Msaada wa kisaikolojia unahitajika

Msaada wa kisaikolojia unahitajika

Afu kwa mfano on my case ni kwamba

Huyu x wake me sikuwahi jua kuwa walikuwa na mahusiano kuna siku nimekaa na huyo bwana akaanza kumkandia dem kamkandia sana tena mbele ya watu wazito tu...
As a man wala sikutaka hata yule mwanamke anote kuwa kuna kitu tumeongea na huyo mtu huezi amini nlisafiri mkoani nlivorudi nliwakuta wana urafiki wa karibu sana 😀 hatimaye wamekuwa pamoja tena. Sema muda nimeamaua kukubali yaishe nkamuonea binti huruma coz huyo mwamba ni mume wa mtu 😀😀😀

Katika yooote wanaume lazima tuwe na vumba la kutosha linapunguza sana stress za mapenzi na linapunguza possibility za kupigwa tukio.

Ujue ukiwa na pesa hata tukio lenyewe unapigwa kama unaombwa hivi 😀😀😀
Aisee 😀
 
Habari zenu wakuu.
Mwenzenu yamenikuta, naombeni msaada namna ya kucontrol hii hali.

Mimi ni kijana wa 34yrs hv, nilikua na mahusiano na mdada mmoja ambae kwangu alikua rafiki, mshkaji na kama ndugu. Yeye ana 31yrs ana mtoto mmoja ambae baba wa mtoto ni marehemu.

Twende kwenye kisa, mahusiano haya yalikua serious kidogo na tulikua na mipango ya kukamilisha taratibu zote mwishoni mwa mwaka huu ili ndoa ifanyike.

Sasa wakuu kisa cha kunileta kwenu kupata ushauri imetokea BREAK UP YA GHAFLA SANA, jambo ambalo linaniumiza sana sina utulivu kisaikolojia.
Moyo wangu unadunda kupita kawaida, sina hamu ya kula, usingizi shida na ufanisi wangu katika kazi umepungua mno.
Kusema ukweli huyu mwanamke nilimpenda sana nae alionesha kunipenda na kunijali sana kwa namna alivyokuwa akifanya kwa muda mfupi ambao nimekua nae.

Kwanza yeye alikua anaishi kwa wazazi wake na nilikua na mazoea ya kumtembelea na ndugu zake tunafahamiana.
Alikua anatoka kazini na kuelekea kwao ama wakati mwingine anakuja kwangu, anaweza akakaa wiki zima kisha anarudi tena kwao weekend.
Sasa wiki iliyopita aliniaga juu kwa juu akiwa kazini akisema anaenda kwao ameitwa na mama yake mkubwa, nikasema sawa.

Tangu jioni ile mawasiliano yakawa ya shida sana, ilikua siku ya Alhamisi. Basi nikajua Ijumaa atakuja maana kwa kipindi hiki ni mfululizo wa mwezi mzima alikua hapa kwangu. Mara Ijumaa ikapita, Jumamosi, Jumapili mpaka namwona Jumatatu.

Anakuja amebadilika yuko serious sana si kama nilivyomzoea ananiambia ana mambo ya kuongea nami mengi sana, nikasema sawa keti tuongee. Yuko busy na simu.
Nikachukua simu nikaweka pembeni. Namwambia tuongee hana cha kusema mara anaanza kukusanya nguo zake.
Vipi tena?

Anasema nataka nichukue nguo za mtoto, nikiangalia anakusanya nguo za mtoto plus kuchanganya na zake. Basi nikatulia nijionee, akamaliza lile zoezi akaanza kuaga, nikamwambia mbona leo mapema mapema? Maana kwa kawaida hata kama amekuja na kuondoka same day huwa anaondoka jioni kabisa sasa siku hiyo nikasmell something fish.

Nikataka kuchukua simu, nione mawasiliano ya mle akawa mbishi kidogo akidai kuna msg sitaki usome humo. Msg gani akasema kuna vitu vya siri tumechat na mama. Nikamwambia its okay, text za mama mimi sisomi akaniacha.
Kuanza kusoma kuna namba ngeni imetext mara nyingi ikiita mke wng.. mke wng, na last text ya kwake ametuma ikisema chaji inaisha simu inazima soon!

Daaah, nikasema huyu mwamba atakua ndie anaemrubuni. Nikachukua namba, nikaweka kwa simu yangu. Akaaga na kutoka, sikumtoa kbs. Nikaipiga ile namba jamaa akapokea, nikamuuliza kuhusu mhusika akajibu anamfahamu ni mtu wake kitambo na alikua nae tangu Alhamis jioni na kaacha mtoto kwake hata ule muda tunaongea ameaga anaenda Serikali za mtaa.

Basi nikamwambia nashukuru, nilitaka tu nijue hilo maana sioni busara kuanza kugombea mwanamke. Tukaishia.

Sasa kinachoniumiza ni situation ilotokea kwa ghafla na mwanamke amenitext leo kuonesha kujutia, nikasema km ni kweli ngoja nijiridhishe aliko leo. Baada ya kutoka kazini nikachukua usafiri mpaka kwao, huku tunachat.

Nimefika nikamuuliza uko wapi? Anashindwa kujibu, mara anauliza kwani umeniona wapi?
Nikajua shits goes on! Nimerudi zangu home nimetulia ila sipo sawa kabisa.

Wataalam wa hizi incidents nifanyeje ili nikae sawa bila kuangukia kwenye mambo ya kunidhoofisha kiakili na kiafya?

Nawasilisha.
View attachment 2496610
Duh,pole sana mkuu,wanawake wapumbavu kama Hawa ndo wanawafanya single mothers wasiaminioe,hata wale wenye Nia njema na wanaojitambua,limtu linapendwa then analeta ujinga,mkuu mwache aende ila atakuja jutia upendo wako kwake,hatapata wa kumpenda kama ww trust me
 
Unaumiza kichwa kwa kusalitiwa na malaya? Shukuru Mungu umemjua kabla haujafanya maamuzi magumu ya kumuweka ndani.

Kinachoonekana wewe umempenda sana huyo singo maza zaidi ya yeye alivyokupenda na ameshajua. Hutokuja kuacha kuona kila rangi hapo. Atakupeleka msobe msobe na utakuja na thread nyingi sana za malalamiko humu.

She is for the streets. Tafuta mwanamke wako utulie nae. Huyo hata ukija kumuoa utachapiwa sana! Hajakupenda!
True
 
Haikuwa rizikyako na Wala haikupangwa awe wako

Kujiumiza kwaajili ya mtu ambae ankula anashiba na analala Kwa mwanaume mwenzio ni matumiz mabaya ya akili relax kubali tu yaishe Kula vizuri vaa vizuri fanya kazizako vizuri ukipata muda enjoy life is too short
Ukijipa thamani sikutatu zinatosha kumsahau
Huu ndio ukweli
 
Nimesoma huu uzi moyo ukaanza kwenda mbio utadhan mi ndiye mtendwa. Anyway, sijawahi kukutana exact situation kama hiyo, ila situation za mapenzi za kuumiza nshakutana nazo.

Like moja iliyowahi kunila sana ni manzi yangu wa muda mrefu alijazwa kibendi na mdau mwingine...ilinila si kidogo. Ila Sikuomba mtu ushauri. Maana najua katika mapenzi, hata ushauriwe vipi, mwamuzi wa mwisho ni wewe.

Ikabidi tuu nijipe muda. katikati ya maumivu hayo, nikachagua kujipa muda maana binafsi nilishindwa niamue nini. Alikuwa ni mwanamke ambae alifahamika hadi kwetu.

Yeye alikuwa tayari kuendelea na mimi maana hata aliyemjaza kibendi alimchinjia baharini. Mtihani kwangu ulikuwa ni kuamua niendelee nae tu au nipotezee...nilimpenda sana.

Hatimaye muda ukajibu. Nikajikuta nimepata ujasiri wa kumtamkia SIKUTAKI. Na hapo moyo wangu ulikuwa wazi kabisa kwamba simtaki. Alilia nakunibembeleza kwa kila meseji. Mimi muda ulishaniponya, hakufanikiwa.

Alifanikiwa kujifungua mtoto wa kike. Ilikuwa 2015 hiyo. And as i speak ni single maza.

Mimi baada ya muda mrefu nikafanikiwa kupata my match. Katoto flani kabichi kabisa, nikawanako in relation kwa miaka mingi, kakanifurahisha, nikakaoa, saii tuko na 3yrs boy na kibendi kingine.

So chakukushauri hapo 'TAKE YOUR TIME'. Maamuzi sahihi yanahitaji muda sahihi.
Hapo ulikuwa sahihi mkuu
 
Haikuwa rizikyako na Wala haikupangwa awe wako

Kujiumiza kwaajili ya mtu ambae ankula anashiba na analala Kwa mwanaume mwenzio ni matumiz mabaya ya akili relax kubali tu yaishe Kula vizuri vaa vizuri fanya kazizako vizuri ukipata muda enjoy life is too short
Ukijipa thamani sikutatu zinatosha kumsahau
Siku 3 zote hizo kwani kafiwa?

Ampotezee ndani ya robo saa akiwa serious atakua kashamsahau
 
Afu kwa mfano on my case ni kwamba

Huyu x wake me sikuwahi jua kuwa walikuwa na mahusiano kuna siku nimekaa na huyo bwana akaanza kumkandia dem kamkandia sana tena mbele ya watu wazito tu...
As a man wala sikutaka hata yule mwanamke anote kuwa kuna kitu tumeongea na huyo mtu huezi amini nlisafiri mkoani nlivorudi nliwakuta wana urafiki wa karibu sana 😀 hatimaye wamekuwa pamoja tena. Sema muda nimeamaua kukubali yaishe nkamuonea binti huruma coz huyo mwamba ni mume wa mtu 😀😀😀

Katika yooote wanaume lazima tuwe na vumba la kutosha linapunguza sana stress za mapenzi na linapunguza possibility za kupigwa tukio.

Ujue ukiwa na pesa hata tukio lenyewe unapigwa kama unaombwa hivi 😀😀😀
Facts
 
alikwambia baba mtoto kafa alijupeleka kaburini ukajiridhisha jina la kaburini na la cheti cha mtoto ni sawa?!? if not umeliwa..

suala la pili shukuru umeachwa salama bila magonjwaa maana huyo angekuja kukuua nayo siku jwa jinsu anaonekana mtaalam wa draft..

move on mwana, wanawake wako kibwena tena wazuuuuuri hata hawajazalishwa!
 
Habari zenu wakuu.
Mwenzenu yamenikuta, naombeni msaada namna ya kucontrol hii hali.

Mimi ni kijana wa 34yrs hv, nilikua na mahusiano na mdada mmoja ambae kwangu alikua rafiki, mshkaji na kama ndugu. Yeye ana 31yrs ana mtoto mmoja ambae baba wa mtoto ni marehemu.

Twende kwenye kisa, mahusiano haya yalikua serious kidogo na tulikua na mipango ya kukamilisha taratibu zote mwishoni mwa mwaka huu ili ndoa ifanyike.

Sasa wakuu kisa cha kunileta kwenu kupata ushauri imetokea BREAK UP YA GHAFLA SANA, jambo ambalo linaniumiza sana sina utulivu kisaikolojia.
Moyo wangu unadunda kupita kawaida, sina hamu ya kula, usingizi shida na ufanisi wangu katika kazi umepungua mno.
Kusema ukweli huyu mwanamke nilimpenda sana nae alionesha kunipenda na kunijali sana kwa namna alivyokuwa akifanya kwa muda mfupi ambao nimekua nae.

Kwanza yeye alikua anaishi kwa wazazi wake na nilikua na mazoea ya kumtembelea na ndugu zake tunafahamiana.
Alikua anatoka kazini na kuelekea kwao ama wakati mwingine anakuja kwangu, anaweza akakaa wiki zima kisha anarudi tena kwao weekend.
Sasa wiki iliyopita aliniaga juu kwa juu akiwa kazini akisema anaenda kwao ameitwa na mama yake mkubwa, nikasema sawa.

Tangu jioni ile mawasiliano yakawa ya shida sana, ilikua siku ya Alhamisi. Basi nikajua Ijumaa atakuja maana kwa kipindi hiki ni mfululizo wa mwezi mzima alikua hapa kwangu. Mara Ijumaa ikapita, Jumamosi, Jumapili mpaka namwona Jumatatu.

Anakuja amebadilika yuko serious sana si kama nilivyomzoea ananiambia ana mambo ya kuongea nami mengi sana, nikasema sawa keti tuongee. Yuko busy na simu.
Nikachukua simu nikaweka pembeni. Namwambia tuongee hana cha kusema mara anaanza kukusanya nguo zake.
Vipi tena?

Anasema nataka nichukue nguo za mtoto, nikiangalia anakusanya nguo za mtoto plus kuchanganya na zake. Basi nikatulia nijionee, akamaliza lile zoezi akaanza kuaga, nikamwambia mbona leo mapema mapema? Maana kwa kawaida hata kama amekuja na kuondoka same day huwa anaondoka jioni kabisa sasa siku hiyo nikasmell something fish.

Nikataka kuchukua simu, nione mawasiliano ya mle akawa mbishi kidogo akidai kuna msg sitaki usome humo. Msg gani akasema kuna vitu vya siri tumechat na mama. Nikamwambia its okay, text za mama mimi sisomi akaniacha.
Kuanza kusoma kuna namba ngeni imetext mara nyingi ikiita mke wng.. mke wng, na last text ya kwake ametuma ikisema chaji inaisha simu inazima soon!

Daaah, nikasema huyu mwamba atakua ndie anaemrubuni. Nikachukua namba, nikaweka kwa simu yangu. Akaaga na kutoka, sikumtoa kbs. Nikaipiga ile namba jamaa akapokea, nikamuuliza kuhusu mhusika akajibu anamfahamu ni mtu wake kitambo na alikua nae tangu Alhamis jioni na kaacha mtoto kwake hata ule muda tunaongea ameaga anaenda Serikali za mtaa.

Basi nikamwambia nashukuru, nilitaka tu nijue hilo maana sioni busara kuanza kugombea mwanamke. Tukaishia.

Sasa kinachoniumiza ni situation ilotokea kwa ghafla na mwanamke amenitext leo kuonesha kujutia, nikasema km ni kweli ngoja nijiridhishe aliko leo. Baada ya kutoka kazini nikachukua usafiri mpaka kwao, huku tunachat.

Nimefika nikamuuliza uko wapi? Anashindwa kujibu, mara anauliza kwani umeniona wapi?
Nikajua shits goes on! Nimerudi zangu home nimetulia ila sipo sawa kabisa.

Wataalam wa hizi incidents nifanyeje ili nikae sawa bila kuangukia kwenye mambo ya kunidhoofisha kiakili na kiafya?

Nawasilisha.
View attachment 2496610
Dogo ebu kua serious na maisha unakosa usingizi sababu ya mbususu!!!
 
Kiufupi ni hivi huyo jamaa na binti hawajaanza leo wala jana, inaonekana wakati ambao ulikuwa naye huyo jamaa alikuwa mbali naye na hivyo karudi. Kimaana nyingine hapo ushaachwa, hakuna mapenzi tena na hata kama akirudi kutoka kwa huyo jamaa baada ya kuachana. Basi elewa ipo siku atakupiga tukio kama hilo na kuondoka tena.

Hivi sasa unachotakiwa kufanya ni kukubali umepoteza, huwezi kuwa nayee tena. Unaumia sababu bado moyo wako haupo tayari kukiri hilo, na ukiendelea kuwa hivyo itakuletea maradhi makubwa ikiwemo presha, utakuja kuingia kwenye ulevi wa kupindukia au uvutaji sigara uliyopitiliza.

MOVE ON FOR YOUR OWN GOOD, hali kama yako ishawahi kunikuta nikiwa chuo hadi nikaja kupata sup mbili za kizembe mwaka wa mwisho na nikaja kukaribia kuboronga project yangu. Ila niliokolewa na kitu cha kwanza nilichotakiwa kukifanya ni hicho.

Pia hakikisha unaondoa kumbukumbu zote ambazo zinazoweza kukufanya ukamkumbuka, kuanzia picha hadi mawasiliano yake na ufanye kama hukuwahi kukutana naye kabla. Kumbukumbu zake zikitoka ni rahisi sana kumsahau.

Pia usipende kukaa peke yako mara kwa mara, hakikisha ni mtu wa kujichanganya sana lakini usiangukie kampani za ulevi au uvutaji sigara. Muda huu una kidonda cha kuumizwa zitakuharibu kabisa.

Nakuomba umnyamazie kimya usimtafute yeyote wala kumlalamikia kitu, hata huko ofisini ukikutana jifanye kama hukuwahi kumwona kabla na hakuna kitu kati yetu. Na usijioneshe ni mwenye mawazo kwake, wewe endele na mambo yako kama kawaida. Hakikisha anakuona haupo sawa na haujaathiriwa na lolote.

Kama mlishachumbiana na ukalipa gharama zingine samehe na endelea na mambo mengine kama vile hakijatokea kitu. Mambo ya kudai vitu ni ya kishamba hayo, waachie kila kitu.

Pia usije ukatafuta mwanamke mwingine kwa lengo la kumkomoa ili ajue nawe umepata, muda huu ambao haupo sawa unatakiwa ufanye ishu zingine zote kasoro hayo mambo. Maana hautapata unayemtaka zaidi ya kukurupuka tu na kuchukua yeyote.

Mwisho kabisa nakushauri umshukuru Mungu sana amekuonesha huyo mwananke jinsi alivyo mapema, hafai kuweka ndani na ni wa kuishi tu bila mume. Hili ni onyo lake amekupa, ili uachane naye na kuangalia kingine. Aliyekuumba amekuokoa na janga, sasa wewe hakikisha unajiepusha nalo usije ukakimbilia kulivaa tena. Hata akirudi kwako analia amepiga magoti usije kukubali katu kurudiana naye, ukidanganyika basi elewa utakuja kulia machozi ya damu.

Hukupangiwa kuishi naye na kumuoa huyo, wewe shukuru Mungu kwa kukuokoa mapema. Ukiona maumivu basi elewa ni jambo jema amekuandalia sasa usikimbilie alichokuepusha nacho.

Pia siku nyingine ukija kupata mzuri wa tabia na kila kitu, hakikisha hajui ni namna gani na usimpe attention kubwa. Vinginevyo atakusumbua sana na kukuhangaisha
 
Back
Top Bottom