Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,163
- 37,801
Mshkaji kamtongoza my wife. My wife kapiga kimya, asinambie. Yamenikuta wa ukae.
To cut the long story short, nna rafiki yng ambae tulikotoka mpk hapa tulipo, inatosha kusema ni ndg.
Ghafla mshikaji wangu ananikwepa, hataki tena ukaribu na mimi (feeling guilty). Wife anapotezea mada yoyote ninayoanzisha kuhusu mshikaji, hachangii na akichangia, anaishia kunambia “si kila rafiki ni wa kumleta nyumbani kwako”. Huwa namjibu, mbona nna marafiki wengi na hata nikiamua kuwaleta wote nyumbani, ntakufa bila hata kutimiza nusu yao!
Lakini nikimbana zaidi, kulikoni, kwa rafiki huyu tu, ndio aseme: “si kila rafiki ni wa kumleta nyumbani!” huwa anakuwa mpole mpaka namuonea huruma, anaonekana anataka kufunguka lakini kuna kitu anasita!
Huyu rafiki in rafiki ambae nilishamqualify kuwa ni ndugu, ni mtu wangu wa ukweli, ni mmoja wa watu ambao mpk safari ya maisha imenifika hapa, nimesimama, ana mchango wake, ni rafiki ambae alikuwa tayari kudraw kutoka ac yake, akanilipia ada chuo, na nikamlipa mdogo mdogo huko mbele ya safari, tena bila kusukumwa, ni rafiki ambae alikuwa radhi atoke mkoani kwake, na mimi nitoke mkoani kwangu, tukutane chuoni, ili tu anipigishe msuli, nichomoe sup! Lakini yapo maeneo ambayo nimemuonyesha uungwana ambao kama hutujui unaweza sema sisi ni ndugu.
Hata wakati nna wakati mgumu wa kuchagua kutoka multiple choices za yupi nioe, huyu rafiki nilimshirikisha huku akiwa hamfahamu mtarajiwa! Alija kumfahamu baada ya ndoa. Kiubinadamu nashindwa, ntampataje na kumuuliza, nini kimempata?
Siwezi kumfata ofisini kwake -jamaa ni mzee wa kambi, siwezi mfata home kwake, ana mke ambae tunaheshimiana sana! Nisingependa haya yafike kwa mkewe.
Nashindwa kumuuliza kuna nini kati yake na shemeji yake? Hapokei simu zangu? Hajibu sms, siku hizi hata nikimtumia zawadi hapokei (kila mmoja wetu akisafiri, safari ya kikazi lazima amletee mwenzie kazawadi kutoka huko alikokuwa), amesharudisha pair of boot niliomnunulia kama zawadi, (hii nilimpa rafiki yake ampelekee) iliniuma sana!
Taarifa za kiintelijensia (naomba nikiri, za upande mmoja tu, za upande wangu) inasemekana mshikaji alijaribu gia namba moja kwa yf wangu, ikagoma! Kabla hawajafika angani, akaingiza gia namba 2, ndio naambiwa akaharibu kila kitu, mbaya zaidi ni nyumbani kwangu, mimi nikiwa safari!
Njiapanda: nauona urafiki wetu na mshikaji unaelekea ukingoni, tena kizembe zembe sana! Huu ni urafiki uliodumu kwa 15 yrs! Siko tayari kwa hili! Natamani suluhu kati yangu na mshikaji, lakini vipi furaha ya wife baada ya urafiki wetu na jamaa kurudi upya? Wife kuna kitu kinamuuma ndani kwa ndani, ni ipi njia sahihi ya kumsaidia?
Kimsingi huwa namuomba mungu aniepushe na majanga lkn linapokuja suala la kupigania ndoa yng, huwa napambana mpk dk ya mwisho!
Waungwana naomba mtie neno hapa, mamsap hana raha, rafiki yng nae anankwepa, wote wawili wananiweka njiapanda!