Msaada wa kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kisheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by GRACE KIRUNDWA, Jul 14, 2010.

 1. G

  GRACE KIRUNDWA New Member

  #1
  Jul 14, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari wana jf,

  kuna rafiki yangu ameomba nimuulizie ili swali.

  1. Yeye ameolewa kwa ndoa ya bomani mume wake ni mwiisilam, wana watoto wawili. Tangu waishi na mumewe takribani miaka mitatu, yeye ndiye anatunza familia kwanzia chakula mpaka ada za shule, watoto wako nursery.
  mume wake hafanyi kazi, ila ananyumba ambayo anapokea kodi kila baada ya mwaka 5,000,000 akipokea tuu anasafiri mpaka zikiisha ndipo anarudi.
  na akirudi anakuwa hana hata mia moja kwa hiyo anakuwa anamtegemea yeye kwa kila kitu.

  sasa huyu dada alikuwa anaomba msaada wa kisheria maana awezi kuondoka na watoto wawili akapange chumba wakati bado watoto wanamtegemea ada na chakula.

  nyumba wanayo kaa ni ya huyo mwanamume

  asanteni, nitashukuru kama mtanijibu
   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  HUyo Rafikiyo anachotaka nini?. Kutengana, Talaka au Matunzo kwa familia?

  vinginevyo:

  1. Ndoa ya Bomani ni ndoa kama zilivyo nyingine, inatambulika kisheria iwapo ilifuata michakato yote ya kuihalalisha. Hata kama wasingekuwa na ndoa bado kuna haki na wajibu ambao unawahusu wawili hao kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ikiwemo malezi na matunzo ya watoto.
  2. Mke au Mume hawezi kuondoka katika nyumba ya ndoa kwa staili yeyote ile iwe ya kuhamia nyumba ndogo au kwenda kupanda sehemu nyingine labda kama hiyo ndoa imesambaratika au mahusinao yamesitishwa kwa maana ya kuwepo kwa amri halali ya mahakama ya kuwatenganisha au kuwaachanisha kwa talaka (separation or divorce). Kwa maana nyingine, kutoka katika nyumba ya ndoa ni kosa chini ya sheria ya ndoa na hilo linaweza kumpotezea huyo Mke haki zake iwapo baadae atadai kuwa alaimua kwenda kupanga kwa kuwa mumewe hakuwa anatoa matumizi.
  3. Kanuni ya jumla kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ni kuwa Mume ndie mwenye wajibu wa Kutunza Mke na watoto isipokuwa kama itabainika kuwa hana uwezo katika hali moja au nyingine ikiwemo kutokuwa na kazi. Hata hivyo, kumbuka pia kuwa kutokuwa na kazi sio kigezo cha Mume kukwepa jukumu la kutunza familia kwani hilo jukumu linalazimisha mwanaume kuhangaika kwa jinsi yeyote ile ili kupata chochote cha kuweza kuifanya familia iweze kuishi.
  4. Ikiwa Mume anapopata kipato anatoweka nyumbani, hali hiyo ni sawa na kuitelekeza familia. Panapo ushahidi wa kutosha inaweza kuwa ni kigezo cha mke kuomba kutengana hata talaka sambamba na hilo la kutoijali familia (kutotoa matunzo).
  5. Ikiwa suala ni matunzo tu, utaratibu uliomwepesi ni kuwelekeza huyo rafiki awasilishe madai yake kwanza kwa wazee wa familia ya huyo mume (kama hajafanya hivyo), ikishindikana aende Ustawi wa Jamii eneo la karibu na walipo wao watamsaidia zaidi jinsi ya kumbana huyo jamaa awajibike kwa familia yake na pia huko watamwelekeza hatua nyingine za kumchukulia ikiwa atazidi kupuuzia ikiwemo jinsi ya kuwasilisha madai kwenye vyombo vya sheria (Mahakamani) pale itakapobidi.
   
Loading...