Msaada wa kisaikolojia unahitajika

Aisee πŸ˜€
 
Demu anaelala nje ya kwao week nzima, unaanzaje kumpenda.?
 
Duh,pole sana mkuu,wanawake wapumbavu kama Hawa ndo wanawafanya single mothers wasiaminioe,hata wale wenye Nia njema na wanaojitambua,limtu linapendwa then analeta ujinga,mkuu mwache aende ila atakuja jutia upendo wako kwake,hatapata wa kumpenda kama ww trust me
 
True
 
Huu ndio ukweli
 
Hapo ulikuwa sahihi mkuu
 
Siku 3 zote hizo kwani kafiwa?

Ampotezee ndani ya robo saa akiwa serious atakua kashamsahau
 
Facts
 
alikwambia baba mtoto kafa alijupeleka kaburini ukajiridhisha jina la kaburini na la cheti cha mtoto ni sawa?!? if not umeliwa..

suala la pili shukuru umeachwa salama bila magonjwaa maana huyo angekuja kukuua nayo siku jwa jinsu anaonekana mtaalam wa draft..

move on mwana, wanawake wako kibwena tena wazuuuuuri hata hawajazalishwa!
 
Dogo ebu kua serious na maisha unakosa usingizi sababu ya mbususu!!!
 
Kiufupi ni hivi huyo jamaa na binti hawajaanza leo wala jana, inaonekana wakati ambao ulikuwa naye huyo jamaa alikuwa mbali naye na hivyo karudi. Kimaana nyingine hapo ushaachwa, hakuna mapenzi tena na hata kama akirudi kutoka kwa huyo jamaa baada ya kuachana. Basi elewa ipo siku atakupiga tukio kama hilo na kuondoka tena.

Hivi sasa unachotakiwa kufanya ni kukubali umepoteza, huwezi kuwa nayee tena. Unaumia sababu bado moyo wako haupo tayari kukiri hilo, na ukiendelea kuwa hivyo itakuletea maradhi makubwa ikiwemo presha, utakuja kuingia kwenye ulevi wa kupindukia au uvutaji sigara uliyopitiliza.

MOVE ON FOR YOUR OWN GOOD, hali kama yako ishawahi kunikuta nikiwa chuo hadi nikaja kupata sup mbili za kizembe mwaka wa mwisho na nikaja kukaribia kuboronga project yangu. Ila niliokolewa na kitu cha kwanza nilichotakiwa kukifanya ni hicho.

Pia hakikisha unaondoa kumbukumbu zote ambazo zinazoweza kukufanya ukamkumbuka, kuanzia picha hadi mawasiliano yake na ufanye kama hukuwahi kukutana naye kabla. Kumbukumbu zake zikitoka ni rahisi sana kumsahau.

Pia usipende kukaa peke yako mara kwa mara, hakikisha ni mtu wa kujichanganya sana lakini usiangukie kampani za ulevi au uvutaji sigara. Muda huu una kidonda cha kuumizwa zitakuharibu kabisa.

Nakuomba umnyamazie kimya usimtafute yeyote wala kumlalamikia kitu, hata huko ofisini ukikutana jifanye kama hukuwahi kumwona kabla na hakuna kitu kati yetu. Na usijioneshe ni mwenye mawazo kwake, wewe endele na mambo yako kama kawaida. Hakikisha anakuona haupo sawa na haujaathiriwa na lolote.

Kama mlishachumbiana na ukalipa gharama zingine samehe na endelea na mambo mengine kama vile hakijatokea kitu. Mambo ya kudai vitu ni ya kishamba hayo, waachie kila kitu.

Pia usije ukatafuta mwanamke mwingine kwa lengo la kumkomoa ili ajue nawe umepata, muda huu ambao haupo sawa unatakiwa ufanye ishu zingine zote kasoro hayo mambo. Maana hautapata unayemtaka zaidi ya kukurupuka tu na kuchukua yeyote.

Mwisho kabisa nakushauri umshukuru Mungu sana amekuonesha huyo mwananke jinsi alivyo mapema, hafai kuweka ndani na ni wa kuishi tu bila mume. Hili ni onyo lake amekupa, ili uachane naye na kuangalia kingine. Aliyekuumba amekuokoa na janga, sasa wewe hakikisha unajiepusha nalo usije ukakimbilia kulivaa tena. Hata akirudi kwako analia amepiga magoti usije kukubali katu kurudiana naye, ukidanganyika basi elewa utakuja kulia machozi ya damu.

Hukupangiwa kuishi naye na kumuoa huyo, wewe shukuru Mungu kwa kukuokoa mapema. Ukiona maumivu basi elewa ni jambo jema amekuandalia sasa usikimbilie alichokuepusha nacho.

Pia siku nyingine ukija kupata mzuri wa tabia na kila kitu, hakikisha hajui ni namna gani na usimpe attention kubwa. Vinginevyo atakusumbua sana na kukuhangaisha
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…