Msaada wa Kudukuliwa

Samboko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2011
Posts
5,417
Reaction score
8,047
Habari wakuu,

Kuna uwezekano mtu akahaki taarifa za mawasiliano ya simu ya mkononi hata kama ukireset simu na kuondoa app zote za kudownload pamoja na email na bado akaendelea kupata taarifa za anaedukuliwa?
Naombeni msaada wakuu, maana nahisi nadukuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nisikilize kwa makini;
kama ulikua na passwords za accounts kama za google na accounts mbalimbali na uliandika username na passwords katika notes let say ukapiga picha, hata u flash hiyo simu akiipata mtu mwingine anauwezo wa kupata hizo details, yaani picha ndio zinakuua, sababu disc haina uwezo wakufuta moja kwa moja, unapofuta picha au ku flash simu, ile memory inafunika kwa juu yake ila haina uwezo wa kufuta kabisa, sasa unapewa simu imeflashiwa haina kitu lakini kama ni mjuzi unaichimba unapata mavitu kibao, kwahiyo uwezekano upo, kama uliflash simu na unahisi bado unadukuliwa badili google account(g mail) ile ya zamani achana nayo. hiyo kiasi flani itasaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna njia nyingi za kumdukua mtu, inategemea anamdukua kwa njia gani, it depends.

inawezekana anadukuliwa kwa kutumia
1. app iliyopo kwenye simu
2. account ya gmail
3 . sim card
4. external device ina intercept mawasiliano katika area aliyopo.

hayo yote yanawezekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi
 
Asante mkuu kwa ushauri, nikibadili email itasaidia au hawezi tena kupata details zangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo nifanyeje kukwepa kudukuliwa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaporeset simu inafuta apps zote na kubakisha system apps. Hivyo inategemea na hio app ya udukuzi imeekwaje.

Kama ilipewa root access na kufanywa kama system app hata uki reset haitasaidia maana system apps hazifutiki unapo reset. Mfano unaporeset simu app ya gallery haifutiki sababu ni system app.

Kama ni app ya kawaida tu basi uki reset itatoka.

Pia inategemea na udukuzi kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, sio lazima iwe imedukuliwa simu pengine anajua password ya email yako. Mfano app zote za google unatumia account moja mtu akiwa na password ya gmail anaweza ona backup ya sms, msg za whatsapp kama unafanya backup ya gdrive, backup ya picha etc.
 
Asante kwa maelezo mazuri Chief-Mkwawa
Je kuna namna naweza jua kama nadukuliwa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa maelezo mazuri Chief-Mkwawa
Je kuna namna naweza jua kama nadukuliwa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Nakushauri badili password za email zako kwa sasa.

2.ingia playstore search app inaitwa glasswire eka kwenye simu yako. Yenyewe ni kama firewall itakuambia kila app inatumia kiasi gani cha data. Mfano kuna app huitumii na inakula data nyingi unaweza ukaileta hapa tui discuss na kuiangalia kama ni suspicious.
 
Asante mkuu, ngoja nilifanyie kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…