ndugu mtoa mada kwanza kabisa makosa uliyoyaleta hapa hayatoshi kukufanya uachane ama utengane na mumeo. kimsingi kabisa hapa hakuna kosa ila naweza kusema ulitaka tu kujua wengine tunalichukuliaje.
Ukweli ni kwamba huyo mdada kumwita mumeo mpenzi inawezekana ni mpenzi wake kweli ama sio nasema sio kwani kuna watu ambao wanahualka ya kuwa na maneno ama majina matamu kwa watu wengine. mfano mimi binafsi huwa ninatabia ya kumwita mtu kaka yangu wa moyoni ama dearest ama mpendwa wangu ama mpenzi lakini kamwe hunikuti namwita mtu dear wangu hili liko served for huzzy. sasa wewe huyu kumwita mumeo mpenzi yaweza kuanguka kwenye hayo makundi mawili.
sikatai kama ni mpenzi wa kweli inaumiza sana lkn mpaka sasa bado huna proof so bado ni suspicious tu ambazo zaweza kuwa kweliama uongo.
istoshe swala la uroda kutolewa mara mbili kwa mwezi basi kosa ni lako mwenyewe. labda nikuulize wajua kuitafuta network wewe kama haipatikani?? je umeshajaribu kuona unahitaj king'amuzi gani kwa signal zilizoko?? mwenzio pengine signal zilizoko ni short wave wakati yeye anataka long wave inakuwaje??
ulishakaa nae chini mkaelezana juu ya hali halisi?? ulishajaribu silaha zako zote za maangamizi za kike ukashindwa?? kumbuka silaha za maangamizi za kike zina nguvu inayoweza kumfanya hata jitu kama samsoni akawa kama mwana mpotevu, tena zina nguvu kuliko upanga as zinaweza kubadili ulimwengu kwa sekunde.
hivyo kama huji kuzitumia njoo uombe ushauri utapatiwa ila mwanamke kukosa kupewa uroda kabla ya kulalamika pima silaha zako za maangamizi kwanza.