Nahitaji Msaada wa kisheria

Moi aussi

New Member
Mar 16, 2024
3
2
Kuna jambo linaniumiza Kichwa sana.

Baba yangu alikufa 2014, babu yangu(baba wa baba yangu) akafa 2021.

Inasadikika muuaji ni mwanafamilia mshirikina; lkn hapa nataka kuleta hoja nisaidike.

Babu aliacha mali nyingi, mshukiwa amejichukulia mamlaka ya kujigawia mali za babu na kumpa yeyote anayemtaka sehem ya mali hizo.

Mimi nilipojaribu kuhoji niliambiwa nikae pembeni maana hiyo si familia yangu. Je, kwa kuwa baba yangu ni miongoni mwa wanufaika wa mali za baba yake, naweza kwenda mahakaman kumfungulia mashtaka baba mdogo?

Hakuna hata mmoja kati ya ndugu zake anayethubutu kumzungumzia kutokana na hofu waliyonayo, anaogopwa sana kwa ushirikina!
 
Aisee pole!

Kwani aliyeteuliwa na Ukoo/Familia au Mahakama kusimamia suala la mirathi ya Babu yenu alikuwa ni Nani?
 
Alie pewa usimamizi wa mali za baba ako ndo aka fungue shauri la kuomba mali za baba ake na baba ako sijui ata kama ume elewa
 
Mkuu wewe huwezi kufanya hivyo kisheria
Msaidie baba yako afungue malalamiko dhidi ya msimamizi wa mirathi
Na kama waligawana kienyeji basi likafunguliwe shauri rasmi la mirathi ili ateuliwe msimamizi atakaye simamia kugawa mali

Kisheria Mjukuu harithi mali iwapo watoto wa marehemu yupo
 
Kuna jambo linaniumiza Kichwa sana.

Baba yangu alikufa 2014, babu yangu(baba wa baba yangu) akafa 2021.

Inasadikika muuaji ni mwanafamilia mshirikina; lkn hapa nataka kuleta hoja nisaidike.

Babu aliacha mali nyingi, mshukiwa amejichukulia mamlaka ya kujigawia mali za babu na kumpa yeyote anayemtaka sehem ya mali hizo.

Mimi nilipojaribu kuhoji niliambiwa nikae pembeni maana hiyo si familia yangu. Je, kwa kuwa baba yangu ni miongoni mwa wanufaika wa mali za baba yake, naweza kwenda mahakaman kumfungulia mashtaka baba mdogo?

Hakuna hata mmoja kati ya ndugu zake anayethubutu kumzungumzia kutokana na hofu waliyonayo, anaogopwa sana kwa ushirikina!
Aisee kwanza pole ndugu yangu, mimi nitajaribu kukujibu kwa kadri ninavyoelewa.

Kwanza kwa situation yako inategemea kama babu kaacha wosia au lah, na kama hajaacha wasia familia mnataka mirathi hiyo igawanywe kwakufata sheria gani, either kidini (uislamu ama ukristo), ama kitamaduni kulingana na life style ya babu. Ni muhimu kujua vitu hivyo kwanza kwani kwa sheria zetu namna ya ugawaji wa mirathi kwa waislamu ni tofauti na kwa wakristo na ni tofauti kwa kukutumia njia ya utamaduni (customary law).

Nitaelezea kwa ufupi;
Katika uislamu: kwenye Qur'an, masuala ya urithi yamefafanuliwa kwa kina katika Surah An-Nisa. Kwa mujibu wa aya iyo, wajukuu hawarithi moja kwa moja kutoka kwa babu zao isipokuwa kupitia wasia tu, ambao hauzidi theluthi moja ya urithi. Hata hivyo, aya za 4:11-14 katika Surah An-Nisa zinaelezea mgawanyo wa urithi kwa watoto, wazazi, na ndugu (including wajukuu).


Tukija kwa Wakristo wao mirathi yao hutumia sheria za mirathi za India/ India Succession Act (ISA), kutokana na ISA, wao wanauhuru wa kuandika wosia na kueleza jinsi anavyotaka mali yake igawanywe vile wapendavyo wao, ikiwa ni pamoja na kuwapa wajukuu (See: Kifungu cha 46 cha sheria ya urithi ya India, 1925). Ikiwa hakuna wosia, bado wajukuu wanaweza kupewa sehemu ikiwa wazazi wao wamefariki kabla ya babu yao 'kama ilivyo kwenye scenario yako'(See: kifungu cha 33 cha sheria ya urithi ya India).

Lakini kwa upande wa utamaduni huku haki za wajukuu kurithi zinaweza kutofautiana sana kutoka kabila moja hadi lingine. Katika baadhi ya jamii, wajukuu wanaweza kurithi sehemu ya mali ikiwa wazazi wao wamefariki. Katika jamii nyingine, urithi unaweza kuendelea ndani ya familia ya kiume na wajukuu wa kike wanaweza kutopewa urithi wowote

Kwa hivyo, ni vizuri kuelewa kuwa haki za urithi zinaweza kuathiriwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na uwepo wa wosia, sheria inayotumika kugawa urithi, na hali maalum ya familia.

Now, connecting with your scenario. Kujua ni sheria gani za urithi mnazitumia kugawa mirathi ya babu kutakusaidia kujua kama una haki ya kurithi mirathi hiyo ama vinginevyo.

Ikiwa hauna haki ya kurithi basi hata haki ya kwenda mahakamani kulalamika(locus standi) unakua huna. Lakini ikiwa haki ya kurithi unayo basi kwanza unatakiwa kujua kama tayari kuna msimamizi aliyeteuliwa na mahakama (SIO FAMILIA) kuwa ndiye msimamizi wa mirathi ya babu, kama hayupo basi unaruhusiwa kwenda mahakamani kuomba barua ya usimamizi wa mirathi. Ila hakikisha unaenda mahakama yenye mamlaka ya kudeal na hiyo mirathi (kwasababu mamlaka za mahakama kwenye mirathi zinatofautiana kutokana na sheria ya urithi inayotumika 'kama nilivyoeleza hapo juu' au thamani ya mirathi either kubwa '100M kuendelea' ama ndogo 'chini ya 100M'), anyway hili tutalizungumzia wakati mwingine.

Lakini ikiwa tayari uyo baba mdogo ama mtu mwingine yeyote tayari ameomba au amechaguliwa kuwa msimamizi wa mirathi basi hapo utatakiwa kufanya zuio (caveat or objection, as case maybe) kama ndo ameomba usimamamizi, na utatakiwa kufanya maombi ya kubatilisha mamalaka yake kama msimamizi wa mirathi (Revocation) kama ikiwa tayari ameshachaguliwa na mahakama kuwa msimamizi wa mirathi. NB: ili uweze kufanya haya yote unatakiwa uwe na sababu maalumu na si sababu yoyote tu ilimradi.

Nimejaribu kutoa general overview tu ili iwe faida na kwa wengi. Naomba kuwasilisha​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom