R Mbuna
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 2,283
- 5,359
Habari zenu wakuu,
Ni matumaini yangu wote tupo sawa na tunahangaika katika ujenzi wa taifa. Nisiwachoshe sana kwa salamu niende kwenye tatizo langu linalohitaji ushauri wenu wa kitaalamu.
Mke wangu tangu juzi alikuwa anahisi kizunguzungu na uchovu yaani muda wote alikuwa anahitaji awe amelala tu. Nikahisi labda huenda itakuwa mimba so tulipoenda kupima hakuwa na mimba ila tabibu akashauri apime pressure na sukari majibu yalipo kuja pressure ilikuwa inasoma 122/80 ambayo kwa mujibu wa tabibu wetu alisema ni ya kawaida na sukari ilisoma 20.7 pia alisema sukari ya kawaida inatakiwa iwe kumi kushika chini.
Naomba kujua je mke wangu atakuwa tayari amepata kisukari na jinsi gani naweza kumsaidia ili iweze kuwa katika kiwango kinachotakiwa.
Naombeni msaada wenu ndugu zangu