Msaada wa kisheria

Q

qoda

Member
Joined
May 19, 2019
Messages
6
Points
45
Q

qoda

Member
Joined May 19, 2019
6 45
BACKGROUND.
(HISTORIA YA BABU YANGU {X} MJOMBA WA BABU {Y} NA BABA YANGU {Z})

Babu yangu {X} alikuwa na nyumba mbili, moja upande wa Singida( Mkalama) na nyingine upande wa Manyara. Makao hasa (base) yalikuwa upande wa Singida ambako alikaa mke wa kwanza.

Kutokana na kujishughulisha na ufugaji alihamisha mifugo upande wa Manyara kutafuta malisho mazuri ya mifugo. Alichukua eneo la ekari zaidi ya 100 na kujenga nyumba nyingine alikokaa mke wake wa pili, huko Manyara babu alikuwa na wafugaji wengeni wenye maeneo yao na mmoja wapo alikuwa ni mjomba wake babu {Y} ambaye alipakana maeneo.

Miaka ya 1988/89 (late 80s) babu alifiwa na mke wake wa kwanza. Wakati taratibu za mazishi zilipo kamilika na marehemu kuzikwa, babu alimtoa mke wa pili upande wa Manyara ili akae alipokuwa akikaa marehemu mke wa kwanza (ambayo ndio base ya familia).

Upande wa Manyara ikabaki mifugo ambayo nayo ikahamishwa pande za Manyoni mwaka 1991 kutokana na kuongezeka kwa idadi ya mifugo na kupungua maeneo ya malisho,kutokana na tukio la msiba, babu aliliacha eneo lote chini ya uangalizi/(trustee) wa mjomba wake{Y}, kwani asingeweza kuyatembelea maeneo yote yaani mifugo iliyohamia Manyoni, nyumba iliyopo Manyara na base ya Singida kwa sababu za umri kumtupa mkono.

Lakini hakutaka kuliuza kwani alitaka kulirudia baadaye mambo yangekaa vyema na pia ana watoto ambapo mmoja wa watoto angeweza kurudi katika eneo hilo.Mwaka 1994 babu yangu alimpendekeza baba yangu{Z} kurudi katika eneo la upande wa Manyara ambalo kwa wakati huo lipo chini ya uangalizi wa mjomba wake babu.

Baba yangu{Z } alikaribishwa na binamu yake (yaani mjomba wake babu {Y}) na kupewa shamba la ekari 4 kwa ajili ya kilimo, ambayo ilimtosha kwa kipindi hicho. Baba hakuanza harakati za kudhibiti eneo lote kwa kuwa ndio alianza maisha.

Mwaka ya 2000 babu yangu {X} alifariki dunia wakati akitembelea mifugo maeneo ya Manyoni. Wakati anafariki watoto wake hawakuwa pamoja, wengi wao walikuwa nyumba lililopo Singida, baba yangu alikuwa upande wa Manyara na mwingine alikuwa na mifugo Manyoni ambako ndipo alipofariki babu. Taratibu za mazishi zilifanyika na babu akazikwa. Hakuandika wosia/mirathi.

Mwaka 2002 mjomba wake babu {Y} alianza kufyeka eneo ambalo lipo karibu na shamba la baba kwa ajili ya kupanua shamba. Eneo hilo baba aliliacha kwa ajili ya malisho mathalani eneo la kutokea mifugo. Hapo ndipo baba alipogundua ukorofi wa binamu yake (mjomba wake babu).

Katika kutafuta suluhu kikao cha wazee wa majirani walikaa ili kuwapatanisha. Katika kikao hicho ndipo baba alipo sikia kitu ambacho hakuamini hadi leo. Mjomba wake babu alisema kwamba alimdai dume babu, hivyo babu alikwisha muuzia eneo lote kutokana na deni hilo la dume.

Na kwa taarifa baba yangu{Z} yupo pale kwa hisani yake tu, na kwamba anatakiwa awe anamuomba shamba, eneo la malisho na kuvuna kuni n.k. na kama hataki kufanya hivo ahame tu.

Hadi sasa baba yangu{Z} ana eneo la ekari kama 6 analolima, kati ya eneo la ekari zaidi ya 100 la marehemu babu yangu {X}. Baba alifanya jitihada za kukomboa eneo hilo kwa kupitia vikao vya wazee wa ukoo. Kutokana na ugumu wa maisha na hali mbaya ya uchumi, hakufanikiwa kwani wazee wa ukoo nao wamesambaa sehemu mbalimbli za mkoa wa Singida na Manyara. Walikaa mara moja na hawakufikia mwafaka.

Baba hakuwahi kulipeleka shauri hili mahakamani kutokana na hali duni ya uchumi, hofu ya gharama za kuendesha kesi, na uwezekano mdogo wa kushinda (narrow margin) kutokana na imani kwamba mjomba wake babu anaweza nunua haki mahakamani kwa njia za rushwa kwani kiuchumi yupo vizuri.

Mimi ni mjukuu wa babu{X} na kwa sasa nina miaka 27 . Karibu maisha yangu yote nishuhudia kero za huyu mtu. Ningependa hizi kero na dhuluma zifike mwisho kwa kuchukua hatua za kisheria ili niwasaidie wazazi wangu.
Naomba msaada wa kisheria wapi pakuanzia? Je hii ni aina gani ya kesi, jinai au madai?, Je ni sheria gani za kutumia katika scenario kama hii? Na pia msaada wa kumpata wakili aliyebobea ktk kutatua migogoro ya ardhi.

Majirani walioishi na babu miaka ya 70s na 80s, baadhi maeneo yao yalipakana na eneo la babu wanafahamu eneo hilo. Lakini wanasita kutoa ushirikiano kutokana na uwezekano wa kushindwa katika kesi za Mahakamani na dhana ya kutoshindwa kwa mwenye nacho, na asiye nacho hunyanganywa hata kidogo alicho nacho.

Pia wana hofu ya kuwa upande wowote kwa dhana ya kuvunjika kwa mahusiano ya baadaye kwa kujihusisha na mgogoro usio wahusu.Hili limekuwa moja ya hofu yangu katika nia yangu ya kulipeleka kesi hii mahakamani. Je ni mbinu ipi nitumie hawa majirani kunipa ushirikiano pengini suala la mashahidi litakapohitajika mahakamani?.
Naomba kuwasilisha......
 
S

softG

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2016
Messages
1,284
Points
2,000
S

softG

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2016
1,284 2,000
Mjomba wa Babu ni Binamu yako? Au hii elimu yangu ya MEMKWA ndo inanichanganya?
 
A

alongakeke

Senior Member
Joined
Feb 3, 2017
Messages
101
Points
225
A

alongakeke

Senior Member
Joined Feb 3, 2017
101 225

Wasiliana na Fulgent legal consultants kwa namba 0769 524 022, utaunganishwa kwa wataalam wa masuala ya sheria ,utahudumiwa kwa gharama nafuu sana.
 
B

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Messages
4,852
Points
2,000
B

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2013
4,852 2,000
1) Kuna hati ya mauziano ya eneo hilo alioacha Babu?

2) Kuna maandishi ya babu ama ushahidi wa kumuachia eneo mjomba wake ili aliangalie?

3) Babu alikuwa na utaratibu wa kulitembelea eneo hilo mara kwa mara baada ya kuliacha kwa uangalizi wa mjomba?

4) Nani anatambulika na serikali ya kijiji kama mmiliki halali wa eneo?

Kama majibu yote yako vizuri, Baba afungue mirathi kwanza na kisha ashughulikie kulitwaa eneo hilo japo mjomba anaweza kudai malipo ya uangalizi.

Kesi ipelekwe baraza la ardhi kuanzia Kata husika.

Akigoma na kutumia pesa, akatiwe rufaa huko mbele pia nadhani mnaweza kumpiga shitaka la Trespass Kutegemeana na ukaidi wake.

Hili ni fundisho pia, Watu tuwe na tabia ya kuandika wosia. Wosia sio kifo bali ni tahadhari
 
Mkuu nashukuru sana kwa kunisaidia pakuanzia.
Hakuna hati yoyote ya mauziano ya eneo wala maandishi ila kuna mashahidi.
Nashukuru kwa mchango wa mawazo.
 
sagaciR

sagaciR

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2017
Messages
630
Points
1,000
sagaciR

sagaciR

JF-Expert Member
Joined Jun 17, 2017
630 1,000
1) Kuna hati ya mauziano ya eneo hilo alioacha Babu?

2) Kuna maandishi ya babu ama ushahidi wa kumuachia eneo mjomba wake ili aliangalie?

3) Babu alikuwa na utaratibu wa kulitembelea eneo hilo mara kwa mara baada ya kuliacha kwa uangalizi wa mjomba?

4) Nani anatambulika na serikali ya kijiji kama mmiliki halali wa eneo?

Kama majibu yote yako vizuri, Baba afungue mirathi kwanza na kisha ashughulikie kulitwaa eneo hilo japo mjomba anaweza kudai malipo ya uangalizi.

Kesi ipelekwe baraza la ardhi kuanzia Kata husika.

Akigoma na kutumia pesa, akatiwe rufaa huko mbele pia nadhani mnaweza kumpiga shitaka la Trespass Kutegemeana na ukaidi wake.

Hili ni fundisho pia, Watu tuwe na tabia ya kuandika wosia. Wosia sio kifo bali ni tahadhari
Ekari zaidi ya100 aende kata mkuu??. Assume ekari 1 ni sh 100,000/= tu zipo zaid ya 100 (100 x 100,000 =10,000,000/=) it means >3,000,000/=.

Aanzie DLHT
 
Q

qoda

Member
Joined
May 19, 2019
Messages
6
Points
45
Q

qoda

Member
Joined May 19, 2019
6 45
Ekari zaidi ya100 aende kata mkuu??. Assume ekari 1 ni sh 100,000/= tu zipo zaid ya 100 (100 x 100,000 =10,000,000/=) it means >3,000,000/=.

Aanzie DLHT
Mkuu nimepitia baadhi ya nyuzi zako humu, you seem to be an expert in this field. Michango yako inanitia moyo hasa ktk suala langu hili. Mkuu ubarikiwe kwa moyo huo wa kushare uliyojaliwa kuyafahamu.
 
Forum statistics

Threads 1,336,567
Members 512,648
Posts 32,543,498
Top