Msaada wa kufuta group la Facebook

Msaada wa kufuta group la Facebook

Habari wana jf , kuna group la face book limefunguliwa ili wanitukane naomba msaada wa kulifuta nikiwa sio memba wa group hilo. Asanteni
Nenda Cyber crime Police department- Report (watafunguwa Jarada- watawasiliana na Facebook HQ kisha FB wataifunga. Wewe ata kama utaweza (kupitia Backdoor) Kuifunga- Facebook watakushtaki kwa kuingilia mtandao wao. So nenda police
 
Hivi huwezi kuwablock usiwaone?

Usipowaona hutaweza kujibu mashambulizi na wao wataishia kupotea tu.

Atakekufowardia ujumbe uliotumwa kule mtahadharishe kwamba utamblock pindi akikutumia next time.

Cha muhimu ni kuwa USIWAJIBU LO LOTE LILE.
 
Click group halafu hivyo vidotihapo bonyeza Sasa click leave the group na unfollow the group kama hujaelewa ni tag nikutumie screenshot
Kasema yeye sio member wa group, anaanzaje kuleave group
Mleta mada anakula mademu za watu sasa watu wameanzisha group special kivyao ili wawe wanamtukana[emoji38][emoji38]
 
Sasa anasomaje comment kama sio member
Kwenye Facebook kuna option ya View group unaweza kuingia kwenye group ukaangalia posts ukasoma comments na magroup mengine unaweza hata kucomment bila ya ww kuwa member. Baadhi hayaruhusu hata kuview ikiwa ww sio member
So, anaweza kuona matusi hata kama sio member [emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom