Msaada wa kisheria

Butiyangu

Senior Member
May 19, 2018
107
250
Kuna rafiki yangu tunaishi nae Kibamba, ni mfanya biashara wa kununua mashamba na kuuza. Hivi karibuni aliingia kwy matatizo baada ya kununua eneo akaamua kulikatakata viwanja, aliuza viwanja kwa wateja Kama watatu hivi, ndipo ilipokuja kubainika eneo Hilo kuwa Lina mgogoro wa kifamilia, ili bidi aanze kuwabadilishia wateja wake viwanja vingine,wateja wawili walikubali kubadilisha viwanja lakini mteja mmoja alikataa kabisa alihitaji pesa zake tu, mauziano ya kiwanja yalikuwa ni milioni mbili na laki moja. Rafiki yangu alikubali kurejesha pesa hizo, alilipa awamu ya kwa tshs 1,900,00/= zikabaki laki 2 ambazo zilitakiwa kulipwa tangu tarehe 31 mwezi wa nane 2020. Cha kushangaza zaidi mteja alikuja na magari mawili ya Police wakiwa na silaha za kivita huku wamefunika nyuso zao, akidai kuwa wametumwa kuja kumkamata huyo rafiki yangu kwa sababu ameshindwa kutimiza ahadi ya hiyo pesa. Mimi nikawaambia hiyo laki mbili mm nitawapatia Sasa hivi kwa sababu rafiki yangu hayupo amesafiri. Yule mteja alinijibu kuwa yeye anadai Tshs 1,100,000/= sio laki mbili, mm nikamuulia aonyeshe mkataba wake wa mauziano, alipouonyesha ulikuwa umeandikwa eneo alinunua kwa Tshs 2,100,000/=. Baada ya majadiliano kushindikana Mimi niliamua kuondoka, na wao waliondoka. Sasa Cha ajabu ni kwamba usiku walirudi tena nyumbani kwa rafiki yangu, wakaamua kumchukua mke wa rafiki yangu wakidai kuwa hadi walipwe pesa ndipo wamrejeshe. Sasa tumefuatilia huko central police walikodai wanampeleka, tukakuta maelezo kuwa pale walimleta kweli lkn mhusika(mdai) aliamua kumchukua na kumpeleka kwake. Mhusika nae inasemekana ni Police. Sasa happy katika swala la kisheria hili Jambo limekaaje? Je? Sheria zinaruhusu kumkamata mke wa mdaiwa? Naombeni msaada katika hili Jambo.
 

mwanateknolojia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
342
500
Kwanza kabisa wahi polis utowe taarifa ya shemeji yako kutoonekana nyumbani maana hakuna sheria inayoruhusu mtu kumuweka mtuhumiwa mahabusu ya nyumbani kwake hata kama anamdai kitu gani, huo ni utekaji!
Pia fanya jitihada jamaa yako arudi fasta maana ndiye anayo mikataba ya mauziano pamoja na yale makabidhiano yao ya awali ya Tshs 1,900,000 ambayo bila shaka yataeleza kiasi halisi cha salio la deni lililobakia! Huyo bwana tayari ni mtata sasa , Dawa ya watu vigeugeu ni kuongea huku ukiwa na Documents.
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
4,035
2,000
Kwanza kabisa wahi polis utowe taarifa ya shemeji yako kutoonekana nyumbani maana hakuna sheria inayoruhusu mtu kumuweka mtuhumiwa mahabusu ya nyumbani kwake hata kama anamdai kitu gani, huo ni utekaji!
Pia fanya jitihada jamaa yako arudi fasta maana ndiye anayo mikataba ya mauziano pamoja na yale makabidhiano yao ya awali ya Tshs 1,900,000 ambayo bila shaka yataeleza kiasi halisi cha salio la deni lililobakia! Huyo bwana tayari ni mtata sasa , Dawa ya watu vigeugeu ni kuongea huku ukiwa na Documents.
Ni kweli mkuu,hicho kipolisi kimekiuka maadili ya kazi.
Hajui kwamba hapo kesi itageuka na kuambiwa mtekaji au mbakaji.
Hapo ni kutafuta pesa za wakili tu wamuonyeshe adabu na upolisi wake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom