Msaada wa kufikisha malalamiko kwa Mh. Rais au Waziri Mkuu

BALAGASHIA

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
387
500
Wanajamvi naombeni msaada wa kufikisha malalamiko yangu kwa wakuu hawa, kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa na Afisa elimu S/M.

Mke wangu amekuwa akiomba uhamisho toka mwaka 2014 kutokana na matatizo mbalimbali ya kiafya. Anasumbuliwa na presha ya kushuka, madonda ya tumbo pia ni mjamzito.

Toka mwaka 2014 amekuwa akiomba uhamisho wa hiari asogee karibu na hospitali, Afisa Elimu huyu amekuwa akikataa kumuhamisha. Kinachosikitisha sasa hivi kaamua kumpa uhamisho wa malipo na kumpeleka mbali zaidi kwa kumkomoa.

Kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu huko alikompeleka imepelekea ujauzito wa mke wangu kuharibika.
 

Mtambwe

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
711
1,000
Wanajamvi naombeni msaada wa kufikisha malalamiko yangu kwa wakuu hawa,kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa na afisa elimu s/m.Mke wangu amekuwa akiomba uhamisho toka mwaka 2014 kutokana na matatizo mbali mbali ya kiafya.Anasumbuliwa na presha ya kushuka,madonda ya tumbo pia ni mjamzito.Toka mwaka 2014 amekuwa akiomba uhamisho wa hiari asogee karibu na hospitali afisa elimu huyu amekuwa akikataa kumuhamisha.kinacho sikitisha sasa hv kaamua kumpa uhamisho wa malipo na kumpeleka mbali zaidi kwa kumkomoa.kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu huko aliko mpeleka imepelekea ujauzito wa mke wangu kuharibika.
Wakati mwengine munapoandika habari zenu kuweni makini musiwe watoto.
Inamaana huyo mke wako ni mjamzito tangu 2014? Nina wasi wasi pengine ilikuwa ya Punda
 

ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,487
2,000
Aache tu kazi,physically unfit.mimba,madonda,pressure jumlisha na misongo ya mawazo,hawezi tena kufundisha huyo,anahasira mno,atauwa watoto wetu. Mpe pole sana.
 

BALAGASHIA

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
387
500
Uhamisho kapewa mwezi wa 4 mwaka huu akiwa tayari mjamzito.kutokana na mazingira ya huko aliko pelekwa kwa mujibu wa daktari huenda ndiyo chanzo cha kuharibika ujauzito
 

BALAGASHIA

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
387
500
Wakati mwengine munapoandika habari zenu kuweni makini musiwe watoto.
Inamaana huyo mke wako ni mjamzito tangu 2014? Nina wasi wasi pengine ilikuwa ya Punda
Sijamaanisha hicho ulicho elewa wewe,nimeambatanisha suala la ujauzito kutokana na uhamisho aliopewa mwezi 4 mwaka huu.
 

BALAGASHIA

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
387
500
Ngoja wajee

Bt umesemaa ni mjamzito alafu tena unasema mimba imeharibika haimake sense mkuu BT polee sana
Uhamisho huu aliopewa mwezi wa 4 mwaka huu alikuwa tayari ana ujauzito,kulingana na mazingira alikopelekwa inaonekana ni chanzo cha kuharibika mimba hiyo.
 

mitogwa

Senior Member
May 9, 2017
142
225
Sasa afsa elimu tu nae mpka uende ngazi hyo? Mkurugenz/Mkuu wa wilaya mpka Mkuu wa mkoa wako wapi??
 

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,966
2,000
Inaonekana wewe na mke wako ni wasumbufu sana kwa mamlaka.

Tiini na heshimuni mamlaka.

Inaonekana ni wazi kabisa Mkeo kwanza alisababisha usumbufu mwingi hapo kituoni kwake na hata huko utumishi.

Poleni kwa yaliyowakuta ila zama hizi angeweza hata poteza kazi.
 

BALAGASHIA

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
387
500
Inaonekana wewe na mke wako ni wasumbufu sana kwa mamlaka.

Tiini na heshimuni mamlaka.

Inaonekana ni wazi kabisa Mkeo kwanza alisababisha usumbufu mwingi hapo kituoni kwake na hata huko utumishi.

Poleni kwa yaliyowakuta ila zama hizi angeweza hata poteza kazi.
Omba Mungu maradhi yanayo msumbua usiyapate katika maisha yako.usije ukajua wote wanaomba uhamisho kwa raha ,wengine ni matatizo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom