Sazira kwetu
Senior Member
- Aug 23, 2015
- 155
- 104
Habari za mda huu wana jukwaa?
Namshukuru Mungu kwa kunifikisha siku ya leo nikiwa mzima wa Afya njema.
Naomba msaada wa mawazo au uzoefu katika swala hili la zawadi kwa watoto wetu wapendwa.
Mwanangu ni mtoto wa kiume mwenye umri wa Mwaka mmoja na miezi Miwili hujaanza kuongea vizuri ila ukimtuma kitu kwa kuonyesha kidole nenda kaniletee kile au hiki analeta na kwa bahati nzuri aliwahi kutembea akiwa na miezi 8 kwa hiyo anauwezo mkubwa wa kutembea na kufanya michezo yote ya kitoto ambayo inaendana na umri wake.
Wazazi wenzangu naomba msaada wa kimawazo Je nimnunulie zawadi gani itakayomfaa kwa umri huo na kuendelea?
Kwa sasa niko Dar es Salaam mpaka mwezi wa Saba ambapo ninatarajia kumaliza masomo yangu ya chuo Kikuu. Bajeti yangu haizidi laki mbili.
Natanguliza shukurani zangu zote kwa wanajukwaa wote.Zawadi ninazozitaka ni zile zenye kujenga na kumfikirisha ili akue akiwa mtoto mdadisi na mwelewa.