Msaada wa kujua kuendesha gari/ Driving school

Msaada wa kujua kuendesha gari/ Driving school

wilch

New Member
Joined
Jul 26, 2015
Posts
2
Reaction score
5
Habari wadau,

Driving school gani au mwalimu gani Mzuri sana wa gari kwa Dar es Salaam ambae anaweza kumsaidia mtu ambaye hana confidence kabisa ya kuendesha gari (ana uoga sana) ukizingatia alishawahi kwenda driving school mara mbili katika vipindi tofauti lakini bado hajui

Msaada jamani wadau nitashukuru sana mkinipa ushauri/ suluhisho.
 
Gari mtafute dereva wa Taxi mtaani au mwenye Bolt/Uber ongea nae kwa siku amfundishe gari huko vyuoni wanajifunza sana sheria ila kwa kukalia gari ni dakika chache sana anapewa Lena mwingine wapo wengi usione hapa watu wanashangaa ila kuendesha gari sio swala dogo kwa watu waliochelewa kujifunza.
 
Hizi auto wengine tulianza kwa kuambiwa maana ya D,d1, p na r!

Chuo ni muhimu kwa Sheria tu, lkn Sheria zote zipo online.

Huyo muoga atakuwa mkeo, wape vijana wamfundishe.

Ukimfundisha wewe utaambulia kumzaba makofi na mkaanza kununiana tu
😂😂😂 umenikumbusha mbali sana, mm wangu nimemfundisha mwenyewe .

Alikuwa ananikera sana.
Siku ya kwanza tu eti anataka nimfundishe kwanza jinsi ya kuwasha taa full , indicator , hazards na zile alama nyingne.

Nikamwambia mm ndio mwalimu wako, hizo kujifunza hata nusu saa tu unaweza. La muhimu ni kuweza kuendesha gar kwanza na ndio somo gumu sio hilo la taa.

Akanuna 😂😂😂
 
Back
Top Bottom