Msaada wa sheria/taratibu za mirathi

A

Ang'ino

Member
Joined
Jun 9, 2013
Messages
42
Likes
0
Points
0
A

Ang'ino

Member
Joined Jun 9, 2013
42 0 0
Ndugu zangu naja tena kwa mara nyingine,nikiwa na hoja yangu ileile ya kupewa Mawazo ya kama ni sahihi au la!
Kufungua MIRATHI ya mwanamke aliyeolewa na ndoa inatambulika kisheria.Tatizo ni kuwa mume na mke wote kwasasa ni MAREHEMU.Mume alikuwa na wake WAWILI na kila mmoja alimjengea nyumba yake inayojitegemea.
mmoja wa wake za mume yungali hai na anayo nyumba yake na watoto wake,
Huyu mke aliyefariki alikuwa ni Mwajiriwa na alizaa mtoto mmoja pekee,pia kuna baadhi ya mali amepata baada ya mumewe kufariki.
Maazimio ya familia ya mume ni kumpa mtoto wa huyu mama URITHI wote unaoangukia upande wa mama yake mzazi.
Je, nisahihi?
Kwa sasa tunasubiri kwenda MAHAKAMANI kumthibitisha Msimamizi wa Mirathi ya huyu mama.Chonde chonde kwa yeyote mwenye ujuzi wa masuala haya tafadhali nipe Msaada.
 
D

daisy

Senior Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
141
Likes
22
Points
35
D

daisy

Senior Member
Joined Jan 22, 2011
141 22 35

umesema mume pia ni marehemu, hivyo natuamaini mirathi ya mume ilishafanyika na mgawanyo wa mali ulimalizika. kamam ndivyo swala la mali za mume halipo tena , hapa ni swala la mali za mke(marehemu).
Je mtoto wa maerehemu ana umri gani? kama ni above 18 basi familia impendekeze huyo mtoto pamoja na mtu mwingine katika familia ambaye huyo mtoto anamuamini ili kwa pamoja wawe wasimamizi wa mirathi.
Lakini hilo hapo juu lifanyike tu pale ambapo marehemu hauacha wosia kuhusu nani awe msimamizi wa mirathi yake, kwa sababu kama wosia upo ni kiasi tu cha kwenda mahakamani ili mahakam imthibitishe aliyetajwa kwenye wosia.
 
queeny

queeny

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Messages
587
Likes
17
Points
35
queeny

queeny

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2012
587 17 35
Mirathi ya baba si ilishaisha? Kinachoangaliwa hapa si mali za mama? Je kuna wosia wowote? Kama hamna wosia mnaona shida gani kwa mali kwenda kwa mtoto pekee? Hao watoto wengine hizo mali zinawahusuje?
 
A

Ang'ino

Member
Joined
Jun 9, 2013
Messages
42
Likes
0
Points
0
A

Ang'ino

Member
Joined Jun 9, 2013
42 0 0
Ahasanteni sana,wote mliojiskia HURU kunipa mchango wa mawazo.
 
Anheuser

Anheuser

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Messages
1,960
Likes
54
Points
145
Anheuser

Anheuser

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2011
1,960 54 145
pamoja na mtu mwingine katika familia ambaye huyo mtoto anamuamini ili kwa pamoja wawe wasimamizi wa mirathi
.
Nilidhani msimamizi wa mirathi lazima awe mmoja wa beneficiaries, na si ndugu yeyote yeyote tu ambae "anaaminika." Nisahihishe ninapokosea tafadhali.
 
D

daisy

Senior Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
141
Likes
22
Points
35
D

daisy

Senior Member
Joined Jan 22, 2011
141 22 35
Nilidhani msimamizi wa mirathi lazima awe mmoja wa beneficiaries, na si ndugu yeyote yeyote tu ambae "anaaminika." Nisahihishe ninapokosea tafadhali.
Sio lazima msimamizi wa mirathi awe one of the beneficiaries. kinachotakiwa ni mtu muaminifu atakaye simamia pamoja na atakayegawa mali za marehemu kwa uaminifu bila kuwadhulumu beneficiaries. Nadhani watunga sheria waliona mbali kwani wakati mwingine beneficiaries wanakuwa bado wadogo hivyo inabidi huyo msimamizi awe ndio mlezi wao na muangalizi wa mali za marehemu hadi pale watoto watapofikia age of majority ili aweze kuwagawia mali zao. Ndio maana tunashauriwa kuandika wosia ili uweze kutaja watu unaowaamini kama wasimamizi wa mirathi pale mauti zitapotukuta.
 
Anheuser

Anheuser

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Messages
1,960
Likes
54
Points
145
Anheuser

Anheuser

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2011
1,960 54 145
Sio lazima msimamizi wa mirathi awe one of the beneficiaries. kinachotakiwa ni mtu muaminifu atakaye simamia pamoja na atakayegawa mali za marehemu kwa uaminifu bila kuwadhulumu beneficiaries. Nadhani watunga sheria waliona mbali.
Sawa ndugu, ahsante.

Kwa hiyo unasema si lazima msimamizi wa mirathi awe mmoja wa beneficiaries. Hebu tusaidiane kutafsiri hiki kifungu cha sheria hapa:

CAP 352, Section 33
THE PROBATE AND ADMINISTRATION OF ESTATES ACT

Letters of administration on intestacy

(1) Where the deceased has died intestate, letters of administration of his estate may be granted to any person who, according to the rules for the distribution of the estate of an intestate applicable in the case of such deceased, would be entitled to the whole or any part of such deceased's estate.

Maana yake nini?
 
Marry Hunbig

Marry Hunbig

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2012
Messages
1,680
Likes
527
Points
280
Marry Hunbig

Marry Hunbig

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2012
1,680 527 280

Habari ndugu, ngoja nimsaidie uyo jamaa, yeye atakuja kujibu maadam nimeliona swali ninaloweza kulijibu, ngojan ilijibu.

kwa kawaida, ni kweli kwamba sio lazima awe mmoja wa beneficiaries, hiyo ni general rule tu. msimamizi wa mirathi anaweza kuwa mtu yeyote yule mwaminifu na atakayeishughulikia ile mali kama vile marehemu ambavyo angeishughulikia. ie. ataitunza, ataigawa kwa haki na usahihi kama vile mali ile ni yake vile. hivyo si lazima awe beneficiary(heir). maana ya beneficiaries hapa wanaweza kuwa wale warithi halali (heirs), wadai (creditors) etc ambao wana maslahi kwenye mirathi hiyo. practically huko mahakamani, watu hawa wenye maslahi huangaliwa kwanza katika kuteuliwa kuwa administrators, lakini kama hawa wote hawatakuwa na uwezo kufanya hivyo, mahakama inaweza kuangalia mtu mwingine yeyote mwaminifu anayeweza kuteuliwa kwa hilo. KABIDHI WASII MKUU (kule RITA) pia huwa anaweza kuteuliwa na mahakama kufanya kazi hii pamoja na kwamba hana maslahi kabisa na mirathi husika.

hata hivyo, ni nadra na haijawahi kutokea, kwa mtu ambaye hana maslahi kabisa na mirathi ya marehemu akaomba kuteuliwa kuwa msimamizi....kwa maslahi gani? kwa faida gani afanye hivyo? wewe hapo uache shuguli zako uanze kukimbizana ma mirathi ya baba yangu mimi wakati hutapata mgao toka mle...sio kitu rahisi. lakini Generally and practically, wale wenye maslahi hupewa kipaumbele kwanza wateuliwe, kama hakutakuwa na wenye uwezo au wanaoaminika, basi mahakama inaweza kumteua mtu yeyote yule.

katika kesi ya SEIF MARARE VS MWADAWA SALUM 1985 TLR 253(HC), iliamriwa kwamba, wajibu wa mahakama katika kumchagua msimamizi wa mirathi ni kuchagua mtu ambaye ana maslahi katika mirathi hiyo na ambaye angeweza kusimamia mirathi, na kulingana na matakwa aliyokuwa nayo marehemu kama yatakuwepo(kwenye wosia).

kuna kitabu fulani hapa cha sheria, ukikisoma kitakusaidia haya yote yameandikwa humo. link yake iko hapa chini.
View attachment 98202
View attachment 98202
View attachment 98203 View attachment 98203 View attachment 98203 View attachment 98203
 
Anheuser

Anheuser

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Messages
1,960
Likes
54
Points
145
Anheuser

Anheuser

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2011
1,960 54 145
hata hivyo, ni nadra na haijawahi kutokea, kwa mtu ambaye hana maslahi kabisa na mirathi ya marehemu akaomba kuteuliwa kuwa msimamizi....
Okay, ahsante sana. Kwa hiyo katika hali halisi jitu ambalo haliwezi kurithi chochote haliwezi kujitokeza kudai lenyewe ndio lipewe letters of administrations.

Na kuna angle nyingine ya swala hili. Ukienda mahakamani au kwa mwanasheria kufungua shauri la mirathi cha kwanza watakachokuuliza ni kikao cha familia kimekaa? Kwa hiyo ni muhimu sana sana kukawa na rekodi za kikao hicho, na chenye saini ya mwenyekiti na wajumbe.

Swali ni je, akidi ya kikao cha familia ni nini?

In other words, members wangapi wa familia au nani na nani lazima wawepo ili kiitwe kikao cha familia? Nadhani tumewahi kusikia au kuwa wahusika wa misiba ambayo kuna pande kama tatu hivi halafu kila kikundi kimefanya kikao chao, ushawahi sikia hiyo? Na kuna kesi ambapo mjomba mmoja anajitokeza baadae kusema mimi sikuwepo kwenye kikao maana sikufahamishwa, wakati hata angekuwepo hana haki ya kuchaguliwa kuwa msimamizi, manake beneficiaries wapo.

Sasa, mtoto mmoja mtu mzima wa marehemu ambae hana ndugu, akikaa na mama yake wakasema sisi wawili ndio kikao cha familia na tumeona mama awe msimamizi wa mirathi. Akidi imetimia? Ikipingwa na wajomba itapita?
 
maswali yako yana mantiki sana na inaonekana unao uelewa mzuri katika jambo hili. nafikiri hakuna idadi halisi ambayo imetajwa kisheria kwamba member kadhaa wanatakiwa kuwepo kwenye kikao na kuorodhesha majina na sahihi zao kuwa wamemteua mtu fulani aende akathibitishwe/akateuliwe na mahakama kama administrator. mawazo yangu nafikiri wanaukoo hawawezi kukaa kisirisiri kufanya jambo hilo na kama wakifanya hivyo, wale ambao hawakuhusishwa wanayo nafasi kupinga kwenye zile siku 90 za tangazo kabla ya kumteua masimamizi. msimamizi hatakiwi kufanya mambo kisirisiri au kwenda kuteuliwa kisirisiri, na bila shaka mle kwenye kikao cha wanandugu/wanaukoo lazima watakuwepo na warithi halali kuhudhuria, sidhani kama ni rahisi sana kwa watu kulaghai katika hili wakati mambo yote yanatakiwa yawe wazi na zipo siku 90 za tangazo na watu kuweka pingamizi pale ambapo wanaona kuna jambo halikwenda sawa.

View attachment 98436
View attachment 98436
View attachment 98440 View attachment 98439 View attachment 98438
 
D

daisy

Senior Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
141
Likes
22
Points
35
D

daisy

Senior Member
Joined Jan 22, 2011
141 22 35
Sawa ndugu, ahsante.

Kwa hiyo unasema si lazima msimamizi wa mirathi awe mmoja wa beneficiaries. Hebu tusaidiane kutafsiri hiki kifungu cha sheria hapa:

CAP 352, Section 33
THE PROBATE AND ADMINISTRATION OF ESTATES ACT

Letters of administration on intestacy

(1) Where the deceased has died intestate, letters of administration of his estate may be granted to any person who, according to the rules for the distribution of the estate of an intestate applicable in the case of such deceased, would be entitled to the whole or any part of such deceased's estate.

Maana yake nini?
Anheuser, thanks na tuendelee kuelimishana. look here I dont dispute the quote above which is the provision of the law regarding administration of the deceased estate but practically i concur with Mishpacha Brucha kwamba sio lazima msimamizi awe mrithi na ndio maana kunapokuwa na mazingira tata katika uteuzi kwa aliyeomba na wanaopinga usimamizi ambapo mahakama inaona ili haki itendeke basi Kabidhii Wasii Mkuu huteuliwa kuwa msimamizi. Je Kabidhi Wasii Mkuu ana interest yoyote katika mali za marehemu ambaye hata hamfahamu. Ndio maana kifungu hicho kina neno MAY(wich means not necessary but depends on the circumstances of the case) and not SHALL(which means no option is available except the way it is)
 
D

daisy

Senior Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
141
Likes
22
Points
35
D

daisy

Senior Member
Joined Jan 22, 2011
141 22 35
Okay, ahsante sana. Kwa hiyo katika hali halisi jitu ambalo haliwezi kurithi chochote haliwezi kujitokeza kudai lenyewe ndio lipewe letters of administrations.

Na kuna angle nyingine ya swala hili. Ukienda mahakamani au kwa mwanasheria kufungua shauri la mirathi cha kwanza watakachokuuliza ni kikao cha familia kimekaa? Kwa hiyo ni muhimu sana sana kukawa na rekodi za kikao hicho, na chenye saini ya mwenyekiti na wajumbe.

Swali ni je, akidi ya kikao cha familia ni nini?

In other words, members wangapi wa familia au nani na nani lazima wawepo ili kiitwe kikao cha familia? Nadhani tumewahi kusikia au kuwa wahusika wa misiba ambayo kuna pande kama tatu hivi halafu kila kikundi kimefanya kikao chao, ushawahi sikia hiyo? Na kuna kesi ambapo mjomba mmoja anajitokeza baadae kusema mimi sikuwepo kwenye kikao maana sikufahamishwa, wakati hata angekuwepo hana haki ya kuchaguliwa kuwa msimamizi, manake beneficiaries wapo.

Sasa, mtoto mmoja mtu mzima wa marehemu ambae hana ndugu, akikaa na mama yake wakasema sisi wawili ndio kikao cha familia na tumeona mama awe msimamizi wa mirathi. Akidi imetimia? Ikipingwa na wajomba itapita?
Ndio maana kesi za mirathi ni moja ya migogoro inayochukua muda mrefu sana mahakamani kwa ajili ya ujinga wa watu wachache wazima kugombea mali za marehemu sijui walikuwa wapi wakati marehemu anatafuta . Mfano hapo uliposema kuhusu wajomba kwa uelewa wangu wajomba ni ndugu wa mama sasa kama aliyefariki ni mume wa mama kikao cha ukoo kinamaanisha ndugu wa baba(ambaye ndie marehemu)mke wa marehemu na watoto wa marehemu, wajomba hawana nafasi.
Kuhusu Akidi ya kikao cha ukoo inategemea na ukoo wenu ni mkubwa kiasi gani pia na mila na desturi za kila kabila kuna utaratibu wa akina nani wanaruhusiwa kuhudhuria vikao vya kifamilia/ukoo vinavyotoa maamuzi mazito.
 
D

daisy

Senior Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
141
Likes
22
Points
35
D

daisy

Senior Member
Joined Jan 22, 2011
141 22 35
maswali yako yana mantiki sana na inaonekana unao uelewa mzuri katika jambo hili. nafikiri hakuna idadi halisi ambayo imetajwa kisheria kwamba member kadhaa wanatakiwa kuwepo kwenye kikao na kuorodhesha majina na sahihi zao kuwa wamemteua mtu fulani aende akathibitishwe/akateuliwe na mahakama kama administrator. mawazo yangu nafikiri wanaukoo hawawezi kukaa kisirisiri kufanya jambo hilo na kama wakifanya hivyo, wale ambao hawakuhusishwa wanayo nafasi kupinga kwenye zile siku 90 za tangazo kabla ya kumteua masimamizi. msimamizi hatakiwi kufanya mambo kisirisiri au kwenda kuteuliwa kisirisiri, na bila shaka mle kwenye kikao cha wanandugu/wanaukoo lazima watakuwepo na warithi halali kuhudhuria, sidhani kama ni rahisi sana kwa watu kulaghai katika hili wakati mambo yote yanatakiwa yawe wazi na zipo siku 90 za tangazo na watu kuweka pingamizi pale ambapo wanaona kuna jambo halikwenda sawa.

View attachment 98436
View attachment 98436
View attachment 98440 View attachment 98439 View attachment 98438
Asante kwa maelezo mazuri. Sio tu kwa mawazo yako ila ndio utaratibu uko hivyo kikao cha ukoo hakitakiwi kuwa cha siri kimsingi kinatakiwa kiitishwe kwa kuwapa wahusika taarifa rasmi kwa maandishi ikiwajulisha tarehe, dhumuni la kikao cha ukoo na wapi kikao hicho kitafanyika, say mwenyekiti wa ukoo anaandika notisi/barua na kupeleka kwa kila mtu anayejua anatakiwa kuhudhuria kikao hicho. Hii inasaidia sana kuondoa wale wabishi wabishi wanaofika mahakamani na kuweka vipingamizi oh, kikao kilikuwa cha siri, sijui muhitasari wakufoji au umechakachuliwa.

Lakini cha msingi kabisa jamani tuandikeni wosia na kuutunza vema pia tukumbushe ndugu na marafiki zetu umuhimu wa wosia ili kuepusha migogoro.
 
Anheuser

Anheuser

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Messages
1,960
Likes
54
Points
145
Anheuser

Anheuser

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2011
1,960 54 145
Mfano hapo uliposema kuhusu wajomba kwa uelewa wangu wajomba ni ndugu wa mama sasa kama aliyefariki ni mume wa mama kikao cha ukoo kinamaanisha ndugu wa baba(ambaye ndie marehemu)mke wa marehemu na watoto wa marehemu, wajomba hawana nafasi.
Kuhusu Akidi ya kikao cha ukoo inategemea na ukoo wenu ni mkubwa kiasi gani pia na mila na desturi za kila kabila kuna utaratibu wa akina nani wanaruhusiwa kuhudhuria vikao vya kifamilia/ukoo vinavyotoa maamuzi mazito.
Sasa huo utakuwa ukoo wa marehemu, sio ukoo wa familia ya marehemu. Kwa nini mama awe peke yake pasipo ndugu zake kwenye hicho kikao? Huoni kwamba hao ma baba wadogo wanaweza wakamzidi sauti kwenye kikao ambacho mwisho wa siku ni Mke/mjane ndio anatakiwa apewe asilimia kubwa ya urithi kisheria?

Huhusu utaratibu wa kimila, mimi nataka sheria zilizoandikwa, sio u-mila mila. You know why? Because sheria za kimila zinasema mtu akifa basi mdogo wake marehemu atamrithi mjane na watoto wake na mali zake, ushasikia hiyo? Total nonsense. Ndo maana tunaenda mahakamani kutafuta sheria zinazo make sense!

Na kama ni mila basi ziwekwe vitabuni tuzijue. What if mke mpogolo mume mdengeleko, mila gani zinafuatwa? What if hakuna huyo so called "mwenyekiti wa ukoo"? What if upande wa mjane wana Mwenyekiti wa ukoo na upande wa marehemu wana Mwenyekiti wao wa ukoo wao, nani ana haki ya kuitisha na kuendesha kikao cha ukoo? What if baba mdogo akakataa kikao cha mjomba (kaka wa mjane) ambae let's say ndio "mwenyekiti wa ukoo" wa mjane, akasema huyo mjomba mimi sio mwenyekiti wa ukoo wangu, hana jurisdiction ya kuniita kwenye kikao, nasubiri chetu. Sheria isemeje?

... nafikiri wanaukoo hawawezi kukaa kisirisiri kufanya jambo hilo .....msimamizi hatakiwi kufanya mambo kisirisiri au kwenda kuteuliwa kisirisiri,... sidhani kama ni rahisi sana kwa watu kulaghai katika hili wakati mambo yote yanatakiwa yawe wazi
Eti hawawezi kukaa kisiri siri?

Unayachukulia mambo ya family disputes kirahisi rahisi mno. Tunapoongelea mashauri ya mahakamani na sheria na kadhalika maana yake kuna kutofautiana, kuna beef, mzozo, ugomvi, vita!

We hujayaona haya kwenye misiba, watu wanagombea maiti kuzika, itakuwa mali za marehemu?

Sio lazima wakae kisiri siri, wanaweza wakakaa wazi wazi lakini unilaterally and separately, in other words kuna misiba miwili miwili na vikao viwili viwili, hujawahi ona hiyo?
Usichukulie kwamba ndugu watatoa ushirikiano kirahisi rahisi tu, ndio maana tunaongelea sheria hapa.
 
D

daisy

Senior Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
141
Likes
22
Points
35
D

daisy

Senior Member
Joined Jan 22, 2011
141 22 35
Sasa huo utakuwa ukoo wa marehemu, sio ukoo wa familia ya marehemu. Kwa nini mama awe peke yake pasipo ndugu zake kwenye hicho kikao? Huoni kwamba hao ma baba wadogo wanaweza wakamzidi sauti kwenye kikao ambacho mwisho wa siku ni Mke/mjane ndio anatakiwa apewe asilimia kubwa ya urithi kisheria?

Huhusu utaratibu wa kimila, mimi nataka sheria zilizoandikwa, sio u-mila mila. You know why? Because sheria za kimila zinasema mtu akifa basi mdogo wake marehemu atamrithi mjane na watoto wake na mali zake, ushasikia hiyo? Total nonsense. Ndo maana tunaenda mahakamani kutafuta sheria zinazo make sense!

Na kama ni mila basi ziwekwe vitabuni tuzijue. What if mke mpogolo mume mdengeleko, mila gani zinafuatwa? What if hakuna huyo so called "mwenyekiti wa ukoo"? What if upande wa mjane wana Mwenyekiti wa ukoo na upande wa marehemu wana Mwenyekiti wao wa ukoo wao, nani ana haki ya kuitisha na kuendesha kikao cha ukoo? What if baba mdogo akakataa kikao cha mjomba (kaka wa mjane) ambae let's say ndio "mwenyekiti wa ukoo" wa mjane, akasema huyo mjomba mimi sio mwenyekiti wa ukoo wangu, hana jurisdiction ya kuniita kwenye kikao, nasubiri chetu. Sheria isemeje?

Eti hawawezi kukaa kisiri siri?

Unayachukulia mambo ya family disputes kirahisi rahisi mno. Tunapoongelea mashauri ya mahakamani na sheria na kadhalika maana yake kuna kutofautiana, kuna beef, mzozo, ugomvi, vita!

We hujayaona haya kwenye misiba, watu wanagombea maiti kuzika, itakuwa mali za marehemu?

Sio lazima wakae kisiri siri, wanaweza wakakaa wazi wazi lakini unilaterally and separately, in other words kuna misiba miwili miwili na vikao viwili viwili, hujawahi ona hiyo?
Usichukulie kwamba ndugu watatoa ushirikiano kirahisi rahisi tu, ndio maana tunaongelea sheria hapa.
Hapo kwenye para 1, ndipo umuhimi wa kuandika wosia unapokuja.Hata sheria za kiserikali wakati mwingine ni non-sense, na ndio maana decisions za mahakama zinatofautiana kuendana na mazingira ya kesi husika na ndio maana wakati mwingine mahakamani inalazimika kuamua kwa kufuata taratibu za mila husika na hii ni kwa sababu watanzania wengi hatujajiwekea msingi mmoja tu wa jinsi ya kuendesha/kufuata katika maisha ya kila siku, yaani tunachanganya taratibu za kimila na sheria za kiserikali.
Na kwa sababu hiyo hata hizo sheria za kiserikali bado zinatambua taratibu za kimila kama hayo mambo ya vikao vya ukoo ambayo kimsingi hayapo kwenye sheria za mirathi za uingereza ambako ndo sheria zetu zimetokea.
kwahiyo hizo taratibu za kimila sio za kishenzi na kuna baadhi ya makabila bado yanazifuata sisi tuliosoma ndo tunaweza ziita hivyo. Kumbuka pia bunge letu halijazifuta hivyo bado zinatambulika na zinatumika japo can be challenged befor a court of law.
 
Marry Hunbig

Marry Hunbig

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2012
Messages
1,680
Likes
527
Points
280
Marry Hunbig

Marry Hunbig

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2012
1,680 527 280
Sasa huo utakuwa ukoo wa marehemu, sio ukoo wa familia ya marehemu. Kwa nini mama awe peke yake pasipo ndugu zake kwenye hicho kikao? Huoni kwamba hao ma baba wadogo wanaweza wakamzidi sauti kwenye kikao ambacho mwisho wa siku ni Mke/mjane ndio anatakiwa apewe asilimia kubwa ya urithi kisheria?

Huhusu utaratibu wa kimila, mimi nataka sheria zilizoandikwa, sio u-mila mila. You know why? Because sheria za kimila zinasema mtu akifa basi mdogo wake marehemu atamrithi mjane na watoto wake na mali zake, ushasikia hiyo? Total nonsense. Ndo maana tunaenda mahakamani kutafuta sheria zinazo make sense!

Na kama ni mila basi ziwekwe vitabuni tuzijue. What if mke mpogolo mume mdengeleko, mila gani zinafuatwa? What if hakuna huyo so called "mwenyekiti wa ukoo"? What if upande wa mjane wana Mwenyekiti wa ukoo na upande wa marehemu wana Mwenyekiti wao wa ukoo wao, nani ana haki ya kuitisha na kuendesha kikao cha ukoo? What if baba mdogo akakataa kikao cha mjomba (kaka wa mjane) ambae let's say ndio "mwenyekiti wa ukoo" wa mjane, akasema huyo mjomba mimi sio mwenyekiti wa ukoo wangu, hana jurisdiction ya kuniita kwenye kikao, nasubiri chetu. Sheria isemeje?

Eti hawawezi kukaa kisiri siri?

Unayachukulia mambo ya family disputes kirahisi rahisi mno. Tunapoongelea mashauri ya mahakamani na sheria na kadhalika maana yake kuna kutofautiana, kuna beef, mzozo, ugomvi, vita!

We hujayaona haya kwenye misiba, watu wanagombea maiti kuzika, itakuwa mali za marehemu?

Sio lazima wakae kisiri siri, wanaweza wakakaa wazi wazi lakini unilaterally and separately, in other words kuna misiba miwili miwili na vikao viwili viwili, hujawahi ona hiyo?
Usichukulie kwamba ndugu watatoa ushirikiano kirahisi rahisi tu, ndio maana tunaongelea sheria hapa.
sidhani kama nachukulia mambo kirahisirahisi, na pia hapa hatupo vitani, tunatakiwa kujadili kwa hoja sio nguvu za maneno. kama unasema wanaweza wakakaa waziwazi lakini unilaterally au seprarately au wakawa na ugomvi na kutoelewana kwa namna yeyote ndio maana mahakama ipo, na kwa kawaida hata huu ugawaji wa mirathi wakati mwingine mahakama inaweza isihusishwe kama hakuna ugomvi kati ya ndugu na warithi, ila panapotokea kuwa kutokuelewana kunanukia au kuna manungu'uniko au kutokurithikwa kwa yeyote hapo mahakamani unatakiwa kukimbilia ili mirathi igawanywe kisheria. kwanini tunaenda mahakamani? ili msimamizi akateuliwe na mahakama, na kama msimamizi hayupo au inaonekana kati ya ndugu au watu wenye interest na mirathi hawapo au hawaaminiki, administrator general (kabidhi wasihi mkuu) au mtu yeyote yule ambaye mahakama inamuona anafaa anaweza kuteuliwa etc. nimeandika msg hii nikiwa na haraka sana, nitajaribu kukaa badae nieleweshe vizuri.
 
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Messages
30,068
Likes
5,279
Points
280
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2010
30,068 5,279 280
Asanteni kwa michango nya haja na lahaja
 
Forum statistics

Threads 1,273,817
Members 490,485
Posts 30,492,954