Msaada wa mawazo kwa wenyeji wa mikoa Dar, Dodoma na Mbeya, na kungine pia napokea

Feb 5, 2017
37
72
Wasalam wakuu wa jukwaa hili pendwa,

Mbele yenu ni kijana mchakalikaji na mpambanaji pia, sichagui cha kufanya.

Naombeni mawazo wenyeji wa maeneo husika hapo juu ila hata nje ya hapo napokea pia.

Nilitoka mkoani nikaja dodoma kwa lengo la kufanya biashara ya mifugo hususani mbuzi, nilifika na kuanza kwenda mnadani kununua mbuzi na kuwapeleka kiwandani, lakini sasa hali imekua kinyume na matarajio niliyokua nayo, kila nikinunua na kupeleka kiwandani lazima badala ya kupata faida nakata hela, nimefanya hivyo kwa awamu mbili tofauti lakini awamu zote zimenikata hela.

Mfukoni nimebakiwa na ml2 tu. Naomba mtu mwenye wazo lolote linaloweza kwendana na bajet yangu hiyo tafadhari anijuze ili nipate kujikwamua kwenye hali niliyokua nayo hapa.

Mikoa niliyoipa kipaumbele zaidi ni Dar, Dom na Mbeya, lakini mikoa yote pia naiweza kuiishi ilimladi niwe na cha kwangu nafanya,

Asanteni
 
Biashara kwenye karatasi ni tamu sana na inashawishi kuifanya, ingia sasa kwenye uhalisia ndio utajua hujui.

Any way huu ni wakati wa mavuno, jichanganye huko mikoani nunua mazao uza huku ukijitafuta mdogo mdogo msimu wa kilimo ukifika nenda kalime.
 
Asante kwa wazo, hususani wapi mkuu
 
Back
Top Bottom