Msaada Wa kisheria katika hili tafadhali

mjenziwakale

JF-Expert Member
Sep 24, 2015
671
824
Habari zenu wakuu,
Kuna mtu tulikubaliana aniuzie kiwanja kwa bei ya Tsh milioni 8, nikamlipa hela ya awali milioni 3.6, tukakubaliana kiasi kilichobaki ntakimalizia ndani ya miezi 6.Kwa Bahati mbaya nilikwama sikuweza kumalizia deni baada ya hiyo miezi 6 kutimu, tukaandikishana kwa Mjumbe kwamba hicho kiwanja atafutwe Mteja mpya kiuzwe katika uwepo wetu sote alafu na Mimi nipewe pesa yangu na wakati huo Wa kumtafuta Mteja ikitokea nikapata pesa naweza nikaenda kumalizia deni langu.
Baada ya miezi kama miwili nikawa nimepata hiyo pesa nikafanya mawasiliano na muuzaji ili nimlipe ,matokeo yake akawa ananikwepa baadae nkipata taarifa kuwa hicho kiwanja kimeshauzwa pasipo Mimi kuwepo hivo sikupewa pesa yangu.

Baada ya hapo nikaenda serikali za mitaa kufungua malalamiko na jamaa akakiri kukiuza hcho kiwanja ila akasema muda huo ana Tsh milioni moja akawa amenipatia hiyo hela na akaahidi kulipa ndani ya miezi mitatu pesa ilobaki na akawa ameweka dhamana ya eneo lake lingine kwamba asipolipa hilo eneo liuzwe na Mimi nipewe hela yangu.

Sikuishia hapo nkaamua niende Baraza la Ardhi la kata yakatolewa maamuzi hayo hayo kwamba hela yangu atanilipa ndani ya miezi mitatu vinginevyo hilo eneo liuzwe nipewe pesa yangu.

Madukuduku yangu ni haya yafuatayo......
1. Endapo jamaa akishindwa kunilipa pesa zangu ndani ya miezi hiyo mitatu ,Je ni nani atakuwa na jukumu la kusimamia na kuuza hiyo dhamana yake na kuhakikisha napata haki yangu?

2. Je asipopatikana Mteja Wa kununua hiyo dhamana ,suala la malipo yangu litakuaje ?

3.Je suala hili naweza kulipeleka mahakamani katika kipindi hiki cha kusubiria hii miezi mitatu mahakama labda inaweza kua na maamuzi zaidi.

Natanguliza shukrani zangu za dhati
 
Kwa upande wangu nakushauri usijali mkuu kama mmeshaandikishana kila kitu wewe subiria tu...haki yako itapatikana wala usijali... Baraza la ardhi, wajumbe wa mtaa na Mahakama ipo utatetewa ili mradi vithibitisho vipo na mmeandikishana..

Ngoja wajuzi zaidi waje mkuu kwa maelezo zaidi
 
Kwa upande wangu nakushauri usijali mkuu kama mmeshaandikishana kila kitu wewe subiria tu...haki yako itapatikana wala usijali... Baraza la ardhi, wajumbe wa mtaa na Mahakama ipo utatetewa ili mradi vithibitisho vipo na mmeandikishana..

Ngoja wajuzi zaidi waje mkuu kwa maelezo zaidi
Nashukuru sana mkuu kwa kutenga muda wako kusoma na kulielewa bandiko langu na kunipatia ushauri huu kwenye kunitia moyo, shukrani sana kiongozi
 
Majibu


1. Serikali za mitaa
2. Itatafutwa mali nyingi ya mhusika kadri balaza la ardhi litakavyoona inafaa.
3. Hapana hauwezi kulipeleka mahali pengine ilihali ulikubaliana na maamuzi ya balaza la ardhi
Ahsante mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom