Tatizo dogo hilo mkuu. mimi nina Galaxy s7 na shida hiyo nmeshawahi kuisolve, lakini uwe makini tu na maelekezo ninayoenda kukupatia.
Kwanza kabisa tatizo hilo linasababishwa na maswala ya setting za simu. Unawezakuwa wewe mwenyew umeweka hizo setting bila yakujua au umemwachia mtu nayeye bila yakujua akawa ameweka seting hizo.
Hatua yakwanza kabisa kagua kama kuna namba umeziblock (yaani umezizuia kupata simu zake au sms). Utafanya hivyo kama ifuatavyo.
Nenda kwenye icon unayoitumia kudial namba za simu, ukishafungua juu upande wakulia utaona vidoti vitatu, viguse alafu nenda sehemu ya chaguo la block number. Baada yahapo nenda kwenye chaguo la blocked number (namba zilizozuiliwa) .kama kuna namba zipo hapo basi itabidi uziunblock.
Kama tatizo litakuwa bado lipo ,tumia njia ya pili nayo ni hii. Nenda setting kisha tafuta sehemu ya call setting alaf utaona sehemu ya call barring, angalia call barring kama imekuwa enabled. Kama iko enabled unatakiwa kuidisable, kisha angalia kama tatizo litakuwa bado lipo.
Kama tatizo bado lipo.. Tumia njia ya tatu nayo ni hii. Nenda kwenye setting ya simu yako kisha ufanye kureset setting zote ulizokuwa umeweka kisha ujaribu tena uone kama tatizo litakuwa bado lipo.
Kama tatzo litakuwepo bado ,basi unatakiwa kuireboot simu yako kwa kuhold volume down buton na start buton mpaka utakaposkia simu imevibrate then uiachie,,, baada ya muda wa hata dakika 1 itawaka, hapo itabidi ukague kama tatzo bado lipo.
Kama shida itakuwa bado ipo basi nikushauri uipeleke simu hiyo kwa mafundi wa software (wanaoaminika)waangalie kwa undani zaidi
View attachment 1627206