Msaada wa kujiondoa kwenye malipo ya Google pay

Msaada wa kujiondoa kwenye malipo ya Google pay

Jbst

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2020
Posts
1,981
Reaction score
4,116
Wakuu habari weekend? Mimi sio mtu wa mitandaoni na sidhani kama nafahamu vitu vingi kuhusu hayo malipo yanavofanyika Google.

Kuanzia 2020 kuna App nilikua nalipia kila mwezi ili kupata kile ninachokihitaji kwao ila kwasasa App hii siihitaji tena na nilishaifuta siitumii.. nina kama miezi 10 siitumii ila cha ajabu ni kwamba kila mwezi wanakata pesa kwenye airtel money yangu bila ridhaa yangu wakati mimi siitumii hiyo App!

Msaada kwa anaefahamuwa kujiondoa ili wasiendelee kukata pesa zangu kila mwezi na kama kuna njia ya kufanya ili pesa zangu kurudishwa. Hapa muda huu wamekata pesa yaani hata sielewi kwann inakuwa hivi!!

Ni mwezi wa 7 huu kila wanakata tu na nikiwasiliana na airtel naona ubabaishaji hakuna msaada wa kueleweka.

Nimekua nikiwasiliana na airtel kuzuia pesa yangu kila wanapokata ila wao airtel wanatuma tu link et niende kuzuia mwenyewe na hawana msaada wowote lkn ukiingia huko kwenye link hakuna la maana ni ubabaishaji tu.

Kwa anae fahamu hebu anisaidie hapa
 
Wakuu habari weekend? Mimi sio mtu wa mitandaoni na sidhani kama nafahamu vitu vingi kuhusu hayo malipo yanavofanyika Google...
Pia ilinisumbua lakini baadae nikaitoa, ukiweza kupata sms wakati unajiunga ina menu ya kubonyeza na kujitoa..
 
Futa hiyo kadi ya airtel Mastercard then hapo card haitokuwa active tena

Ubaya wa airtel ni kuwa Mastercard inauganishwa direct na account yako ya kawaida ya Airtel money

Ila vodacom ina afadhali unatenga hela za Mastercard zinakaa kwake na Hela za Mpesa zinakaa kwake
Nielekeze vizur mkuu
 
Nimefuta lkn wanasema nambq haiajaunganishwa na mastercard!! Sasa kama haijaunganishwa nani ana kata?

Airtel ni vibaka
 
Nimefuta lkn wanasema nambq haiajaunganishwa na mastercard!! Sasa kama haijaunganishwa nani ana kata?

Airtel ni vibaka
Airtel ni majambazi
Screenshot_20230326-235629_Messages.jpg
 
Wakuu habari weekend? Mimi sio mtu wa mitandaoni na sidhani kama nafahamu vitu vingi kuhusu hayo malipo yanavofanyika Google...
Hapa airtell utawaonea bure tu engagement yako ni ya third part airtell ana facilitate tu hayo malipo deal na play store
 
Fungua play store yako, halafu angalia kiduara kilicho pembeni ya alama ya kengele click then nenda kwenye payments and subscription, halafu unsubscribe
Asante sana mkuu nimeikuta hiyo applications na nime unsubscribe. Asante sana
 
Hapa airtell utawaonea bure tu engagement yako ni ya third part airtell ana facilitate tu hayo malipo deal na play store
Na waonea bure ki vp? Wanatakiwa warudishe pesa au wazuie sasa wenyewe hata kunisaidia tu namna ya kufanya ila wanaleta ubabaishaji
 
Fungua play store yako, halafu angalia kiduara kilicho pembeni ya alama ya kengele click then nenda kwenye payments and subscription, halafu unsubscribe
@wilcoxon mkuu kama unafahamu njia ya kurudisha na pesa nisaidie pia hii waliochukua nairudisha vp?
 
Fuata hatua hizi.
1. Tenegeneza virtual card mpya ya airtel
2. Nenda playstore update taarifa za malipo kwa kuweka virtula card mpya uliyotengeneza.
=
Muhimu
3. Rudi tena kwenye menu ya airtel na DELETE hiyo virtual card uliyotengeneza awali (na kuweka taarifa zake playstore.)
4. Hapo utaona kuwa kule playstore zitabakia taarifa za virtual card ambayo TAYARI umei_delete | Hivyo hakuna makato tena utakayokatwa kwenye laini yako ya airtel kila mwezi.
 
warudishe pesa au wazuie sasa wenyewe hata kunisaidia
Kuzuia ni jukumu lako

Hapo juu umepewa njia tatu za kuzuia

1. Kupitia email yako
2. Kupitia app ya playstore
3. Kupitia virtual card | Nimeeleza hapo juu.

Wewe ndio unapaswa kuchukua hatua. na hutakiwi kuwalalamikia watoa huduma.
 
@wilcoxon mkuu kama unafahamu njia ya kurudisha na pesa nisaidie pia hii waliochukua nairudisha vp?
Kama unataka kurudisha nenda hapo kwenye payments and subscription kisha uende kwenye budget & history then omba kurefund lakini hii itawezekana ndani ya masaa 48 toka makato yalipofanyika.
 
Kama unataka kurudisha nenda hapo kwenye payments and subscription kisha uende kwenye budget & history then omba kurefund lakini hii itawezekana ndani ya masaa 48 toka makato yalipofanyika.
Muamala haujafikisha hata masaa 24 ila ukienda hapo budget&history hakuna sehemu ya ku refund@wilcoxon
 
Back
Top Bottom