Msaada : Wali wa jiko la gesi

Hata mimi nafanya hivi unakauka vizuri sana
 
ina maana mkuu ukiwasha jiko moto ni huo huo mwanzo mwisho?
ahahaa pole sana
maji yakishakauka unageuza mchele halafu unaweka moto mdoogo mpaka ulainike kabisa.
ila wali wa gesi sio mzuri kama wa mkaa au umeme
 
Ukishaweka mchele punguza moto mpk mwisho maji yakianza kauka tafuta mfuko wa nailon uoshe ufunike wali na mfuniko unaiva na mvuke
Nailoni????
Mbona hamjipendi?

Kansa nje nje

Heri ungemwamhia afunike kwa foil
 
Ukishanunua mchele wa kutosha ule super kabisa, weka ndani hakikisha hamna wadudu waharibifu, kisha oa mke halali wa ndoa, kuanzia hapo we shinda sebulen nakuapia wali wa jiko la gesi utasahau usumbufu wake.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
sio lazima maji ya moto hats ya baridi, ukishaweka mchele weka maji ya baridi funika uchemkeee, ukiona maji yanapungua punguza moto kabisaaaaa then funika, ingia jf uchart kwa nusu saa,
 
Nimezoea kupika wali jiko la mkaa hapo zamani .. Sasa nimeanza kujipikia mwenyewe tatizo Nikipika wali kwa jiko la gesi ukianza kukaukia nikiutoa either utakuwa umeungua au mbichi hauliki.. Nipeni mbinu za timing ya kuuivisha vizuri.
Me sijui ushamba, huwa maji yakishakauka nna kifuniko fulani imara sana cha chuma, napunguza moto kisha naweka hicho kifuniko katikati ya moto na sufuria kisha naendelea na shughuli zangu yaani wali unachambuka vzr sana. Nafanya haya hata kwenye jiko la mchina

si ni bora maji yakiisha aumwage kabisa juu ya moto wa jiko
 
Ukishaweka mchele punguza moto mpk mwisho maji yakianza kauka tafuta mfuko wa nailon uoshe ufunike wali na mfuniko unaiva na mvuke
Hii ya mfuko wa nailon hapana, mfuko huo si salama kwa Afya , mengine yes
 
Mimi nikiwa na haraka zangu hupika wali kwenye jiko la gesi pia, hupendelea kuukaanga kwanza nikishaukaanga naweka either tui au maji ya vugu vugu au ya moto naweka maji kiasi tu yaan sentimita chache toka ulipoishia mchele(hapa hutegemeana na ugumu wa mchele wenyewe) kisha napunguza moto mpka chini kabisa yaani kama nataka kuuzima vile huu moto nnaoacha ikitokea upepo ukapuliza kwa nguvu huweza kuzimika nafunika wali wangu alafu naendelea na issue zingine Epuka kugeuza geuza chakula chako kwani Mchele huvunjika vunjika ukitaka wali mnyoosho ulionyooka usigeuze geuze kila wakati, maji yakikaukia na kubaki kwa ndani nageuza chakula changu nakifunika na kukiacha kiive
 
Kama hupendi usumbufu nunua pressure cooker.Binafsi huwa inanisaidia sana maana hakuna mambo ya kugeuzageuza wala kuhofia kuunguza.
 
Race cooker ndo mnyama gani?
 
Kakwambia ye ni mwanaume?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] uyo mnyama ukimjua na mie ntajie usikute ni kitoweo kipya hapa mjini
[emoji13] [emoji13] [emoji13] hebu tusubiri majibu kutoka kwa mhasibu
 
Race cooker utakua humtakii mema huyu ndugu yetu unataka ageuze wali kuwa Ferrari ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…