Msaada wa kisaikolojia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kisaikolojia

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Averos, Jun 14, 2011.

 1. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Wanajamvi, naomba mnisaidie ni kitu gani kinatengeneza tabia ya mtu, yaani mwngine anakuwa mkali, mwengine mpole, mwengine bahili, mwengine mpenda makuu, mwengine mchafu, mwenigne mtanashat, mwengine katili, mwengine mlafi, mchoyo, mroho, na tabia nyenginezo kama uwongo, ukweli, umbea na kadhalika.
   
 2. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Wanajamvi naomba msaada wa kujua sababu ya binadamu kuwa na tabia mbalimbali kama uvivu, ukarimu, ushujaa, umbea, upole, ukali, uwongo, kupenda sifa na kadhalika.
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  binadamu ni kama wanyama wengine tu, kuna tabia za kurithi (za kuzaliwa nazo) na kuna tabia za kufunzwa, na ndio maana si ajabu una kuta watoto wa familia moja waliolelewa malezi ya wazazi wamoja lakini wanatofautiana kitabia
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Tabia hizo hurithiwa na zingine hutokana na mazingira unayoishia. Pia tabia zingine hutegemea context kwa mfano, namna nitakavyobehave nikiwa kwenye nyumba ya ibada ni tofauti na namna nitakavyobehave nikiwa club.
  Kwahiyo hapo ni sababu 3. Wengine watajazia.
   
 5. s

  shukia Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabala ya kugusia nini chanzo za tabia tulizo nazo ningependa nitoe maana fupi ya tabia: Tabia ni jumla ya matendo yote ayafanyayo mtu ama mnyama. Mambo haya yanajumuisha yale tunayoyaona kwa macho (mfano kula, kulala, kunywa, kutembea, kukonyeza, kuua, kuiba, kupigana, kusoma, nk) na yale tusiyoyaona kwa macho, mfano kufikiri, hisia zetu nk. Mambo makubwa mawili yanayofanya tuwe na tabia tulizo nazo
  1. Urithi kutoka kwa wazazi wetu kibailojia.
  2. Mazingira. Unapozungumzia mazingira unaangalia mambo mengi, mfano, watu wanaotuzunguka. Mtu anaweza akaiga tabia za mtu mwingine, misukumo (pressure) kutoka kwa watu wangu, malezi, ugumu wa mazingira tunamoishi, kiwango cha elimu nk. Kwa ujumla mazingira ni mambo yote ambayo sio ya kibaiolojia. Hope imekupa mwanga. For more information: yombwe2001@yahoo.co.uk
   
Loading...