Msaada wa kuachana na my wife

Kwa kweli inasikitisha sana mtoto wa miaka mitatu anakwenda boarding school?anakosa malezi ya wazazi wote wawili mapema,sipati picha ni taifa lipi tunalijenga la baadaye.

kwa ufahamu wangu mama anatakiwa akae na mtoto mpka miaka saba ndio baba unaweza kumchukua,kuhusu kumlipia nyumba sidhani kama lina mantiki, nachofahamu ukikaa na mwanamke kwa miezi sita mfufulizo sheria ya ndoa inatambua ni mkeo.

kama atafuate sheria mwache afuate then intavunjwa mahakamani haya ya kulipiana kodi haya msingi wowote.

pole sana thats life
 
na nyie msiwe mnaendeshwa kama magari ya dubai au ya japani ovyo eti kisa umelipia MV au insurance.

I wish to see that lady.Ni wa ajabu hata sijawahi kuona anajivunia nini kwa kumtreat mwenzie hivyo?

Anyway kwa kumlazimisha huyo bwanae amlipie kodi ya nyumba wakati hawapo pamoja na kulazimisha ndo ifungwe kwa kuzingatia ulokole kamwe haileti maana ila ninachodhani kuna kitu hakikusemwa na mleta mada kinachopelekea huo ugomvi.

Ni nini chanzo cha huyo dada kuokoka?

walikubaliana na mzazi mwenza?
Je wakati wanapanga masuala ya kufunga hiyo harusi alikuwa bado kuokoka au hakumshirikisha na uamuzi wa kuokoka?

Jamani tujaribu kuwa na moyo wa utu siku zingine kwa kuwa wote tu viumbe vya mungu huyohuyo./

Kwa nini tyuwapelekesha kwa starehe ya inayowapa raha wote wawili?
acheni kujishusha mtu unapata mshahara mkubwa kuliko mwananume halafu hutumii zako unataka kutoboa mfuko wa mwenzio maana yake nini.

Kikubwa amuweke chini amwambie kila kitu na madhara ya baadae kwa mtoto na wote kwa pamoja na kama mwanamke akipenda kumshitaki mimi nitakuwa wakili kwa upande wa huyo mwananume .

Kwa upande mwingine tumezidi kuwaonea hawa ndugu zetu ilhali ndo waliotoa ubavu wao ili tuwepo duniani.
 
Una bahati umeuliza,siku hizi kuna ma pastor from Nigeria pale TZ,wao wanachofanya ni kula wake za watu na wasichana ambao ni bikira na ambao wako desperate na either pesa,love,marriages,kazi and the likes.
Yaani huwezi kuamini,lakini wasichana graduates na F4 na d F6 ndio wanakwanguliwa kweli na hao Nigerians na counter part zao waswahili. Msichana anaaambiwa vua nikuwekeee upako anavua,anakuja kujiangalia,tayari pastor aliishamaliza kazi.Nina dada kabisa ana mtoto wa pastor fake na dada kilichomponza ni kutaka kuolewa,upako ukaja na mimba.
Ninachokushauri kama ameishaleweshwa na hao ma pastor na akanywa ulevi wao,mtafaute dada yako au jamaa wa karibu akulelee huyo mtoto,maana by the time huyo dada anakuja ku realise anaweza hata akawa ameishabeba haya magonjwa yetu. Wewe usifuate cha sheria wala nini,muache yeye ndie afuate sheria ambayo kama unasema ukweli huenda ikakusaidia.
 
Hivi nikiishi au nikiwa na nyumba ndogo miezi 24 je mahakama pia itahalalisha na kutambua kuwa huyu ni mke wangu??
 
Last edited:
Watu wanashindwa kujua kwamba wokovu upo kila kanisa. Unaweza kuokoka ukiwa ndani ya kanisa lako si lazima uhame kanisa na kwenda kwenye makanisa mengine. Mungu ni huyu huyu wote tunayemwabudu lakini matendo yako ndiyo WOKOVU wako. Wamama wengi wanadanganyika na hizi imani kwamba yesu yupo huku nao wanaamini. Yesu yupo kwa ajili ya kila mtu matendo na maisha yako ndiyo yatakayomkaribisha yesu kuwa nawe.
Kikubwa pia ambacho wamama wengi wanakimbilia kwenye kuokoka ni matatizo yaliyopo ndani ya nyumba hasa katika swala la mahusiano. Wengi wanashindwa kujua ni vyema kutatua tatizo kabla ya kukimbilia kwenye kuokoka ambako hawajui hata maana ya wokovu. Mimi ningekushauri ukae na mkeo mjaribu kushauriana na kuelewana kabla hamjafikia hatua ya kutengana hasa mkiangalia swala la mtoto ambaye hajui lolote.
msifanye maamuzi ya kuachana kwa kuridhisha haja za miili yenu bila kuangalia madhara yatakayompata mtoto siku za mbeleni
 
Mkuu wiki kama tatu zilizopita kuna dada mmoja wa RITA alikuja kazini kwetu kutupa semina juu ya haya mambo ya Urithi na Ndoa. Alisema kisheria kama hakuna cheti cha ndoa ya aina yoyote ile basi mahakama haitambui uwepo wa ndoa hata kama mmeishi miaka 10, watu wanajidanganya wanasema eti mkiishi sijui miezi sita kama mke na mume under one roof eti yule ni mkeo kisheria hakuna kitu km hicho, sheria haitambui so kuna kitu hapo amesema eti umlipie kodi ya nyumba anakohamia ama laa atakwenda mahakamani, asikutishe mkuu akifika mahakamani ataulizwa km yeye ni mke halali wako, akisema yeye ni mke halali ataulizwa chei cha ndoa kiko wapi hapo lazima apige kimyaaaa, so plse may peace be with you.
 
A wife should give a good balance in life ....huyo kaka hapana!

Hebu check mke hapa wajibu wake....

5699d1251133092-a-image002.jpg
 
Pole sana jamaa yetu kwa hayo yaliyokukuta.
Ushauri wangu kwako:
1. Huyu si mke mwema,
Jamani mlokole aliyeokoka maana yake hana dhambi (kwa mujibu wa walokole). Lakini kwa matendo hayo aliyoyafanya kama ni kweli basi hapo ana madhambi makubwa sana. Kwa mtazamo wangu huyo hafai kabisa.

2. Kuhusu mtoto:
Mtoto bado ni mdogo sana na anahitaji malezi ya baba na mama. Kwa kuwa yeye hataki basi tumia njia yoyote ile ya kumlea mtoto wako bila kujali masharti anayotoa mkeo. Mgharamie mtoto wako kila kitu anachohitaji maana ni haki yake.

3. Kuhusu wewe Gamaha.
Mkeo (japokuwa sipendi sana kumwita mkeo kwa tabia aliyonayo) ana kipato kikubwa zaidi kuliko wewe, kwa hali hiyo ana uwezo wa kujitegemea, kwa hiyo usimlipie kodi ya nyumba aliyopanga hata senti moja, wewe lipia kodi ya nyumba unayokaa na mtoto wako tu na si vinginevyo.

LKN pia anataka nimlipie kodi ya nyumba yake atakayo hamia yeye kama yeye sababu mtoto atakuwa tayari shule na anasema nisipo fanya hivyo anaenda kwenye sheria.
Hapa hakuna sheria inayokubana alipe yeye mwenyewe usitoe hata senti.

lkn bahati mbaya au nzuri huyu mwenzangu alikuwa kaokoka. na akawa anadai kuwa kama nataka kumuoa basi tukafunge harusi kanisani kwao ambalo ni kanisa la kilokole.

Mimi si mwanasheria lakini kwa kawaida mwanamke anatakiwa kufuata dini ya mwanaume kama itabidi kuwa hivyo. Kama walivyochangia wachangiaji wengine, mnaweza kushauriana kama anashaurika mkafunga ndoa katika kanisa analotaka yeye lakini ukabaki na dhehebu lako la Lutheran.

Halafu naomba nikuulize Gamaha. Mkeo anataka mfunge ndoa kanisani kwao au anataka ubadili dini na kufuata ya kwake ya kilokole? ______________________________

Mkuu ni kwamba hataki mtoto akae na mtu yoyote si mama si dada wala nani... na yeye anasema atakuwa busy so option pekee aliyonipa ni kupeleka mtoto shule. hata mimi naona mtoto bado ni mdogo ila sina cha kufanya.
Sasa yeye anategemea nini? Wewe kama una ndugu zako au wengine unaoona wanafaa we waite wakae na mtoto.

Ngoja niishie hapo kwanza.
 
Pole sana ndugu yete. Nisingependa kurudia yaliyosemwa na wenzangu tayari, ila ningependa kukazia machache tu ili niweke uzito kidogo:

1. Kuhusu mtoto
Kwa hali yoyote ile, usikubali mtoto wa miaka 3 aende boarding hata siku moja. Baba yangu mdogo ni mtu tajiri, aliona hana muda wa kukaa na mwanae akampeleka boarding akiwa na umri wa miaka 5. Mpaka hivi leo, yule mtoto ameharibika huwezi dhania. Amekua na tabia za ajabu mpaka hata mimi zilinishangaza.

Watoto wanahitaji sana malezi ya karibu ambayo hawezi kuyapata akiwa boarding. Ni lazima akuwe na wazazi, au mlezi ambaye atamkuza kama mama/baba yake na sio mwalimu mwenye kuangalia watoto 50 kwa wakati mmoja!

2. Kuhusu Huyo Mwanamke
Nashukuru sana maana hukumwoa huyo msichana. Kwa kifupi huyo msichana hakufai, na anaonyesha hawezi kufikiria hata kidogo na asiye na uchungu na mwanae. "Mwanamke gani anaweza kusema mtoto apelekwe boarding kisa atakuwa busy?"

Huyo msichana ni mjinga na yote anayoongea ni upuuzi mtupu! Wewe kama mwanaume, chukua nafasi yako na ufanye maamuzi ya msingi. Huyo msicha inaovyoonesha maisha yake yameshaharibika, na ukifanya mchezo ataharibu ya kwako pia!

3. Kuhusu kulipa kodi
Ni jambo la busara kulipa matumizi ya mtoto, maana ukimwachia huyo mwanamke iko siku utasikia mwanao kafa njaa!

Lakini kuhusu kulipa pango lake la nyumba, hilo ni jambo la kipumbavu. "Mwanaume utalipaje chuma cha mwanamke asiye wako?" Ni sawa na kulipa hela ya Guest ili mwanamke wako akalale na mwanaume mwingine -- hiyo inaingia akilini?

4. Kuhusu kukuchukulia hatua za kisheria
Kwa kifupi, huyo mwanamke sio mkeo, bali ni mtu uliyezaa nae tu. Kama hakuna ndoa ya kanisa wala kiserikali hakuna anachoweza kukudai zaidi ya matumizi ya mtoto ambae ni wako.

Kwa kifupi, angalia utaratibu wa huyo mtoto, tena umwombee sana asije akarithi tabita za mama ake!
 
nimeishi na huyu mwanamke kwa mda wa miezi 11, na tayari nilikuwa nimezaa naye kabla ya hapo, mtoto wetu ana miaka mitatu sasa. kisa kilichotokea ni kwamba mwezi wa saba tulikuwa tunajadili kufunga ndoa ili tukae kihalali kwa maana ya misingi ya DINI.

lkn bahati mbaya au nzuri huyu mwenzangu alikuwa kaokoka. na akawa anadai kuwa kama nataka kumuoa basi tukafunge harusi kanisani kwao ambalo ni kanisa la kilokole. mimi nasali lutherani na yeye before alikuwa anasali lutherani pamoja na wazazi weu wote wanasali lutherani, ubishi ulienda mpaka ikafikia harusi kuahilishwa na ikabidi tutengane.

Hapa ndio ugomvi unapotokea yeye anasema kwa kuwa anahama basi mtoto wetu wa miaka mitatu tumpeleke shule ya bodding kwa sababu na yeye anafanya kazi hivyo itakuwa busy. nimekubaliana naye na gharama za kumpeleka mtoto shule ntatoa kwa aslimia 100.

Gharama za kumludisha mfanya kazi wetu wa ndani ambaye anatoka mbeya pamoja na kumlipa angalau ahsante ya kukaa naye pamoja ntaghalamia mimi kwa asilimia 100.

LKN pia anataka nimlipie kodi ya nyumba yake atakayo hamia yeye kama yeye sababu mtoto atakuwa tayari shule na anasema nisipo fanya hivyo anaenda kwenye sheria ili niweze kukidhi haja zake. kumbuka kuwa mshahara wangu na wake wa kwake ndio mkubwa. naomba ufafanuzi wa kisheria je ninapaswa kufanya haya yote kwa huyu mama tunaye achana, ambaye hata ndoa hatukufunga bado.

(I) Kufuatana na Sheria ya Ndoa (Law of Marriage Act, 1971) wewe hujaoana na huyu mama, na huna ulazima kisheria kumtunza yeye. Sheria hii inatambua ndoa aina tatu, (1) civil, yaani ya kiserikali, kama watu wanavyokwenda kwa area commissioner kufunga ndoa, (ii) ndoa inayofungwa kidini, kama vile kanisani au msikitini (iii) ndoa iliyofungwa kwa mila ya desturi - kitamaduni. Kufuatana na uliyosema hapa, wewe hukufanya yeyote haya matatu. (angalia kifungu 25 cha sheria ya ndoa, 1971)

(II) Umeishi na huyu mama kwa miezi 11 ambayo haitimii miezi 24 ambayo sheria inaashiria ndoa (yaani Presumption of marriage) katika kifungu 160 cha sheria ya ndoa. Kama mngekuwa mmeishi miaka 2 na kuendelea basi hata kama mlikuwa hamjafunga ndoa kufuatana na maelezo ya (I) hapa juu, sheria ingewatambua kama wanandoa. Na kama mngehitaji kutengana basi ingetakiwa kufuata taratibu za kuachana zilizo orodheshwa kisheria. Kwa hiyo kama anataka kwenda mahakamani atashindwa.

(III) Haimanishi basi kwamba huna majukumu yeyote kwa matunzo ya mtoto wako. Unasema wewe una kipato kikubwa kuliko mama wa mtoto wako, kwa hiyo kisheria unatakiwa kutoa matunzo. Sheria inayoitwa Affiliation Ordinance inampa hakimu uwezo wa kutoa summons kama ataridhishwa kwa wewe ni baba wa mtoto (Affiliation Ordinance Act, 1964, kifungu cha 4) kwa hiyo kama ukikataa kutoa matunzo ya mtoto wako, unaweza kufikishwa mahakamani na kulazimishwa kutoa matunzo ya mwanao.

Nadhani hii imekupa mwanga kidogo wa nini cha kufanya.
 
Mkuu kwa ufafanuzi tu zaidi hii ndoa ambayo inajihararisha kisheria kwa kukaa na mwananmek kwa muda wa meizi 24 katika matabaka ya ndoa itatambulikaje kati ya zile tatu kuu za mwanzo ambazo sheria imezielezea na kuzitambua kihalali?
 
Kaka pole sana, nakushauri ujipe moyo yote yawezekana. Hiyo gharama unayotaka kutoa kwa mtoto 100% toa na msimamo wa kutompleka mtoto wa miaka 3 boarding. Kama yeye ameamua kutokuolewa isiwe sababu ya kumuumiza mtoto mdogo kama huyo.

Kuna mambo mengine kama mwanaume unasema huna haja ya kujadili. Kuliko kumpeleka huyo mtoto boarding bora mmpeleke kwa bibi yake akampe mapenzi. Huyu dada hana huruma sijui wanawake tumekumbwwa na upepo gani usiopungika.

Pole.
 
na nyie msiwe mnaendeshwa kama magari ya dubai au ya japani ovyo eti kisa umelipia MV au insurance.

I wish to see that lady.Ni wa ajabu hata sijawahi kuona anajivunia nini kwa kumtreat mwenzie hivyo?

Anyway kwa kumlazimisha huyo bwanae amlipie kodi ya nyumba wakati hawapo pamoja na kulazimisha ndo ifungwe kwa kuzingatia ulokole kamwe haileti maana ila ninachodhani kuna kitu hakikusemwa na mleta mada kinachopelekea huo ugomvi.

Ni nini chanzo cha huyo dada kuokoka?

walikubaliana na mzazi mwenza?
Je wakati wanapanga masuala ya kufunga hiyo harusi alikuwa bado kuokoka au hakumshirikisha na uamuzi wa kuokoka?

Jamani tujaribu kuwa na moyo wa utu siku zingine kwa kuwa wote tu viumbe vya mungu huyohuyo./

Kwa nini tyuwapelekesha kwa starehe ya inayowapa raha wote wawili?
acheni kujishusha mtu unapata mshahara mkubwa kuliko mwananume halafu hutumii zako unataka kutoboa mfuko wa mwenzio maana yake nini.

Kikubwa amuweke chini amwambie kila kitu na madhara ya baadae kwa mtoto na wote kwa pamoja na kama mwanamke akipenda kumshitaki mimi nitakuwa wakili kwa upande wa huyo mwananume .

Kwa upande mwingine tumezidi kuwaonea hawa ndugu zetu ilhali ndo waliotoa ubavu wao ili tuwepo duniani.
shost you wil be suprised to hear, siwezi kumsemea huyu kaka kwamba kuna kitu anaficha inawezekana kweli au pia ikawa si kweli ndungu yangu. nimeona kwa macho mama kuna ndugu alianza kwenda kwa kakobe tangu alivyorudi siku ya kwanza alibadilika kitabia mpaka ukawa ugomvi na mumewe na ikaishia kutengana coz wote waislam sasa anamlazimisha mumewe awe mlokole imekaaje hiyo? mwenzangu hawa watu wakiiingia kwenye hiyo dini wanakuwa hawashikiki , balaaa lake si dogo.so wala simshangai huyu kaka zaidi nampa pole na bora waachane tu maana huyo keshakuwa obsessed na hazinduki leo.
 
(I) Kufuatana na Sheria ya Ndoa (Law of Marriage Act, 1971) wewe hujaoana na huyu mama, na huna ulazima kisheria kumtunza yeye. Sheria hii inatambua ndoa aina tatu, (1) civil, yaani ya kiserikali, kama watu wanavyokwenda kwa area commissioner kufunga ndoa, (ii) ndoa inayofungwa kidini, kama vile kanisani au msikitini (iii) ndoa iliyofungwa kwa mila ya desturi - kitamaduni. Kufuatana na uliyosema hapa, wewe hukufanya yeyote haya matatu. (angalia kifungu 25 cha sheria ya ndoa, 1971)

(II) Umeishi na huyu mama kwa miezi 11 ambayo haitimii miezi 24 ambayo sheria inaashiria ndoa (yaani Presumption of marriage) katika kifungu 160 cha sheria ya ndoa. Kama mngekuwa mmeishi miaka 2 na kuendelea basi hata kama mlikuwa hamjafunga ndoa kufuatana na maelezo ya (I) hapa juu, sheria ingewatambua kama wanandoa. Na kama mngehitaji kutengana basi ingetakiwa kufuata taratibu za kuachana zilizo orodheshwa kisheria. Kwa hiyo kama anataka kwenda mahakamani atashindwa.

(III) Haimanishi basi kwamba huna majukumu yeyote kwa matunzo ya mtoto wako. Unasema wewe una kipato kikubwa kuliko mama wa mtoto wako, kwa hiyo kisheria unatakiwa kutoa matunzo. Sheria inayoitwa Affiliation Ordinance inampa hakimu uwezo wa kutoa summons kama ataridhishwa kwa wewe ni baba wa mtoto (Affiliation Ordinance Act, 1964, kifungu cha 4) kwa hiyo kama ukikataa kutoa matunzo ya mtoto wako, unaweza kufikishwa mahakamani na kulazimishwa kutoa matunzo ya mwanao.

Nadhani hii imekupa mwanga kidogo wa nini cha kufanya.

Thanks mkuu umenipa mwanga wa kutosha
 
Back
Top Bottom