Msaada wa Ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa Ushauri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kiroroma, Feb 18, 2009.

 1. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Wana-JF,Naingia hapa jamvini kama mdau mchanga sana,Kwenu naomba ushauri wa janga hili;Shoga yake na wife ambaye ni jirani yetu hapa maskani alinikamata mguu miaka kama mitatu imepita kwa kisingizio kwamba ndani kwake hapati huduma stahili.Anaye mdau kama mimi ila nililong'amua ni kwamba mdau kazi zimemzidia na kinywaji sana.Sasa sihitaji kuendelea na maisha haya.Nimempa mpango huo live haelekei kuelewa ndo kwanza anaweka shinikizo kali na mkwara kibao.Nimekata mguu lakini hataki kuachia ngazi.Hanigharimu kitu chochote kwa maana ya mali au hata fedha lakini dhamira yangu inanishtaki sana.Uhusiano wa kifamilia ni mzuri kabisa wife hata fununu hana!Kwani shoga ni msiri hata kuliko Misri,hafanyi kosa yeye shida yake kubwa huduma tuu.Nifanyeje wajemeni?Roho haitaki tena udhalimu huu.
   
 2. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Uliyataka endelea kuyaoga
   
 3. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Hapo imekula kwako maana umeshakubali kukamwatwa mguu na huyo shoga hataki kuuachia. Lazima ukubali kwamba ulikosea sana tena ni rafiki wa mkeo,hujui tu inavyouma kula na kipofu tena akijua itakuwa balaa.
  Tayari umeona kuwa ukitaka kusitisha anakuwekea mikwara hiyo ina maana ipo siku vitu vyote vitajulikana kwa wanandoa wenzenu hata kama huyo shoga ni msiri kama misri.
  Jaribu kumwambia huyo shoga kuwa mkeo anahisi kuna kitu kati yenu, hivyo mpunguze na kuacha kabisa kushikana miguu polepole ikiwa atakuelewa maana naona mwisho wenu utakuwa wa shwari kwavile shoga hataki kukuachia.
  Wakati mwingine mtu unapotaka kufanya kitu ni vizuri ukaangalia mbele na kufikiri jinsi hicho kitu kina faida au hasara gani. Kama hapo sasahivi inaonekana umekosa amani na unataka kitu hicho kiishe ila shoga ndo kanogewa.
  Pole sana ndugu!
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  kamua mzigo kamanda........
   
 5. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Belinda Asante kwa ushauri wako wenye kutoa mwelekeo wa kimaadili,Hatua hiyo ndo inashika kasi kwa sasa,Haiashirii mafanikio sanaa sijui kwa baadaye.Kwetu ni kwenu nakushukuru kwa jibu lako lisilo na tija,YoYo masihaara kwenye dhiki ya ushauri wa kina si mchezo mzuri.Kama ushauri wenye kutoa ufumbuzi hakuna basi kaa kimya.
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Huna uaminifu kaika ndoa yako. Huna mapenzi ya dhati kwa mkeo. Ungekuwa navyo hivi usingekubali uasherati wa shoga wa mkeo. It is a shame!!!! Ni kufuru hiyo kaka/dada!!!!

  Jua hakuna siri duniani. Siku moja mkeo ataipata taarifa ya ku cheat kwako huko tu.
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280

  Maane nadhani huyu bwana ameshaona hayo hapa ametaka ushauri, tusimhukumu ki hivyo hayuko peke yake katika hili

  Nikirudi kwako kwenye mada,, mkuu nakushauri uende naye pole pole yaani upunguze taratibu ukifanya chap chap hakitaeleweka, ndo njia pekee manake hapo tayari ni mashoga. mweleweshe taratibu huku ukienda aste aste tu ataona tu kuwa huna deal atafute mwingine
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...baada ya miaka mitatu? kwanini hutaki kuendelea naye?

  ...ndio maana nikakuuliza hapo juu, baada ya uhusiano wenu mkiaka mitatu na ushee, kwanini hutaki tena kuendelea naye?

  ...baada ya kula hilo tunda kwa muda wa miaka mitatu? umegundua nini? tupe darasa ndugu yangu

  ...WRONG!... nakupa 51% kwamba mkeo anajua kinachoendelea, na 49% Mkeo atakuwa ana cheat na huyo 'mdau', unabisha? soma maelezo yako hapa chini...

  ...Confess kwa mkeo, mbele ya mdau na huyo madame-Jirani. 'udhalimu' huo hautorudiwa tena.
   
 9. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mkuu Mbu nakushukuru kwa analysis yako na ushauri pia labda hukuweza kuainisha tatizo linalonikabili kikamilifu.Ujue kuwa ni jambo la watu wawili nami mmoja ndiye nataa kujitoa!!Upande wa pili hautaki!!Sasa ukilipeleka mbele ya Mdau Mkuu yaani My Wife nitakuwa nimemhukumu huyu Shoga Jirani na kusababisha kujenga uadui.Jambo nisilolitaka.Bado upembuzi yakinifu haujafanyika juu ya mahusiano haya.
   
 10. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ndio maana niligomaga kuwa na kiumbe anaeitwa "shoga" maishani mwangu, hamjamtendea haki kabisa mama wa watu, mume na rafiki yake wa karibu ndio mnataka kuifinya roho ya mama wa watu kwa kiasi hicho? kwa miaka 3? yaani sijui siku huyo mama akigundua itakuwaje? alwayz "kikulacho ki nguoni mwako."

  yani sasa hivi ndio umezinduka usingizini unaona ulivyofanya si haki? haya sasa asikutishe kwa hili wala lile mana wote hapo mmecheza rafu mwambie nimeamua kusitisha huduma coz wife ameshtukia kitu na sitaki gogoro na mama watoto wangu, mchezo umeisha asikutishe nini wala nini mana kwa jinc mnavyoendelea na ndio uwezekano wenu wa kubambwa unakaribia, haaa
   
 11. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Anti Nyama Yao hayo yoote uliyoyasema ni kweli tupu wala sipingi kitu,Lakini ujue janga halina mganga,Sasa hatua uliyoshauri ndiyo nimechukua na hapo ndipo tulipo lakini bado kungali na mashauriano yasiyoisha kwa muda wa mwezi sasa NDO maana nipo hapa jamvini kwa nasaha zenu Wakuu wa mashauri mazito ya kijamii .
   
 12. B

  BeNoir Member

  #12
  Feb 20, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama umeshaamua kuacha na umemtaarifu, ni lipi tena linaendelea? Mnajadiliana nini tena?
  Hebu wewe kaa mbali uone atachukua hatua gani ya ziada.
  In the meantime, anza kujitayarisha incase bomu linalipuka.
  There are consequences for every action, but still its not the end of the world.
   
 13. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  unajua sikuelewi unashauriana nae nini, kwani mliwekeana mkataba?naona hujipendi/hupendi family yako, atleast now hata huyo shoga akiamua kumwaga mtama kwenye kuku wengi (ambayo sio rahisi sana)una kauwezo ka kudanganya ili utete ndoa yako, sasa unasubiri mfumwe?
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  si ndio hapo na mie najiuliza wanashauriana kitu gani hawa watu? labda atuambie waliandikiana mkataba.
   
 15. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...tatizo linalokukabili ni uasherati.
  ...unataka, hujaamua kujitoa!
  ...ndio maana nikasema hamuwezi kuacha dhambi hiyo...
  ...hakuna upembuzi wowote utaokufaa hapa ndugu yangu, WEWE uliamua kumsaliti huyo mdau Jirani yako kwa kutembea na Mkewe, mama wa watoto wake wakati mwenzio yupo busy kazini kufidia kipato cha kuwafaa wanafamilia wake. NYIE kwa kisingizio hicho, mmekuwa mnajivinjari mfululizo kwa muda wa miaka zaidi ya mitatu...

  Nini kinachokupelekea/kinachokushawishi sasa kuacha? ukijibu hili ndipo utapoeleweka una nia gani katika kusitisha huo uhusiano wenu.
   
  Last edited: Feb 20, 2009
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ikishindikana kabisa hama mtaa, nenda mbali nae, mbali sana. Kwani waswahili wanasema "fimbo ya mbali haiui nyoka"... na wengine wanasema
  "out of sight out of mind".
  Na delete mazagazaga yake yote kwenye simu yako.
   
 17. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  namna ya kuachana kwa njia endelevu jamani..nia anayo ila mwili ni dhaifu!
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kiroroma

  Kifupi wewe ni weak sex, hakuna justification ya wewe kucheat kwa shoga wa mkeo!! Kwa maana hiyo huna mapenzi na mkeo na nhata huyo dada unayekula urada for 3 yrs. Nakuhakikishia mkeo naye anamegwa na wajanja maana huwezi kuwa unanyumba ndogo na mkeo uniambie unatosheleza wote...Binafsi huwa na cheat mara chache chache tena si na wake za watu kupasha moto ....ila kwa miaka 3 nomaaaa....hebu fikiria jamaa anahangaikia familia yake wewe unakamua tu!! walahi unatakiwa upigwe risasi ufe kabisa...jamaa kulewa huenda anamsongo wa mawazo anajua unachokifanya miaka mitatu duuu mzee hapo hata condom hutumii

  Ushauri

  Achana kabisa na tamaa za ngono na wake za watu!! Fanya uwezalo uachane na huyo mama rudi kwa mkeo ulee watoto wako. Ukifumaniwa ipo siku utajificha wapi mkware wewe!!! Alaaaaaaaaaaaaa
   
 19. B

  Bibi Kizee JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  pole sana ndugu yangu,

  wachangiaji wengi wameonngea kutokana na fikra zao, na inawezekana pana wengine wanafanya makubwa kushinda hilo ila ni kwakuwa hawajayaweka jamvini tu! kwahiyo usikate tamaa kwa majibu unayoyapata, kizuri ni kuwa umegundua kosa lako, na unania ya kujirekebesha basi jitahdidi kuomba sana kwa imani yako upate mwanga sahihi wa kuliendea hilo bila kuwa na madhara kwako, kwa mkeo,na kwa mwingine yeyote!

  kubwa ambalo naweza kukushauri kama unania ya dhati ya kuacha hilo ni kwanza kuwa muwazi, mueleze dhamira yako, kwa kumfafanunulia sababu ya kufanya hivyo, pengine anahisi umepata kimwana mwingine! mueleze kwa uwazi madhara yake kwa ndoa zenu na pia katika jamii kwa ujumla, kama ulivyosema ni ngumu lakini inaweza kukusaidia,

  Pia jitahidi uwe mbali naye ule ukaribu mliokuwa nao uupunguze ingawa, hii ingesaidia kama huyu bibie asingelikuwa jirani au mtu wako wa karibu, kama unaweza hata kuhama katika hilo eneo kwa usalama wa ndoa yako, na pia kuhifadhi maadili yako,

  Lingine ambalo lingeweza kusaidia pia ni kuepuka mawasiliano na huyo mama, kama si simu basi tafuta japo line nyingine uzuri bogo laini unaokota chini, pia badili utaratibu wako wa kazi, tafuta mambo ya kukushughulika na kukufanya busy ili ule muda ambao huwa mnakutana uwe na shughuli na isiwe rahisi kukutana naye pengine unaweza kutumia hizo excuse za kazi na nafasi kama sababu ya kuwa mbali naye hatimaye apatapa uchovu wa hisia na kuhisi huna haja naye tena na hivyo naye kutoona umuhimu wa kuwa nawe,

  ila kama utaendelea kumumsikiliza, kumjali na kumpa akitakacho basi huu mchezo mwisho wake ni aibu na fedheha kwenu, ilazimishe nafsi, kukkosea si kosa kosa kurudia kosa, na ubaya wa kosa ni pale unapolifanya ukiwa unajua kuwa unakosea!!!!
   
 20. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  mhusika hakuomba hukumu bali kaomba ushauri wa jinsi ya
  kutatua shida aliyokuwa nayo.

  mkuu binafsi nadhani tatizo lipo kwenye jinsi unavyotaka
  kujinasua na hali uliyopo. inaelekea njia uliyotumia imemfanya
  huyo "shoga" wa mkeo ahisi umemtumia na sasa unaona hana
  maana tena. aidha inawezekana huyo bibie ndio "kishafika" kwako
  kikwelikweli kiasi kwamba yu radhi kuvunja ndoa yake akiamini utaendelea naye.
  kama hali ndio hii pole sana.

  mdau kibunango hapo juu kakushauri uhame nami naamini huo ndio
  uamuzi muafaka. kama nyumba uishio ni yako basi tafuta mpangaji
  wewe uhamie eneo lingine hata kwa miaka mitatu ijayo. vinginevyo
  kama hali inaruhusu nenda masomoni ukifika huko kata kabisa mawasiliano
  labda hii itasaidia.

  lakini khaa! kama moyo umependa endeleza libeneke kwani hujui msemo usemao nzi kufia juu ya kidonda... :)
   
Loading...