Wala hakuna shida nitakuelekeza.
1.0 Hii ni forums na wala si blog kama ulivyosema.
2.0 Pili unapost uzi kama huuoni njia za kuupata ni,
(a) Kwenda jukwaa husika ulilopost na kuitafuta,
(b) Kuitafuta thread yenyewe kwa kutumia kitufe cha search ambacho kipo kulia kwa juu kama unatumia desktop.
(c) Kwenda kwenye profile yako mwenyewe na kuangalia
latest thread kisha click utaiona.
3.0 Thread kutoonekana kunachangiwa na thread yenyewe kutochangiwa na watu baada ya kuispost.
Kwa hiyo thread zinazokaa first and second page ni zile ambazo members wanareply mara kwa mara.
Mwisho ili uzi wako uweze kuwa replied sana unatakiwa kufanya nini sasa.
Kwanza unatakiwa kuweka heading nzuri itayovutia watu.
Pili, heading iendane na content yake. Siyo mathalani unasema matokeo ya CCM Nec halafi ndani unasema mwenye taarifa atujuze zaidi juu ya matokeo. Ni wazi hapo lazima uambulie matusi kwa sababi heading ni sahihi na ni habari ambayo watu wengi wangependa kuisikia lakini ndani haiendani na heading.
Mwisho ni jinsi unavyoandik habari yako. Watu wengi wanasahau kuweka paraghaf hivyo habaro kukosa mtiririko mzuri kwa msomaji.
Pia ukishapost usipitee kabisa jukwaani maana kuna watu ambao watakuwa wanahitaji kujibiwa kama hawajaelewa.