Msaada wa ushauri kuhusu kozi ya Diploma ya Clinical Medicine

Msaada wa ushauri kuhusu kozi ya Diploma ya Clinical Medicine

Joined
Apr 29, 2020
Posts
41
Reaction score
24
Habari wana JF,

Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Afya ngazi ya Diploma nachukua Diploma ya Clinical Medicine. Kwa sasa nipo mwaka wa kwanza ndo tuliorudishwa kwenye hii likizo lakini nilikuwa tayar nimefanya baadhi ya mitihani ya semester ya kwanza nikiwa nimebakiwa na mitihani ya oral exams pekeake.

Leo nimeleta huu uzi wana JF mnisaidie kwa ushauri , chuo ninachosoma ni cha private na ada yake ni kubwa.. Inaenda 3milion, dah kwa hali ya uchumi nahisi nitapata tabu san maana hata kufanya tu mtihani wa semester nimekumbana na vikwazo vingi vya kufukuzwa ada na pia isitoshe chuo chetu kina sheria kali kwenye udaiji wa ada, kiukweli kiasi nilichotoa hata mimi najioneaga aibu yani ni laki mbili tu.

Lengo langu nlilotaka kulifanya nlitaka niapply upya mwaka huu nikaanze tu upya chuo cha serikali kule angalau ntapata ahueni ya kusoma na kulipa taratibu. Kiukweli naipenda sana hii kozi na ndio ndoto zangu kuitimiza.. Hofu inapokuja ni kuhusu usajili na mitihani ambayo nimeshaifanya tayari.

Je, nikiapply upya mwaka huu inawezekana nikachaguliwa na kama, na kama jibu ni hapana nifanyaje ili niweze kuingia vyuo vya Serikali?
 
Vyuo vya serikali vina ushindani mkubwa. Kama huna Div 1 si rahisi kwenda. Div 2 kidogo kidogo! (science of course) Hivyo angalia kwanza pass zako zikoje!

kama ziko vema , apply. Utapata regardless uliomba mwaka jana private.
By the way NACTE wanafungua lini dirisha la udahili?
 
Division one ni kwa kidato cha nne au sita?
 
Anapata mkuu ufaulu mzuri ila afanye hivi

1.Usiombe diploma omba Certificate
2.usichague vyuo vyenye ushindani mkubwa kama Mtwara,Lindi,Kibaha,Lugalo(sio cha serikali maana ada zaidi ya 1.9M),Kilosa
3.Hakikisha unaomba mapema bila kubadili badili

Nyongeza....

Pia unaweza usiombe upya,andika barua ya kuomba uhamisho,kuna dogo ila kwa bahati mbaya now sina mawasiliano yake yeye alisoma chuo cha private kwa semister moja akashindwa then akaomba kuhamia mtwara ili aanze mwaka upya akapata na hivi sasa ndo yupo semister ya kwanza.

Pia kuna kozi iangalie imewatoa wengi Radiology,
Hapa chuo cha serikali si rahisi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anapata mkuu ufaulu mzuri ila afanye hivi

1.Usiombe diploma omba Certificate
2.usichague vyuo vyenye ushindani mkubwa kama Mtwara,Lindi,Kibaha,Lugalo(sio cha serikali maana ada zaidi ya 1.9M),Kilosa
3.Hakikisha unaomba mapema bila kubadili badili..
Nashukuru sana mkuu kwa kunionyesha mwanga. Maana nlitarget ivyo vyuo vyenye majina makubwa kumbe kwa ushindani uliopo ningeangukia pua
 
Habari wana JF,

Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Afya ngazi ya Diploma nachukua Diploma ya Clinical Medicine. Kwa sasa nipo mwaka wa kwanza ndo tuliorudishwa kwenye hii likizo lakini nilikuwa tayar nimefanya baadhi ya mitihani ya semester ya kwanza nikiwa nimebakiwa na mitihani ya oral exams pekeake...
Kama upo private waweza ukafanya mpango ukaamia chuo cha serikali ndugu ila inatakiwa ukalie sana kwa wajamaa so fanya ivyo maana serikali ada ni raisi zaidi maana hiyo million 3 ni ada yangu ya miaka mitatu full michango yote,......karibu mtwara cohas(cotc)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huu uzi uko poa mtawasaidia wengi.

Sorry nilikuwa pia nataka kufahamu uhitaji wa clinical officers nchini ukoje manake mke wangu kahitimu hiyo course Mwaka huu kwenye chuo mojawapo Cha private nchini
 
Kama utaweza jitahidi umalizie mwaka huu wa kwanza then baada ya hapo omba uhamisho ila hakikisha kabla ya kuomba uhamisho uhakikishe umepata nafasi kwenye chuo unachotaka kuhamia na kupata nafasi unaweza kupata chuo chochote hata hivyo venye ushindani lakini shida ni connection tu
 
Kama kapata G.P.A nzuli mwambie aombe degree ( MD) dilisha likifunguliwa (kwa maana baada ya matokeo ya form six kutoka) na mkopo pia aombe bila shaka atapata.... Baada ya muda utaona impact yake..

I stand to be corrected..
Mkuu huu uzi uko poa mtawasaidia wengi.

Sorry nilikuwa pia nataka kufahamu uhitaji wa clinical officers nchini ukoje manake mke wangu kahitimu hiyo course Mwaka huu kwenye chuo mojawapo Cha private nchini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A
Kama utaweza jitahidi umalizie mwaka huu wa kwanza then baada ya hapo omba uhamisho ila hakikisha kabla ya kuomba uhamisho uhakikishe umepata nafasi kwenye chuo unachotaka kuhamia na kupata nafasi unaweza kupata chuo chochote hata hivyo venye ushindani lakini shida ni connection tu
Ahsante sana mkuu kwa ushauri
 
Back
Top Bottom