Msaada wa kutatua ugomvi wa ardhi.

TomJunior

Member
Oct 15, 2011
12
2
Kwa ufupi mimi ni kijana wa chuo, nina ishi na baba na mama. Baba yangu ni mfanyabiashara, miaka 10-15 iliyopita baba alifanya biashara kwa karibu na mfanyabiashara mwenzie ambaye ni ndugu, katika makubaliano yao ya kumaliza kufanya biashara pamoja yule ndugu alikubali kumwachia baba yangu eneo lake tupu lililokuwa kama sehemu ya takataka miaka hiyo ya 90. baba akaliendeleza eneo lile kwa kupanda miti, kujenga fremu za kupangisha na kuendesha biashara yeye mwenyewe pia mahali pale.
Tatizo linakuja baada ya miaka zaidi ya 10-15 yule ndugu analitaka hilo eneo sasa! mwaka jana alifanya fujo kwa kubomoa baadhi ya majengo katika eneo hilo bila kufanya chochote katika eneo hilo, baba akalijenga tena eneo hilo, amebomoa tena mwaka huu! kwa kujali undugu baba hajaenda mahakani bado, na yule ndugu hataki mazungumzo ya kisheria anadai lile eneo ni lake.
Ninaomba ushauri... BABA YANGU ANA HAKI GANI ZA KISHERIA JUU YA ENEO(ARDHI) ILE?
- nikijibiwa kwa mujibu wa sheria nitashukuru zaidi.
 
..., katika makubaliano yao ya kumaliza kufanya biashara pamoja yule ndugu alikubali kumwachia baba yangu eneo lake tupu lililokuwa kama sehemu ya takataka miaka hiyo ya 90....
"Alimwachia" kwa masharti gani? Kwa muda? Huyo nduguye yeye alipata nini kwa kuachia hiyo sehemu yake ya ardhi?
 
alimwachia jumla bila masharti yoyote, nduguye hakutaka chochote wakati huo. baada ya biashara ya pamoja kumalizika kila mtu akaendelea na maisha yake mpka hivi karibuni. NB: ni ndugu wa mbali
 
  • Thanks
Reactions: SMU
"Alimwachia" kwa masharti gani? Kwa muda? Huyo nduguye yeye alipata nini kwa kuachia hiyo sehemu yake ya ardhi?

Huwezi pata jibu sahihi kwa staili hii. Kuna maswali mengi ya kuuliza kuhusu jambo hili ambayo si rahisi kuulizwa na kujibu kwa usahihi kwenye JF. Kinachotakiwa amuone mwanasheria yeyote ambaye atamsaidia tu. Kwani kuna vielelezo vingi vitahitajika kabla ya kupata ufumbuzi. Mafano huyo rafiki yake ana hati ya hiyo sehemu au anamiliki eneo hilo kimila, kama kuna maandishi waliyoaandikiana wakati akimpa, na yeye wakati anajenga aliweka kumbukumbuku zozote za umiliki etc. Kama vipi baba yako aende kwenye vyombo vya sheria - mabaraza ya Ardhi wataitwa kusikilizwa. Kama huyo mwenzie hataki basi hukumu itatolewa pasipo huyo mwingine kuwepo kutokana na hali halisi ya swala husika na vielelezo atakavyovitoa.
 
alimwachia jumla bila masharti yoyote, nduguye hakutaka chochote wakati huo. baada ya biashara ya pamoja kumalizika kila mtu akaendelea na maisha yake mpka hivi karibuni. NB: ni ndugu wa mbali
Na bila ya shaka hakukuwa na kuandikishiana au kuhusisha mashahidi kwa namna yoyote? Kama ni hivyo inaweza kuwa ngumu kwa mzee wako kuthibitisha umiliki wa hilo eneo.
 
yule nduguye hana hati yoyote. maendeleo yote yamefanywa na baba, na kila document imeandikwa kwa jina la baba yangu mpaka meter za umeme zimeandikwa kwa jina lake na risiti zipo toka 90's. nashukuru kwa ushauri na msaada wa hapo juu, lakini kwa sasa ningeomba nipewe msaada kutokana na hii scenerio.
 
sheria za ardhi zinazotambua umiliki wa mtu katika ardhi zipo nyingi,lakini moja mabayo watu wengi hawajui au nisema haifahamiki sana ni, umiliki ambao mtu amekua akitumia eneo fulani kwa zaidi ya miaka kumi na mbili bila mmiliki halali wa eneo husika kujitokeza,wala kutoa taarifa kwa mtua anayeendelea kutumia eneo hilo kuwa ajue anatumia tu lakini si la kwake,sheria hii inatambua kuwa alokuwa akitumia eneo hilo basi ndo mmiliki halali.kitalaamu inaitwa "adverse possession"
kwa sasa nisingeshauri sana kuanza na hatua za kimahakama, hebu busara itumike kwanza,waitwe watu wazima au niseme wenye busara na hekima,wajaribu kuongea na huyo ndugu,wamwelimishe tu kuwa taratibu ziko naman gani,halafu wamwambie huo anaofanya ni uhalifu thidi ya mali ya mtu,kama ikishindikana taratibu za kwenda baraza la ardhi zifuatwe haki itapatikana tu .
 
Kwa mujibu wa maelezo yako, ni dhahiri suala lako ninagusa sheria za Ardhi na sheria ya mikataba, kwa msingi kwamba namna ardhi hiyo ilivyopatikana inategemea mkataba/makubaliano na ushahidi wa uwepo wa makubaliano hayo, kwa mantiki hiyo iwapo hakuna uthibitisho wa haki ardhi hiyo kuhama kutoka kwa mmiliki wa awali kuja kwa mzee wako kimkataba nidhahiri itakuwa ngumu kutumia substantive part ya sheria, aidha umiliki usiopingwa (adverse possesion) unakua na nguvu pale tu ambapo mmiliki wa pili anathibitisha kutumia ardhi hiyo kwa kipindi kirefu (zaidi ya miaka12) bila kubughudhiwa na mtu/watu wanaodai kumiliki/kuwa na maslahi na ardhi hiyo. kwa msingi huu kwa kua tayari kuna mvutano toka kwa mmiliki wa awali ni dhahiri pia ni vigumu kwa mzee wako kushinda kesi hii mahakamani, mimi nashauri suala nhilo lisuluhishwe kidiplomasia zaidi muafaka utakua mzuri zaidi kuliko njia ya kesi
 
Back
Top Bottom