Msaada wa kisheria unahitajika wadau

IT PROFESSIONAL

JF-Expert Member
Mar 17, 2016
228
95
Kuna jamaa yangu alikamatwa kwa kesi ya kuhisiwa kavunja kaunta ya Bar ,baada ya kumkamata wakampiga na kumpeleka kituo cha polisi, wakachukuliwa Maelezo na mtuhumiwa kawekwa ndani kwa siku 4,baada ya Mimi kupata taarifa nikaenda kumwekea dhamana ambapo kwenye Maelezo ya mshitaki imeelezwa kiasi kilichoibwa yasadikiwa kama 1,200,000 ambacho kilichuuliwa kwa awamu tofauti tofauti ,

Jamaa yangu alikuwa anafanya kazi kama mlinzi aliyeajiriwa kwenye Kampuni mojawapo ya ulinzi hivi kwa siku hiyo alikua lindo hapo walipomkamata na kuhisiwa kwamba kavunja kaunta.Kwa sasa kesi ipo mahakamani bado haijasikilizwa .Je mimi kama mdhamini ni nini wajibu wangu na kisheria hili kesi imekaaje ,

Naombeni ushauri kwa hili
 
Naandikia hukumu kesi kama hyo ya walinzi wawili wakiwa lindoni wezi wakavamia na kuiba.inshrt ww kama mdhamini unapaswa kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani kila siku ya mahakama bila kukosa maana tatz litakua kwako.Na sidhani km kuna kesi hapo labda km prosecution ina ushahidi wa nguvu
 
Back
Top Bottom