Msaada wa Kumshtaki anayekuzushia Uongo

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
4,137
3,323
Habari zenu waungwana. Kama kichwa cha habari kilovyo. Ninaomba kujua ni hatua gani za kisheria naweza kuzichukua kwa watu wananizushia kwa lengo kunichafua.

Hili suala limeniumiza kwa muda mrefu hapa kazini kwangu, nimefadhaika na kukwazika sana. Nimejitahidi kuwaonya wahusika lakini hawakomi. Hali ikiendelea hivi naweza ugua ugonjwa wa presha hivi hivi.

Sasa naomba mnieleweshe nawezaje kutatua tatizo hili kisheria kama ifuatavyo:

1. Ni kwa mujibu wa sheria ipi wahusika watakuwa wamekiuka?
2. Ni ushahidi gani unahitajika kwenye kesi hii
3. Ikiwa watabainika na hatia ni adhabu ipi watapata?

Ni matumaini yangu mtanisaidia.
 
Cha msingi km walivyosema wenzangu JE UNEZUSHIWA NNI??? (Kuzushiwa ni kutolewa maneneo/picture kwa mtu wa tatu (third party) ambayo sio kweli (ya uongo) na yanakuadhiri kwa watu/jamii kukuepuka, kukudharau, kuwa na chuki na wewe na kukuondolea heshima yako uliyokuwa nayo awali.

HOJA
1. Je maneno/picture hizo ni za uzushi?
2. Je uzushi umefka kwa third party?
3. Ni kweli umeadhirika na uzushi huo?

HATUA ZA KISHERIA (km ulivyoomba)
1. Fikiria ni kiasi gan cha pesa ukilipwa utapata nafuu
(e.g 1,000 10,0000, 100,000 1,000,000 10,000,000. Etc
2.Nenda kwa mwanasheria akwandikie hati ya madai (PLAINT)

3.Hati hyo utaipeleka mahakamani (kuanzia ya wilaya etc kulingana na kiasi utakachodai) ila sio ya rufaa. (Mwanasheria anajua sna atakwelekeza)

4.Mahakaman utalipia ada ya usajili wa kesi (kulingana na kiasi utakachodai)

5.Kesi yako itakuwa imesajiliwa rasmi na itasikilizwa

NB; Hii ni kwa mjibu wa sheria tulizozipokea za Uingereza (LAW OF TORTS) ni mila za Uingereza na ndo maana nimeesema itakuwa kuanzia mahakama ya wilaya. Ya mwanzo haina uwezo kusikiliza mila tulizotoa Uingereza kuanzia tarehe 22 July 1922.

USHAURI WANGU!
Usifikilie mahakama zaid kuliko suluu nyingine. So mwandikie notisi ya kukuomba msamaha na akanushe uzushi wake km alivyo ueneza heshima itarudi!.
 
Nashukuru sana kwa maelekezo muhimu
 
Back
Top Bottom