Msaada wakuu kwa waliosoma advance

Msaada wakuu kwa waliosoma advance

Mtu akikuambia kitu fulani ni kigumu! fikiri kwanza! Ugumu ni kwao! wewe ulijaribu lini ukajua ni ngumu! mimi sijasoma PCB nimesoma PCM leo naona PCM ni dililess! kakomae uache bata uache upumbavu wote! ni rahisi kufaulu! utakuta mtu na div 1.7 uko nae lkn anajiamini na div yake! usiwasikilize wala kufanya mambo yasiyo ya maana nao! maisha sio history maisha ni sasa! Mimi nikutume ukomae sana!!!
 
Nenda kasome weka bidii sana hasa kwenye physics.... Nakumbuka physics tulikuwa tunafundiswa swali kabla ya paper kama wiki kadhaa kabla na ilo ilo linaletwa kwenye paper lakini bado unatoka kapa... Apo ndo nilipoona physics inaitaji kurudia kusoma mara kwa mara...mambo ni mengi but ukijipanga unatoboa. Sema usisahau kuna maisha pia enjoy kiasi ii itakufanya uipende shule. Jitaidi kupanga mambo yako.
 
Nikikumbuka maisha ya A Level nakosa hata cha kusema

Anyways kasome kijana.Ukisoma vizuri utafaulu
 
Wakuu msaada naombeni ushauri lengo langu kusoma Mchepuo wa pcb kwa sasa nasubiria post nijiunge na kidato cha tano ila kuna feedback nimekuwa nikipewa ya kuwa haujasoma tuition hasa kwa shule za goverment inakucost kwa kuwa hamna walimu sasa ninaomba msaada wa ushauri juu ya usomaji wa Mchepuo hili niweze faulu vizuri
hujachelewa anza kupga msuli kwa sasa maana hyo si ya mchzo unapaswa ukate topc mapema ili uwe fiti mapema
 
Hata uende shule ambayo wanafundisha bila juhud zako binafsi A level achana nayo nenda chuo tuu
 
Nikikumbuka maisha ya Advance siamini nilichomokaje bila zero. Hakuna kitu kigumu wala kirahisi, juhudi zako binafsi na kujua nini unataka ndio vitakavyokutoa kwenye final. Ukweli kabisa Physics sio rafiki kabisa bora Chemistry kuna topics ukiziweza umeweza. Nakutakia mafanikio mema ila asikitishe mtu ni ngumu mbona mi mwanamke niliweza we mtoto wa kiume huwezi kushindwa kitu.
 
nimesoma shule. hizo bt cha muhimu ni msuli binafsi coz mwalimu ata akiingia darasani hakuna tofauti na. asipoingiaaa piga tuit soma discus utatoka tuu
 
huko utafeli dogo kama ndoto zako kuwa dokta fanya hivi apply college za afya za serikalini usomee medical officer ngazi ya deploma miaka 4 na clinical assistance ngazi ya cheti miaka 2 tu ada haizidi laki 5 kwa mwaka na ukimaliza tu unapangiwa kazi iwe zahanati au hospitalini
 
mkuu sikufichi usimtegemee mwalimu japokua utaingia vipindi vyake vyote. achana na madem michezo kama kweli unaisaka division one kwa sisi watu wa Mwenyezi-Mungu huwa tunasali kwanza na kumtanguliza baba tafuta marafiki wakupige pindi na kukusaidia maswali tuition nenda narudia tena soma sana acha maringo hata kama ulitoka na division 1 ya point 7 zero utaipata tuu kichwa kikiwehuka advance ni levo nyingine man usijione mjuaji. mwenzio nimetoka huko sema sikupata ushauri hata nisingeenda uko sababu nlikua napenda course za afya udaktari, famasi na maabara kilichonikuta nakupa siri nimemaliza 2015 ufaulu wa BRN ulikua mkubwa sana sikuweza kupumua vyuo vya serikali nniliishia kuviskia na kuviona mtandaoni tuu hata private kama bugando nako hali ilikua tete pcb wengi walienda education
wengine wakaenda bachelor of veterinary medicine sua wengine course za ajabu ajabu. tuu kama family consumer, forestry, fishing n.k out from. udaktari????
man pambana rafki ushauri huu nakupa kama nipe yako pm nikupigie kwa msaada zaidi pia anza kusoma kwanzia dakika hii kwa uchungumambk. mazuri hayaji hivi hivi.
summary ya vitu vyote hapo juu kama unapenda kwenda ile. sekta yetu pendwa ya afya kwa vyuo vya serikali ni. lazima upate division 1 ya kwanza hadi point 5 hapo ndo unakua na uhakika wa kuzama MUHASI, UDSM, UDOM, KCMC, BUGANDO, halafu sijui IMTU, ARCHIBISHOP JAMES SONGEA, KAIRUKI ST FRANCIS YA MOROGORO kule division 2 pia hata 3 unapata bila tatizo lolote ila omba ukute ufaulu ni mdogo hivyo ushindani ni mdogo pia nakwambia kwa six yetu ya 2015 mambo yalikua magumu sana wengi walienda education na diploma za clinical officer na nursing kabisa.
man kama vipi unaona uwezo wako ni wa kawaida tuu au wastani PLEASE usiende advance ni kupoteza mda tuu. ndugu kama wataka sekta ya afya nenda diploma matokeo yakp naju yanaruhusu ni miaka 3 tuu ukimaliza unaaajiriwa fasta tuu halafu baadae un miaka miwili au mi3 unaenda zako bachelor ila huko diploma pia uwe na GPA kubwa usipumbazike mambo ni magumu ushindani upo. ni hayo rafki yangu sijui mdada au mkaka nimekutambulisha kama man kama kuna tatizo samahani. ni hayo tu man Mungu akutangulie sasa ushajua mchele ni upi na pumba ni zipi we chagua kimoja. kwa maoni zaidi nipe namba yako pm tuongee.
naoma moderator wa hili jukwaa aiweke hii post mwanzonk ili kila atakae fungua huu uzi aione ni mmsaada mkubwa mnk kwa ndugu zetu wanaotaka kwenda advance au diploma.

natanguliza shukrani.
 
Dah umenikumbusha mbali hiyo Pugu 2006 egm nikiwa na watabe kibao rip mashineeee mtabe from kilombero k1
 
Back
Top Bottom