Msaada wa kisheria toka kwenu wadau kuhusu ununuzi mpaka usajili wa gari yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kisheria toka kwenu wadau kuhusu ununuzi mpaka usajili wa gari yangu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pa1, Oct 21, 2012.

 1. P

  Pa1 New Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2009 nilinunua gari yangu aina ya Toyota kupitia rafiki yangu ambaye ni mfanyabiashara wa kuagiza magari yaliyotumika toka japani.
  Huyu rafiki yangu pia ni mwanasheria, tuliandikishana kimaandishi namna ya kulipana na mashariti yote nilifuata na gari likafika nchini mwaka huo, 2009. Mashariti ilikuwa mimi kumlipa hela yote katika awamu mbili, nusu ya hela wakati wa kuagiza na nusu mara niletewapo gari ikiwa imeshasajiliwa kwa maelezo yangu husika.

  Nimetumia gari hili bila matatizo yoyote, ilipofika November, 2011 wakati naenda kurenew leseni ya barabarani, nikaambiwa gari langu limekuwa blocked, kwakuwa lina matatizo ya usajili, nilipofuatilia TRA nikaambiwa halikulipiwa ushuru, hivyo linakamatwa na pia nahitajika kulipa na faini( Lakini TRA wakimfahamu fika Agent huyu aliyeingiza gari yangu pia kukiuka ulipaji wa kodi). Mtu aliyefanya hivi amabaye ni huyo rafiki yangu, nilimjulisha na amekuwa ananiahidi bila utekelezaji kuhakikisha anafuatilia gari langu ili niweze kulitumia, huu ni mwaka sasa hapokei wala kujibu mawasiliano yangu ya simu. Naomba USHAURI WENU Je, ni hatua zipi za kisheria naweza kumchukulia mtu huyu na haki itendeke.... maana nashindwa kuanzia ngazi hizi za mwanzo kwa kuwa najuafika huyu jamaa anakuwa na influence ya kupindisha ukweli wa mambo, naomba msaada jamani !!
   
Loading...