa kujishughulisha na biashar nyingine tofauti na kazi yangu.

Siku zote nimekuwa na hamu ya kufanya biashara ya Bar lakini mimi sinywi pombe yoyote

Sasa nimepata mtaji nataka kuanza biashara hii ya bar kwa maeneo ya Dar es salaam

Swali langu:

1.Je ni utaratibu gani inabidi nifuate ili niweze kuanza?
2.Ni vitu gani vya kufanya ili kuvutia wateja? hapa location yake nimeishapata ni nzuri
3. Je Biashara ya bar kuna unafuu wa kupata faida kidogo? maana makadirio yangu
ni kupata kama laki 2-3 kwa siku
4. Mtaji wangu ni 20million, Je huu inatosha kwa kuanzia?
 
2.Wauzaji wawe akina dada warembo kama wewe, jiko la uhakika na burudani mbalimbali kama pool table
 
Adui mkubwa wa biashara ya Bar ni huduma mbovu dada yangu. Unajua ladha ya bia ni ile ile na bei ni almost zile zile kwa bar nyingi sasa jiulize kwanini bar zingine zinajaa na zingine hazijai kabisa. Mtu yuko radhi atoke kazini posta apite Calabash alafu ndio aende home Gongolamboto au Temeke. Wadada wauzaji wanachangia sana tena kuvuta au kufukuza wateja......
 
Fadia ya laki mbili tatu kwa siku? Hah hah talking about 9m per month? May be . And that may be a reason fro quitting your 2 m job. Kila la kheri
 
Nimesimamia biashara ya baa kwa muda mrefu najua mengi nipigie tuongeee 0755394701
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom