Wakuu habari weekend? Mimi sio mtu wa mitandaoni na sidhani kama nafahamu vitu vingi kuhusu hayo malipo yanavofanyika Google.
Kuanzia 2020 kuna App nilikua nalipia kila mwezi ili kupata kile ninachokihitaji kwao ila kwasasa App hii siihitaji tena na nilishaifuta siitumii.. nina kama miezi 10 siitumii ila cha ajabu ni kwamba kila mwezi wanakata pesa kwenye airtel money yangu bila ridhaa yangu wakati mimi siitumii hiyo App!
Msaada kwa anaefahamuwa kujiondoa ili wasiendelee kukata pesa zangu kila mwezi na kama kuna njia ya kufanya ili pesa zangu kurudishwa. Hapa muda huu wamekata pesa yaani hata sielewi kwann inakuwa hivi!!
Ni mwezi wa 7 huu kila wanakata tu na nikiwasiliana na airtel naona ubabaishaji hakuna msaada wa kueleweka.
Nimekua nikiwasiliana na airtel kuzuia pesa yangu kila wanapokata ila wao airtel wanatuma tu link et niende kuzuia mwenyewe na hawana msaada wowote lkn ukiingia huko kwenye link hakuna la maana ni ubabaishaji tu.
Kwa anae fahamu hebu anisaidie hapa