Msaada wa kisaikolojia: Nawaogopa wasichana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kisaikolojia: Nawaogopa wasichana

Discussion in 'JF Doctor' started by mark11, Dec 17, 2011.

 1. m

  mark11 Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari jf

  Mimi ni kijana umri miaka 25. Niliwahi kua na mpenzi wa kike kwa miaka 6 mpaka July mwaka huu. Nilitokea kumpenda sana, nikamjali kwa kila kitu. Mambo mengi yalikua yakitokea nikavumilia lakini ikafikia hatua siku moja ukatokea ugomvi. Nili hack akaunti yake ya yahoo nikafanikiwa kuingia ktk akaunti yake ya facebook(baada ya kuhisi naibiwa kutokana na dharau za wazi alizokua akinionesha)

  nilichokuta fb kilinistua sana, nikajaribu kufatilia kwa jamaa wa kwanza. Basi my x akapata habari na kuamua kunipgia simu. Kilichofata hapo ni yeye kunitukana na kunipa ukweli kua amekua na wanaume 13 tofauti kwa muda wa miaka 6 wakati niko nae na akawataja majina.

  nilistuka sana hasa kwa vile hakuna kitu ambacho alikosa kwangu. Pia kwa kua nilimpenda kwa moyo wangu wote hata ndugu na marafiki walikua wanajua

  nikafanya maamuzi magumu, kumuacha. Tatizo limekuja kua karibu kila siku lazima nikumbuke tukio hilo kwa muda wote huu tangu july. Nikiwaona wasichana napata hasira / naogopa hata kuwasalimia kwa kuwaona ni watu wabaya na wasiofaa.
  Nimehangaika sana na hali hii na najua navyowafikiria sivyo. Msaada wana jf, nifanyeje maisha yangu yarudi ktk hali ya kawaida?
   
 2. GABOO

  GABOO Senior Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole kwa kutendwa,inabidi umuombe mungu akupe nguvu uweze kusahau na kusamehe,ukiweza haya hutoogopa tena wasichana.
   
 3. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,164
  Likes Received: 10,512
  Trophy Points: 280
  du pole sana. ngoja wataalam wanakuja.
   
 4. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  karibu leo jioni tupate supu na bia mbilimbili halafu nimealika rafiki zangu wa kike watano na washikaji, tunasherehekea birthday ya mshikaji. ishu ni wewe kujichanganya na uwazoee tu kama binadamu, chuki si nzuri. mapenzi ni game of dynamics/tricks na haina formula. karibu, wanywa whysky, lager, soda nk
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Una uhakika gani hamna alichokosa?
  Yeye tu ndo mwenye uhakika kama alikosa kitu au alipata kila kitu.

  Nwy, kitu cha kwanza kinachoweza kukusaidia ni wewe kutafuta vitu ambavyo vitatumia muda wako mwingi badala ya kukaa tu na kufikiria yaliyokukuta.Fanya kazi, tafuta hobby, jichoshe ukipanda kitandani unazima.

  Pili jitahidi kuzungukwa na watu ambao ni positive na wanaokufurahisha. Epuka kuongelea hilo swala kila mara.

  Spend time with your lady relatives, hii itakusaidia kuona wasichana sio wabaya bali "baadhi ya wasichana ni wabaya". . . pia itakusaidia kupunguza chuki uliyonayo.

  Nna vitu kama viwili vitatu hivi ukifanya vinaweza kukusaidia, kama unataka kushiriki nijulishe.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  na dhahiri kuwa unahitaji ushauri nasaha. lakini hata kama hautapata ushauri huo, usihofu, baada ya muda utapona tu hilo tatizo lako. Imeshatutokea watu wengi na over time inajirekebisha yenyewe hasa pale ambapo unakutana na mwingine utakayempenda zaidi ya yule aliyekuvunja moyo. kama ukiona miaka ikatika na hakuna mabadiliko katika hali yako, watafute washauri nasaha... kuna shangazi anaitwa anti Sadaka, yupo pale House of talents, ni mzuri sana kwa masuala hayo
   
 7. m

  mark11 Member

  #7
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahsante Lizzy kwa ushauri wako. Ndio nahitaji kushiriki. Naomba unicheki ktk jamaaflani@gmail.com
   
 8. m

  mark11 Member

  #8
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu akubariki kwa ushauri wako, nitaenda kuonana nae
   
 9. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni vigumu sana kusahau kuliko kusamehe. Jaribu kutokuwa na hasira ndugu kwani kufanya hivyo, kunaweza kukuvurugia mahusiano mengine. Pia kumbuka kuwa kufanya mambo tofauti na unavyofanya siku zote kunaweza kukusaidia haraka kusahau yaliyopita.
   
 10. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ndio ukubwa huo... Vibuti ni kawaida sana ... Kama hiki ndio kibuti cha kwanza lazima roho iume jipe muda utapata mwengine ...
   
 11. sixlove

  sixlove Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  ndo kwaida yao hao hawana fair play
   
Loading...