Msaada wa notes na videos kusaidia vijana wa shule za sekondari

mashizo

Member
Feb 24, 2009
43
32
Habari zenu JF members,

Kutokana na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na ata yale ya arts na biashara,
nimefikia wazo la kuanzisha website ambayo itakuwa inahusiana na wanafunzi kupata materials (notes)pamoja na videos.

kwa kuanzia mimi binafsi nimeshaanza kuandaa notes za physics kuanzia kidato cha kwanza na cha pili na videos pia.
Pia teyari nimeshatengeneza website nasubiri materials (notes) ziwe teyari ili nianze kuziweka.

msaada kutoka kwa JF members

1) mtu yeyote anaweza kunitumia materials (notes) pamoja na videos ikiwezekana ila lazima awe ana ujuzi wa kutosha kuhusu somo husika (awe amefaulu vizuri somo husika, itakuwa vizuri kama alipata A o-level)

2) materials (notes) ziendane na vitabu vya wizara ya elimu (syllabus) na ukiongezea ubunifu wako itakuwa vizuri zaidi ila ubunifu usitoke nje ya mada husika za somo hilo na itakuwa vizuri videos zikiwa zitaelezewa (kufundisha) kwa kiswahili ili wanafunzi wengi zaidi ata wale ambao kiingereza kinawasumbua waweze kuelewa na kupata maarifa (ujuzi).

3) materials (notes) pamoja na videos ni kwa kujitolea (hakuna malipo yeyote) maana tunafanya kwa ajili ya vijana wetu wa kitanzania (elimu nzuri ni haki ya kila mtu).
4) notes pamoja na videos (kutoka somo husika) sitoziweka kwenye website mpaka zihakikiwe na JF members zaidi ya 20 ambao wamefaulu somo husika kwa kiwango cha A au B na nitawatumia forms ambazo watasaini ili kudhibitisha kukubali kwao kwa kiwango cha ubora wa notes pamoja na video husika

Binafsi nimemaliza chuo na ni engineer kwa sasa, O-LEVEL nilipata div 1 points 12. physics na chemistry nilipata A na masomo mengine saba yaliyobaki B
aliye teyari kushiriki kusaidia vijana wetu anitumie pm then tupange mipango zaidi.

TAIFA BORA LA KESHO LITAJENGWA NA SISI WENYEWE KWA KUJITOLEA MUDA NA MAARIFA MUNGU AIYOTUJAALIA NA SI VINGINEVYO.
 
Back
Top Bottom