Msaada wa kisheria

Ndera

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
653
548
Wadau mnisaidie, kuna ndugu yangu alikuwa na kesi kazini kwake lakini kabla ya kutatuliwa katika kikao cha nidhamu mdau alikuwa anajiskia kuugua hata akashindwa kuhudhuria tarehe zilizopangwa katika kikao, alihudhuria hospitali nakupewa ED 8 kwa mda tofauti (ED,3,3,2) baada ya hapo kikao kilifanyika lakini ofisi ikaomba Ripoti ya daktari kwa kutuma email hospitali husika ambayo ndo ina mkataba na kampuni hiyo ili kudhibitisha hali yake kama amepona na anaweza kuendelea na kazi ya kabla ya kupangiwa majukumu. Alipofika hospitali alipangiwa kumuona specialist ambaye alimfanyia check up na kuendelea na matibabu upya na daktari akasema hawezi kuandika ripoti mpaka atakapo jua hali yake.

swali langu, nimekuwa nikijulisha kuhusu utaratibu unaoendelea hospitali lakini naona kama pia sio suala langu sana kujulisha ofisi yake kwa sababu wao wenyewe waliitaji ripoti tena kwa njia ya email kwa hiyo wanaitaji kumsubiri Dkt hadi atakapotoa taarifa yake. Sasa Je, anapoendelea kuwa nyumbani mpaka hapo atakapo pata ripoti ni sahihi? au ataonekana mtoro? au aendelee kuripoti ofisini japo anaendelea na matibabu huku akisubiria hiyo ripoti?
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini(labour law) sheria namba 06 ya mwaka 2004 ni wajibu wa mgonjwa au ndugu/mtu wa karibu wa mfanyakazi ambaye ni mgonjwa kutoa taarifa za kutokuhudhuria kazini kwa mfanyakazi kwa sababu ya ugonjwa,haijalishi wakati unatoa taarifa lazima uwe na ripoti ya hospitali kama daktari bado hajathibitisha nini hasa tatizo lake,ispokuwa baadaye ndipo mfanyakazi huyo atalazimika kupeleka vyeti vya hospitali au kituo cha matibabu kuthibitisha kuwa alikuwa mgonjwa na akapata tiba.Na mgonjwa huyo halazimishwi kwa mujibu wa sheria za kazi kwenda kazini akiwa mgonjwa na wala hatokuwa mtoro kisheria kwa kuwa sheria imeweka wazi kuhusiana na haki za mfanyakazi ikiwemo haki ya likizo ya ugonjwa(sick leave) rejea kifungu cha 32 cha Sheria ya Ajira Na Uhusiano Kazini
 
Kwa hiyo wewe unatakiwa kupeleka taarifa ya ndugu yako kazini kwake vinginevyo ataonekana mtoro kazini. Ila pia lazima ufahamu kwamba likizo ya ugonjwa ina ukomo. Ukomo ukifika basi atafutwa kazi.
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini(labour law) sheria namba 06 ya mwaka 2004 ni wajibu wa mgonjwa au ndugu/mtu wa karibu wa mfanyakazi ambaye ni mgonjwa kutoa taarifa za kutokuhudhuria kazini kwa mfanyakazi kwa sababu ya ugonjwa,haijalishi wakati unatoa taarifa lazima uwe na ripoti ya hospitali kama daktari bado hajathibitisha nini hasa tatizo lake,ispokuwa baadaye ndipo mfanyakazi huyo atalazimika kupeleka vyeti vya hospitali au kituo cha matibabu kuthibitisha kuwa alikuwa mgonjwa na akapata tiba.Na mgonjwa huyo halazimishwi kwa mujibu wa sheria za kazi kwenda kazini akiwa mgonjwa na wala hatokuwa mtoro kisheria kwa kuwa sheria imeweka wazi kuhusiana na haki za mfanyakazi ikiwemo haki ya likizo ya ugonjwa(sick leave) rejea kifungu cha 32 cha Sheria ya Ajira Na Uhusiano Kazini

Asante sana kwa ufafanuzi wa sharia kaka.
 
Back
Top Bottom