Asante.
Sikutaka kumpeleka huko kwenye kufungua kesi ya msingi (land application), zuio la muda (temporary injunction) na kuomba isikilizwe kwa haraka kwa kuweka hati ya dharura (certificate of urgency), kwasababu hizo ni hatua za mbele sana.
Yeye alitaka cha kufanya sasa kwasababu jamaa ameanza kuvuna miti.
Kwa sasa polisi wanaweza kumsaidia kwa kutumia nakala ya hukumu. Hapa itatumika busara na siyo Sheria, kwasababu so far, hata hao polisi hawamjui mmiliki halali.
Vinginevyo afanye kama nilivyoshauri mwishoni kwamba amuache aendelee kuvuna wakati huo afungue shauri la msingi, akishinda adai fidia.