Msaada wa maneno haya

Msaada wa maneno haya

kbmk

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2013
Posts
776
Reaction score
158
naomba mnisaidie maana ya vidahizo vifuatavyo1.kitivo2.mhanga3.miongo4.tumbua5.nyenyele6.matandu7.matlaba8.sandali9.uzimbezimbe10.kinyenyezi11.prediketa12.esperanto
 
naomba mnisaidie maana ya vidahizo vifuatavyo

1.
kitivo = hii ni sehemu ndogo ya taasisi kubwa inayoshughulika na jambo tofauti na vitivo vingine lakini ikiwa ni sehemu ya mamlaka ya taasisi tajwa

2.
mhanga = huyu ni mtu ambaye amejitoa mhanga, nikimaanisha ameamua kwa hiari yake kupata madhara (ikiwezekana hata kifo) kwa lengo la kufaidisha wengine au kutetea imani/msimamo fulani. kuna uwezekano katika kujifanya mhanga akawadhuru wengine pia (tofautisha na muathirika wa tukio la kujitoa mhanga)

3.
miongo = muongo mmoja ni kipindi cha miaka kumi (cheki idadi, naweza nikakosea) kwa hiyo ukiambiwa miongo x, then zidisha x mara kumi ndo idadi kamili ya miaka tajwa

4.tumbua = tumbua inaweza ikawa ni kupasua kitu chenye umbo la kutuna/mviringo ambacho ndani kina aidha hewa au maji maji

vile vile linatumika katika kuelezea matumizi mabaya au yasiyo ya busara ya mali, fedha, nk...na inaweza tumika kumaanisha kufurahia mapenzi au raha kwa kiwango cha juu

5.nyenyele - silifahamu

6.matandu = haya ni majengo na njia ya buibui

pia ni ukoko wa juu wa wali

7.matlaba - sifahamu

8.sandali - hii naona imeelekea kwenye viatu aina ya sandals!!!
9.uzimbezimbe - siifahamu
10.kinyenyezi - siifahamu
11.prediketa12.esperanto
= hii kama itakuwa inatokana na "predicator" ya kiingereza basi itakuwa na maana ya neno au kitenzi kinachotegemewa na neno au kitenzi kingine katika sentensi


NB:All answers are subject to further proof..I was just thinking aloud!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom