kwanza wala usihofu juu ya hilo,huyo ndg yako nakuhakikishia uwezo wa kufauru anao mkubwa ila tu kilichotokea ni kwamba platform aliyokuwepo sio nzuri,hvyo imechangia kufeli kwake.
mimi enzi hizooo wakati nipo shule,nilipata division 0 yaani nilipiga F flat-ukwel nilikata tamaa sikutaman tena kusoma kwa sababu nilijiona sina uwezo darasani.
ila miaka 10 mbele ilinibidi nirudi darasan kwa sababu kile cheti cha form kwa kutokuwa nacho,kilinifanya sehem nying nishindwe kupenya.
nili-reset mwaka mmoja tu nikapata pass kama zote na ma credit,kumbuka nilirudia baada ya miaka 10 nadhan unaweza kuvuta picha hapo.
nachokusihi hiyo kijana kama yupo dar,nitumieni namba zenu PM tuwasiliane ntakuelekeza centre ya kwenda ku-reset,ninachokuhakikishia huyo ndg yako kwa mwaka mmoja tu,atakuleteeni matokeo mazuri saaaana na mtashangaa wenyewe,
kwenye hiyo centre haijawahi kutokea mwanafunzi kukosa hitaji lake kimasomo/walishasoma hapo wanafunz wagumu na walioshindikana kufauru kwenye mashule watokayo ila hapo walifanikiwa niamin hakika nakwambia.
naamini malengo yake ni kufika chuo kikuu baada ya kusoma 5&6 hvyo ndoto yake ataifikia kama utaniamini kwa kumuelekeza akasome hapo paliponitoa kimasomaso kwani hata mimi nilikuwa najisikia kama ajisikiavyo yeye.
natamani niandike vingi ila niishie tu hapo
Sent using
Jamii Forums mobile app