Msaada wa kubadili jina la riwaya yangu

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Nina omba msaada kama kuna mwana fasihi mwenzangu mwenye akili ndefu kama zangu aje aungane na mimi abadali content nzima ya riwaya yangu ya Shimo la taka ndani ya Ikulu na sasa aihamishe iitwe Shimo la taka ndani ya wizara ya fedha.

Miaka mitatu iliyopita nilianza kuandika riwaya hii na niliwahi kuomba kama naweza pata mtu anae weza kuhariri kupitia Jf nikakosa. Niljikuta nipo mikononi ya Rastafale mmoja yupo Marekani ila ni mbogo, tulitofautiana pahala padogo alipo omba malipo.

Nikahisi amenipigia na kitu kizito, yaani nilipe pesa yangu itoke Bongo mpka Marekeni? Mjomba wangu mmoja mkulima wa kahawa kutoka kijiji cha Itongo wilaya ya Muleba, niliwai mpigia simu kumuomba anipe hela mwaka mmoja uliopita.

Aniuliza kwa herufi kubwa hivi sifi leo ulishawai ona pesa inatoka kijijini kwenda mjini? Nikajibu sijawahi, akasema na hutuiona. Labda serikali kama ilivyo amua sasa hivi kuweka tozo kila pahala, ndiyo sasa hivi nadai akienda kutoa pesa M-Pesa inakatwa na wanadsm walio Voda makao makuu vinginevyo pesa yake isingekanyaga mjini.

Niliumia sana maana nilipanga riwaya yangu ikiwa tayari nimwalike marehemu Mwendazake, aje aifungue (ilipanga hivi ila Mungu akapanga hivo). Wakati naanza kuandika riwaya hii niliwasiliana na rafiki yangu anaitwa "Rwambogo," nikamweleza nia yangu ya kutunga riwaya hii, aliniambia sitoweza kwa sababu mbili.

Mosi kichwa cha habari kilisadifu yakuwa nilikuwa namdhahaki Mwendazake, kwa hiyo nitaogopa kuitoa.
Pili aliniambia ndugu yangu sifi leo siku hizi unakula na kushiba bwana uwezi andika riwaya ambayo inalenga ukumbozi wa fikra za watu wa hali ya chini ilihali unashiba sio kama wao.

Nikiliwazi wakati wa raha, mathalani nikiwa pahala na wanangu tunakula vyetu sijawai andika hata mstari mmoja na sasa nipo ukurasa wa 222. Nikiliwazi riwaya hii nilijua wazi ikikamikika basi ningetakiwa kufa au kuhama nchi enzi za Mwendazake.w

Kwakuwa yeye alipenda kusifiwa nilikuwa nimetenga ukurasa mmoja wa kumsifia kwa kutumia jani la karagwe kwa kipindi kirefu ila kichwa chake hakikuwai haribiwa. Niachane na porojo nyingi miongoni wa watu nisio waelewa ni Mwigulu Lameck Mwichemba (mmiliki bandia kama original wa Ester Coach) lazima nikiri simwelewi kwa matendo yake, na maamuzi yake, na matamshi yake.

Sasa kwa kuwa riwaya ililenga Ikulu nipo tayari kuibadili jina lake badala ya "Shimo la taka ndani ya Ikulu" iwe "Shimo la taka ndani ya wizara ya fedha". Ombi kubwa kwa Waziri naomba aoneshe orodha ya walio omba kutozwa tozo na kodi Tanzaniia ili hali kila huduma tunanunua, ni haki?

Kutoa elimu bure tena elimu chakavu ndo wajitambe hivyo? Kama siyo elimu bure chakavu ajake ni watoto wake wangapi wanasoma huko? Ni mtoto wa Samia yupi au mjukuu yupi anasoma elimu hiyo ya bure? Nani asiye penda cha bure ili aburudike?
Nihitaji mtu wa kushare nae muda ili tuibadili riwaya hii jina lake.
 
Nina omba msaada kama Kuna mwanafasihi mwenzangu mwenye akili ndefu kama zangu aje aungane na Mimi abdali content nzima ya Riwaya yangu ya Shimo la taka ndani ya Ikulu na Sasa aiamishe iitwe Shimo la taka ndani ya wizara ya fedha.

Miaka mitatu iliyopita nilianza kuandika Riwaya hii na niliwai kuomba kama naweza pata mtu anae weza kuhariri kupitia. Jf nikakosaa niljikuta nipo mikononi ya Rastafale mmoja yupo Marekani ila ni mbogo tulitofautiana pahala padogo alipo omba malipo,nikaisi amenipigia na kitu kizito yaani nilipe pesa yangu itoke Bongo mpka marekeni?mjomba wangu mmoja mkulima wa kahawa kutoka Kijiji Cha itongo wilaya ya Muleba niliwai mpigia simu kumwomba anipe Hela, mwaka mmoja uliopita, akiniuliza kwa herufi kubwa hivi@sifi Leo ulishawai ona pesa inatoka Kijijini kwenda Mjini?nilikujibu sijawai akasema na hutuiona,labda serikali kama ilivyo hamua Sasa hivi kuweka Tozo Kila pahala, ndo Sasa hivi anadai"akienda kutoa pesa M pesa inakatwa na. Wanadsm walio Voda makao makuu vinginevyo pesa yake hisingekanyaga mjini.

Niliumia sana MAana nilipanga Riwaya yangu ikiwa tayari nimwalike Marehemu Mwenda zake, aje aifungue.(Nilipanga hivi ila Mungu akapanga hivo).
Wakati naanza kuandika Riwaya hii niliwasiliana na rafiki yangu anaitwa, 'Rwambogo,"nikamweleza niia yangu ya kutunga Riwaya hii aliniambia sitoweza Kwa sbabu mbili.
Mosi kichwa Cha habari kilisadifu yakuwa nilikuwa namdhahaki mwendazake,kwa hiyo nitaogopa kuitoa.

Pili aliniambia ndugu yangu sifi leo siku hizi unakula na kushiba bwana uwezi andika Riwaya ambayo inalenga ukumbozi wa fikra za watu WA Hali ya chini ilihali unashiba sio kama wao.
Nikili wazi wakati wa Raha, mathalani nikiwa pahala na wanangu tunakula vyetu sijawai andika hata mstari mmoja na Sasa nipo ukurasa wa 222. Nikili wazi Riwaya hii nilijua wazi ikikamikika basi ningetakiwa kufa au kuhama nchi enzi za mwendazake.kwa kuwa yeye alipenda kusifiwa nilikuwa nimetenga ukurasa mmoja wa kumsifia Kwa kutumia Jani la karagwe Kwa kipindi kirefu ila kichwa chale hakikuwai haribiwa.
Niachane na porojo nyingi miongoni wa watu nisio waelewa ni Mwiguru Lameck Mwichemba(mmiliki bandia kama original waa ester coach lazima nikili simwelewi kwa matendo yake, na maamuzi yake,na matamshi yake na Sasa Kwa kuwa Riwaya ilirenga Ikulu nipo tayari kuibadili jina lake badala ya Shimo la taka ndani ya Ikulu iwe Shimo la taka ndani ya wizara ya fedha.
Ombi kubwa kwa Waziri naomba aonneshe orodha ya walio omba kutozwa tozo na Kodi tanzaniia Ili hali kira huduma tunanunua ni naji?
Kutoa elimu Bure Tena elimu chakavu ndo wajitambe hivyo?kama sio elimu Bure chakavu atake ni watoto wake wangapi wanasoma huko?ni mtoto wa Samia yupo au mjukuu yupi anasoma elimu hiyo iliyoya Bure?nani hasiye penda Cha burerer Ili aburudike?
Nitaji mtu wa kushare nae muda Ili tuibadili Riwaya hii jina lake.
Andika:SHIMO LA TAKA KWETU NYUMBANI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom