Msaada wa kuombewa jamani!

PADRU

New Member
May 26, 2017
3
0
Wakuu heshima kwenu! Naomba niende moja kwa moja kwenye maada kwa yeyote anayeweza nisaidia Ustadhi (Shekhee) ambaye atanisaidia kunifanyia dua kwa ajili mambo yangu sababu mambo kibao yamekwama wakuu yani kila ninalofanya linaenda likifika mbele linagonga mwamba sio ajira sio nini kiujulma mambo ni hayaeleweiki...

Kazi sina kila nikifanya application wazee zinagonga mwamba hata kujitolea bure tu na gharama ni zangu wauu lakini bado watu wananitolea njee wezangu ambao nimesoma nao tena wengine nimewazidi wanazidi kutoboa,

Madogo niliwaacha tena ni wadogo kwangu wanakuja wanapata makazi wanatoboa mimi bado nahaha tu nimejaribu kujiingiza kwenye kilimo jamani nikalima nyanya huko Igawa mkoani mbeya nyanya zikaenda poa ikafika katikati akatokea mdudu sijui anaitwa KANTANGAZE nyanya zikapigwa yani na mtaji ukakata naona nazidi kuchanganyikiwa tu hapa familia imenisomesha kwa nguvu zote ila sahizi nashindwa hata kumsaidia Mother wangu anaumwa hatari yani sijui nilezeje jamani wakuu naombeni mnisaidie sijui shida ni nini?

kuna Interview nimeenda kufanya sehemu nilivyotoka badae kuna jamaa aliyekuwepo kwenye panel akaniambia dogo interview umefanya poa ila sasa hii nafasi ya project coordinator wa huu mradi kuna dada ameshaandaliwa ndo atapewa mimi nitakusaidia upate kujitolea kama watakubali tu dah niliishiwa nguvu nikajiona kama nimelogwa vile.

Naomba ifahamike mimi ni mkrsitu nimeamua kutafuta Shekhee kwa ajili ya kufanya dua sababu nimeona wachungaji wamekaa kiupigaji tu..niliungwanishwa na mtumishi GEO Dev sasa kabla sijampigia natakiwa nimtumie Sh.Elfu kumi kwenye simu yake alfu baada ya hapo nataja matatizo yangu alfu nitaambiwa gharama sasa hapo ni hospital au? Naombeni msaada wakuu naamini humu kuna watu ambao kwa namna moja au nyingine walipitia magumu mbali mbali walijua walivyojichomoa kutoka huko mimi nipo Dar, Tabata Bima...Nipo kwenye tanuri la moto jamani....
 
Huyu hana elimu, wana JF hebu muelimisheni huyu, ana amini miujiza badala ya kujiajiri au kuendelea kutafuta kazi
 
Huyu hana elimu, wana JF hebu muelimisheni huyu, ana amini miujiza badala ya kujiajiri au kuendelea kutafuta kazi
Elimu ninayo mkuu ila mambo yamekwama tu kujiari si ndo hivyo nimeenda hadi huko kulima nimekuambia kilichotokea au hujaelewa? wewe kama unamsaada saidia sio kuanza majungu
 
Jiombee mwenyewe Mungu anasikia kila mtu huhitaji mtu mwingine akufanyie maombi.
 
Ndugu hapo naona kabisa kuna jambo linalosababisha kukwama na afadhali umeliona mapema. Mimi nimekuwa na uzoefu huo kwa miaka mingi sana licha ya kuwa na fedha nzuri za miradi niliwekeza kwa miaka saba lakini hakuna matokeo yoyote na hata baada ya kumaliza elimu kubwa ngazi ya udaktari (PHD) bado kazi haikupatikana kwa mwaka na nusu. Nilikuwa nikiomba Mungu kila wakati na mwaka huu mwanzoni Mungu alituma waombaji na kuniombea pamoja na familia yangu yote na baada ya wiki 3 tu niliitwa kwenye usaili na baada ya wiki 4 hivi nikaitwa kwenye usaili ya kazi kutoka Marekani lakini inafanyikia kusini mwa Africa. Mambo yangu mengi yalikwama ikiwa ni pamoja na migogoro katika kila ardhi niliyonunua!

Hivi sasa naandaa safari na kwenda kazini na kazi yenyewe ni nzuri na yenye kulipa mshahara zaidi ya anaopata waziri hapa Tz. Nasema Bwana YESU asifiwe!

Nakushauri mpendwa kwanza usiombewe na shekhe, utapoteza muda wako, pili hata kwa huyo Geo Davie ni uzushi tu nafikiri anatumia nguzu za kipepo na sio mtumishi wa Mungu aliye hai. Nitakupatia number ya watumishi wa Mungu wakuombee ulipo, kama upo Moshi au Arusha watakuja hadi nyumbani kwako wape nauli tu. Kama upo mbali na Moshi basi mtaongea kwa simu na mambo yatakwenda sawa. Tafadhali wasiliana na namba hizi na uwaeleze matatizo yako wapo Moshi Masama. 0656491487 Kuwa na imani Mungu atatenda yote kwa kupitia Yesu Kristo Mwokozi wetu. Ubarikiwe.
 
Mkuu fazil asante sana kwa ushauri ubarikiwe sana sana kiukweli asante narudia japo nimechelewa kujibu Mungu akubariki sana nimesoma maelezo yako yamenibariki na kunitia nguvu upya ubarikwe sana.
 
Back
Top Bottom