Msaada wa kweli wa wafadhili kwa Tanzania...

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,950
..ni kutoipa misaada kabisa. Tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania imekuwa inapokea missada na mikopo lukuki kwa miongo kadhaa sasa lakini hakuna mabadiliko makubwa.

Hoja inayotolewa siku hizi (na kina Bob Gerdolf -naweza kuwa nimekosea spelling za jina lake) ni kuwa mataifa maskini yaachwe bila kupewa misaada tena MAANA misaada inayotolewa hutumiwa vibaya na watawala.

Wajameni mnalionaje hili? Tuanze kampeni ili wafadhili watuache tujiendeleze wenyewe?
 
hapna mkuu misaada watuletee ila wapitishie ktk NGOs.kwa kufanya hivyo hawa wahuni watakua na wigo mdogo wa kujichotea at the sametime wahitaji wataendelea kupata huduma thru NGOs
 
Siku zote msaada ni muhimu ndio maana tunasaidiana hata kwenye misiba na shughuli zinazofanana na hizo. Tatizo litakuwa pale ukipewa msaada ukaenda kufanya lile lisilokusudiwa. Chukua mfano huu- Una ndugu yako mlevi wa kutupa na ana watoto wanasoma, ipi itakuwa njia bora ya kumsaidia??? Kumpa pesa ili akawanunulie watoto uniform na mahitaji mengine AU wewe kununua hivyo vitu na kuwapa hao watoto??
Chigwiye kasema uzuri - Pitishia kwa NGOs.
 
Back
Top Bottom