Msaada wa kisheria: Mume anataka kuuza Mali za familia pasipokushirikisha familia yake na familia haijaafiki

Marshall plan

JF-Expert Member
Nov 3, 2019
644
980
Wakuu salaam kwenu!

Naomba kujua Sheria inasemaje ikiwa Mme katika familia anataka kuuza Mali za familia pasipokushirikisha familia yake na familia haijaafiki uuzwaji wa Mali hizo!

Tatizo lipo hivi Baba wa familia anataka kuhama eneo wanapoishi na kuhamia eneo jingine,ila tatizo linakuja katika mchakato wa uuzwaji wa Mali hizo kwani Baba wa familia hajaishirikisha familia zaidi ya kuwapa taarifa ya kuuza hizo Mali, Mama wa familia hataki kuuzwa kwa mali hizo kwasababu hajashirikishwa ipasavyo.

Kibaya zaidi inasemekana sahihi za uuzwaji wa Mali hizo zimewekwa na mtoto ambaye yupo nje ya familia ya mama wa familia kwa maaana ya "nje ya ndoa". Wataalam wa sheria mnamsaidiaje huyu mama na familia yake!

Karibu kwa msaada mama aanzie wapi kupata
 
Mali za familia haziuzwi mpaka kuwe na free consent kwa wanafamilia, yani makubaliano ya hiari kwa wanafamilia kuwa mnataka kuuza mali fulani, hakuna mwenye mamlaka peke kufanya hivyo nje ya utaratibu huo, nje ya hapo ni kosa kisheria, pingamizi Mahakamani unapeleka vielelezo na utapata msaada
 
Mali za familia haziuzwi mpaka kuwe na free consent kwa wanafamilia, yani makubaliano ya hiari kwa wanafamilia kuwa mnataka kuuza mali fulani, hakuna mwenye mamlaka peke kufanya hivyo nje ya utaratibu huo, nje ya hapo ni kosa kisheria, pingamizi mahakani unapeleka vielelezo na utapata msaada
Asante!!
 
Kama nyumba ni ya mke na mume kwenye sales of agreement lazima mke wake atoe consent kwa kusign nnje ya hapo ni void
 
Asante sana Mkuu!! Na kama tiali ameshapokea pesa??
Hata kama ameshapokea pesa mnunuaji hakuna aliekua juu ya muhimili wa mahakama, mahakama ikisema hivi basi huwa ni amri na sio ombi, kitakachofanyika copy ya zuio moja atapelekewa alienunua na ingine alieuza na moja mtabaki nayo mliotoa malalamiko then taratibu ya kuinusuru mali mahakama itaanza kuchukua
 
Hata kama ameshapokea pesa mnunuaji hakuna aliekua juu ya muhimili wa mahakama, mahakama ikisema hivi basi huwa ni amri na sio ombi, kitakachofanyika copy ya zuio moja atapelekewa alienunua na ingine alieuza na moja mtabaki nayo mliotoa malalamiko then taratibu ya kuinusuru mali mahakama itaanza kuchukua
Vipi kama mume alishapokea pesa a mkewe wa nje ya ndoa alisaini mkataba wa mauziano, na sasa mume alishafariki?
 
Vipi kama mume alishapokea pesa a mkewe wa nje ya ndoa alisaini mkataba wa mauziano, na sasa mume alishafariki?
Ndugu mali ya familia ni mali iliyochumwa kwa pamoja baina ya mume na mke wa halali. Kimada/hawara huwa sio mke na kwa case za mali za ndoa basi huwa hana haki.

Mauzo ya mali ya familia (matrimonial property) yaliyofanyika pasipo ruhusa (consent) ya mwenza basi mauzo hayo huwa ni batili hadi pale mwenza atakapothibitisha, mbali na hapo huo ni utapeli mbele ya macho ya sheria na ujue huo mkataba ni haramu tangu ulipoingiwa.
 
Back
Top Bottom