whitehorse
JF-Expert Member
- Aug 29, 2009
- 2,565
- 4,426
Wadau wa uga huu wa kisheria naomba msaada. Nilikuwa na kesi na mwajiri wangu baada ya kunitimua kazini kinyume na taratibu. Kesi ilisikilizwa nikashindwa mwajiri akakata rufaa. Hii ilikuwa 2010 kesi iliendelea ikafikia mwisho wakati wa kusoma hukumu ikaonekana kuna makosa kidogo ya kibinaadamu kuwa mwaka nilionza kazi haulingani na ule mwaka nilioandika wakati nafaili kesi. Hivyo jaji akaamuru mwajiri alete vithibisho vya lini nilianza kazi hii ilikuwa 2011 mwishoni. Hadi naandika leo hii sijawahi kuletewa summons na nikienda CMA ni kizunguzungu je hadi leo hii ile kesi itakuwepo kweli naomba kujua kisheria kesi inakaa muda gani hadi kutupiliwa mbali.
Sent from my BlackBerry using JamiiForums
Sent from my BlackBerry using JamiiForums