MSAADA WA MATIBABU ELFU 20

MSAADA WA MATIBABU ELFU 20

Nelson nely

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
4,251
Reaction score
2,870
Habari za asubuhi,wakuu wiki iliyopita jumanne huku porini nikiwa nachimbua visiki kwa ajili ya maandalizi ya kuchoma mkaa kwa bahati mbaya sururu iliteleza na kukita kwa juu kidogo ya vidole vya mguu wa kulia,maumivu niliyoyapata siwezi kuelezea,sikutumia dawa yoyote zaidi ya panadol maana sikuwa na pesa.Ndani ya siku mbili maumivu yalipungua na nikawa na matumaini ya kuendelea na shughuli,lakini ghafla usiku wa kuamkia jumatatu nilipata maumivu makali mno kwenye mguu ule ule na mbaya zaidi wiki yote hii kwangu imekuwa ni kukesha na kulia tu na mguu unavimba na nahisi kama kunakuwa na baridi kali kwa ndani.Kwa kifupi hali yangu si nzuri na inabadilika kila kukicha,naomba kwa atakayeguswa na akawa ana uwezo wa kunikwamua kwa kiasi chochote ili nifikishe hiyo elfu 20 ili niweze kutoka huku kijijini nifike hospital nipate walau vipimo...0693265348,NATANGULIZA SHUKURANI.
 
Angalia isijekuwa tetenus mkuu, utakatwa mguu, na kama imesambaa mwili mzima basi huwa hainantiba. Pia nakushauri uza smartphone uende hospitali. Huku ukisubiri mtu wa kukusaidia elf 20
 
Asante mkuu,nina simu ya kawaida sana tecno ya button,nimejaribu kuiweka bond hata kwa elfu 8 imeshindikana watu wanalia ukata ndio maana nimeona nije nijaribu huku.
 
Kumbe JF hata tecno ya batani inakubali tu!!!!
Tuma picha ya jeraha useti na tarehe uliyopiga kwenye hiyo picha hapo msaada utakuja kwa speed ya 4G Ila pole sana.
 
pole sana.ungesema uko wapi ,na unataka kwenda hospital gani?.kuna madaktari wengi tu uku itakua rahisi pia kupata msaada na waombe mods waamishe huu uzi kwenye ili jukwaa
 
Angalia isijekuwa tetenus mkuu, utakatwa mguu, na kama imesambaa mwili mzima basi huwa hainantiba. Pia nakushauri uza smartphone uende hospitali. Huku ukisubiri mtu wa kukusaidia elf 20
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16].jamii forum!
 
pole mleta mada...

upo wapi ? unataka uende hos p gani ? una uhakika hiyo 20000 itatosha ?

nimeuliza hayo maswali kwa sababu unaweza kukuta upo eneo ambalo memba wa hapa yupo na akakugea msaada wa karib hata kukulipia hayo matibabu. au ukifika hosp utoe adress ya hosp husika ili watumiwe hiyo hela direct na wewe upate matibabu.
 
Ni kweli mkuu nipo kijiji kinaitwa IJAKA wilaya ya kongwa dodoma .
 
Kumbe JF hata tecno ya batani inakubali tu!!!!
Tuma picha ya jeraha useti na tarehe uliyopiga kwenye hiyo picha hapo msaada utakuja kwa speed ya 4G Ila pole sana.
Ina kamera mkuu lakini najaribu kuweka picha nashindwa,
 
pole sana.ungesema uko wapi ,na unataka kwenda hospital gani?.kuna madaktari wengi tu uku itakua rahisi pia kupata msaada na waombe mods waamishe huu uzi kwenye ili jukwaa
Asante mkuu niko kijiji cha ijaka,kongwa huku na kwa hapa jirani ni kibaigwa
 
pole mleta mada...

upo wapi ? unataka uende hos p gani ? una uhakika hiyo 20000 itatosha ?

nimeuliza hayo maswali kwa sababu unaweza kukuta upo eneo ambalo memba wa hapa yupo na akakugea msaada wa karib hata kukulipia hayo matibabu. au ukifika hosp utoe adress ya hosp husika ili watumiwe hiyo hela direct na wewe upate matibabu.
Mkuu nimeomba hicho kiasi ili nifike hospitali tu basi maana hali inabadilika kila siku,naona bora ikanibadilikie hospitali
 
Back
Top Bottom