Msaada wa kufikisha malalamiko kwa Mh. Rais au Waziri Mkuu

Wanajamvi naombeni msaada wa kufikisha malalamiko yangu kwa wakuu hawa, kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa na Afisa elimu S/M.

Mke wangu amekuwa akiomba uhamisho toka mwaka 2014 kutokana na matatizo mbalimbali ya kiafya. Anasumbuliwa na presha ya kushuka, madonda ya tumbo pia ni mjamzito.

Toka mwaka 2014 amekuwa akiomba uhamisho wa hiari asogee karibu na hospitali, Afisa Elimu huyu amekuwa akikataa kumuhamisha. Kinachosikitisha sasa hivi kaamua kumpa uhamisho wa malipo na kumpeleka mbali zaidi kwa kumkomoa.

Kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu huko alikompeleka imepelekea ujauzito wa mke wangu kuharibika.
Mmmmm toka 2014 ni mjamzito:)
 
Omba Mungu maradhi yanayo msumbua usiyapate katika maisha yako.usije ukajua wote wanaomba uhamisho kwa raha ,wengine ni matatizo.
Sijakejeli maradhi ya Mkeo...nimesisitiza tu kufuata taratibu na kutii mamlaka.

Kuwa na maradhi si kigezo cha kutotii mamlaka.

Huyo afsa elimu aliyemuhamisha lazima mlimtoa kwenye roho ya utu. Sidhani kama aliamua tu.

Ahsante.
 
Uhamisho kapewa mwezi wa 4 mwaka huu akiwa tayari mjamzito.kutokana na mazingira ya huko aliko pelekwa kwa mujibu wa daktari huenda ndiyo chanzo cha kuharibika ujauzito
Hicho Kijiji alichopelekwa hakuna watoto wanaozaliwa Huko??

Na hiyo mimba ulimpachikia wapi??
 
Sijakejeli maradhi ya Mkeo...nimesisitiza tu kufuata taratibu na kutii mamlaka.

Kuwa na maradhi si kigezo cha kutotii mamlaka.

Huyo afsa elimu aliyemuhamisha lazima mlimtoa kwenye roho ya utu. Sidhani kama aliamua tu.

Ahsante.
Nashukuru kwa kuwa hata huu ni ushauri,ila kama ni kuheshim mamlaka hakuna asie lijua hilo.Lazima ifike mahali na wewe ukubali kuwa kuna wakati pia hata wenye mamlaka wanakosea.
 
Aache tu kazi,physically unfit.mimba,madonda,pressure jumlisha na misongo ya mawazo,hawezi tena kufundisha huyo,anahasira mno,atauwa watoto wetu. Mpe pole sana.
Ushauri wako ni mzuri,ila hautatui tatizo.hata wewe kesho yanaweza kukukuta haya.maradhi si jambo la kebehi.hujafa hujaumbika.ila sikuombei hivyo.
 
Hicho Kijiji alichopelekwa hakuna watoto wanaozaliwa Huko??

Na hiyo mimba ulimpachikia wapi??
Mkuu sijamaanisha kuwa huko hakuna watoto,wataalam huwa wanatoa ushauri kulingana na matatizo ya mgonjwa husika haijalishi kule anakoenda kuna watoto au hamna.Tatizo ni pale unapowapelekea wahusika taarfa za kitaalam wanapuuza,halafu tatizo linakuja kutokea.
 
Wanajamvi naombeni msaada wa kufikisha malalamiko yangu kwa wakuu hawa, kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa na Afisa elimu S/M.

Mke wangu amekuwa akiomba uhamisho toka mwaka 2014 kutokana na matatizo mbalimbali ya kiafya. Anasumbuliwa na presha ya kushuka, madonda ya tumbo pia ni mjamzito.

Toka mwaka 2014 amekuwa akiomba uhamisho wa hiari asogee karibu na hospitali, Afisa Elimu huyu amekuwa akikataa kumuhamisha. Kinachosikitisha sasa hivi kaamua kumpa uhamisho wa malipo na kumpeleka mbali zaidi kwa kumkomoa.

Kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu huko alikompeleka imepelekea ujauzito wa mke wangu kuharibika.
mkeo nae, anakaaje na ujauzito miaka yote hiyo. toka 2014
 
Ushauri wako ni mzuri,ila hautatui tatizo.hata wewe kesho yanaweza kukukuta haya.maradhi si jambo la kebehi.hujafa hujaumbika.ila sikuombei hivyo.
Hujanielewa tu,mie pia ninaweza au ninamagumu kuliko hayo,ila inabidi niwe na maamuzi magumu wakati fulani kwa ajili yangu binafsi.Wala simkebehi ila ndo hali anayopitia. Hizi kazi hatukuzaliwa nazo mkuu na ukifa inapata mwingine.
 
Wanajamvi naombeni msaada wa kufikisha malalamiko yangu kwa wakuu hawa, kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa na Afisa elimu S/M.

Mke wangu amekuwa akiomba uhamisho toka mwaka 2014 kutokana na matatizo mbalimbali ya kiafya. Anasumbuliwa na presha ya kushuka, madonda ya tumbo pia ni mjamzito.

Toka mwaka 2014 amekuwa akiomba uhamisho wa hiari asogee karibu na hospitali, Afisa Elimu huyu amekuwa akikataa kumuhamisha. Kinachosikitisha sasa hivi kaamua kumpa uhamisho wa malipo na kumpeleka mbali zaidi kwa kumkomoa.

Kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu huko alikompeleka imepelekea ujauzito wa mke wangu kuharibika.
kaka mmefunga ndoa? maana kama mna ndoa sheria ipo wazi kabisa angetoka kukufuata mume wake ulipo kwa kuambatanisha cheti halali cha ndoa si kuomba kusogea karibu na hospital kwa kuwa pressure,vidonda vya tumbo havina haja ya kuishi mjini maana asilimia kubwa ya jamii ya leo wanahayo matatizo na huenda karibia robo tatu ya wafanyakazi huko alipo wana hayo matatizo pia.
 
Vyeti vya ndoa vipo na viliambanishwa kwenye maaombi ya uhamisho huu,kusogea karibu na hospitali ni ushauri aliopewa na madaktari si hivyo tu hata kulala chumba cha peke yake hakushauriwa.kwa kuwa presha inaposhuka huwa hajiwezi kabisa.
 
Hujanielewa tu,mie pia ninaweza au ninamagumu kuliko hayo,ila inabidi niwe na maamuzi magumu wakati fulani kwa ajili yangu binafsi.Wala simkebehi ila ndo hali anayopitia. Hizi kazi hatukuzaliwa nazo mkuu na ukifa inapata mwingine.
Ni sahihi unachokizungumza,likini kwa nini mtu uyatumie mamlaka yako kuwakandamiza watu.
 
Back
Top Bottom