Msaada wa kuset google adsense account

Hepatis B

Senior Member
Feb 11, 2013
183
127
Habari wadau naomba msaada jinsi ya kuset adsense account. Nimeunganisha na you tube channel yangu nimejibiwa hivi mara mbili kila navyoconnect. Msaada tafadhali sijui nakosea wapi.
Screenshot_20221119-121440.jpg
 
decline = ombi lako la kujiunga nao limekataliwa.

Wame review (kupitia) channel yako wameona haikidhi vigezo (sijui ni vipi).

Kukataliwa sio moja kwa moja, wamekwambia unaweza kufanya mabadiliko yanayokidhi masharti yao na uombe upya
 
decline = ombi lako la kujiunga nao limekataliwa.

Wame review (kupitia) channel yako wameona haikidhi vigezo (sijui ni vipi).

Kukataliwa sio moja kwa moja, wamekwambia unaweza kufanya mabadiliko yanayokidhi masharti yao na uombe upya
Sijui kitu gan natakiwa kuset kwenye adsense maana kila kitu nimejaza.
 
Habari wadau naomba msaada jinsi ya kuset adsense account. Nimeunganisha na you tube channel yangu nimejibiwa hivi mara mbili kila navyoconnect. Msaada tafadhali sijui nakosea wapi.View attachment 2420861
Gabeji in gabeji Out!

Jua haya mambo hayataki shortcut, kama ulileta janja janja hutoboi mahali! Ndio wazungu walivyo hivyo!

Sasa wewe jiulize nini umezingua? Je ni video za watu uliiba? Hauna copyright strike yeyote? Je kwenye email hawajasema umezingua nini?

Hao ni wazungu sio wabongo, hawawezi kukuzuia bila sababu ya msingi!!
 
Kama U amiliki Blog na unahitaji iwe approved na Adsense zingatia yafuatayo.
1. Lugha, Adsense wana lugha zai ambazo wanahitaji uzutumie kwenye uandikaji wa contents zako. Note kiswahili hakipo katika lugha ambazo Adsense wanazikubali. Hakikisha hakuna content ya kiswaili wakati unaapply Adsense.

2. Copyright, hakikisha content unazoweka kwenye blog/site yako haina content ambazo umecopy na kupaste kutoka kwa site nyingine, google inatambua kabisa kuwa content hii imetolewa sehem nyingine. Hakikisha unapochukua content za mwingine zibadilishe, edit katika mfumo ambao ztakuwa hazina 100% ya ufanano.

3. Hakikisha unaweka pages muhimu katika site yako. Mfano About page, Contact us, Terms of Use, Privacy Policies. Kama hauwezi namna ya kuandaa Terms of Use na Privacy Policies nambie ntakupa link ya Tool ambayo utaenda ugenerate za kwako automatic.

3. Duration. Sometimes huwa wanataka atleast uwe umefanya zaidi ya miezi sita, ila kigezo hiki hakina nguvu sana kwa sabab kuna watu wanakuwa approved ndan ya mwezi mmoja hadi miwili.

4. Kabla hujaaply Tengeneza content angalau Post 20 zenye content nzuri, kama ni picha nzuri, .

Nikutakie kila la heri Uliza chochote ntakujibu kwa uzoefu wangu, maana mm ni mnufaika wa Adsense, imewahi kunitoa pabaya katika maisha.
 
Back
Top Bottom